Maonesho ya urejesho wa taji kwa Bikira ya Raphael kutoka Makumbusho ya Vatican hadi Perugia
Vatican News
Baada ya karne mbili, kuwekwa taji kwa Bikira, iliyotengenezwa na mchoraji Raphael Sanzio na kukamilishwa na wanafunzi wake Giulio Romano na Giovan Francesco Penni kwa Kanisa la Mtakatifu Maria Mpalizwa Mbinguni huko Monteluce, Picha hiyo inarudi kwenye maonesho huko Perugia. Kwa njia hiyo “Urejesho uliosubiriwa: Kuanzia kwa Rapahaeli hadi Monteluce kutoka Jumba la Makumbusho Vatican itakuwa maonesho yatakayoanza Septemba 24 hadi tarehe 7 Januari 2026, kwenye Jumba la Makumbusho la Kanisa Kuu la Mtakatifu Lorenzo huko Perugia nchini Italia, katika Uwanja wa IV Novemba, Perugia).
Kazi hiyo, ambayo awali ilichorwa kwa ajili ya makazi ya kale ya kimonaki ya Waklara Maskini, inakuja jijini kutokana na ushirikiano wa Jimbo Kuu la Perugia-Città della Pieve na Makumbusho ya Vatican. Kwa mara ya kwanza, itaoneshwa pamoja na predella na historia kutoka katika maisha ya Maria, iliyochorwa na Berto wa Giovanni, kwa mkopo kutoka Jumba la Makumbusho ya Umbria. Maonyesho hayo yanaongoza wageni kwenye safari ya kugundua kazi inayozunguka mipaka kati ya fikra ya Mwalimu na nguvu, kati ya kufungwa na jiji, kati ya historia ya sanaa na kiroho. Picha mahususi, ambapo kwa Kupalizwa na Kuwekwa taji huunganishwa katika wakati mmoja wa ukumbusho uliojaa utukufu, maajabu, na matumaini, unasimuliwa kwa kuonekana kwa nguvu ya ukuta wenye rangi. Kupitia uwiano sawia na utofautishaji stadi, ubora ulioboreshwa wa na eneo la kazi ya Raphael ambayo hujitokeza.
Nuru ya dhahabu ya anga huweka taji ya rangi ya samawati inayoongoza ya mwangaza wa mawingu wa mandhari ya nyuma na aina mbalimbali za mavazi ya mitume ambao wamekuja kutafakari muujiza duniani. Hii inafanyika shukrani kwa uwezekano wa msaada wa Mfuko wa Perugia, ambapo maonyesho ni fursa nzuri ya kuungana tena, baada ya karne nyingi kutokuwepo, vipengele vya mojawapo ya kazi muhimu zaidi kipindi cha kuzaliwa upya katika historia ya kisanii ya Perugia, ambayo ilichukuliwa na Askari wa Napoleon mwaka 1797. Katika moyo wa Jubile ya Matumaini, ni kurudi kwa muda mrefu sana uliotamaniwa.