Papa Leo XIV akutana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican tarehe 22 Agosti 2025 imebanisha kuwa “tarehe 22 Agosti 22025, Baba Mtakatifu Leo XIV alimpokea na kukutana katika Jumba la Kitume na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Bwana Wavel Ramkalawan.
Baadaye Rais Ramkalawan alikutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican, akiandamana na Monsinyo Miros?aw Stanis?aw Wachowski, Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa.
Mazingira, afya, elimu, mazungumzo
Wakati wa majadiliano ya ukarimu katika Sekretarieti ya Vatican yalionesha uhusiano mzuri kati ya Vatican na Shelisheli na mambo mbalimbali ya hali ya kisiasa na kijamii ya nchi yalijadiliwa, hasa ushirikiano na Kanisa la mahalia, katika nyanja za ulinzi wa mazingira, afya, na elimu, kwa kuzingatia hasa elimu ya vijana wa visiwa hivyo. Mazungumzo yaliendelea kwa kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa, yakisisitiza umuhimu wa kukuza mazungumzo na ushirikiano kati ya mataifa.
Zawadi kutoka kwa Baba Mtakatifu
Papa alimpatia Rais nakala msingi inayoonesha fumbo la Taalimungu ya mchoraji Raphael Sanzio inayopatikana katika chumba cha mihuri katika Makumbusho ya Vatican; mwanamke akiwa amezungukwa na makerubi wawili wenye maandishi "Divinar(um) rer(um) notitia," ikimaanisha taalimungu kama "ufunuo wa mambo." Zawadi zingine kutoka kwa Papa: kitabu cha Ghorofa ya Watazamaji katika Jumba la Kitume na Ujumbe kwa Siku ya Amani Ulimwenguni kwa mwaka 2025.
Zawadi kutoka kwa Rais
Rais wa Visiwa vya Shelisheli alimpa Papa mfano mdogo wa mtumbwi wa kawaida wa mbayo wa kuvua samaki kutoka kwenye visiwa.