Papa Leo XIV amemteua Mons.Eric Soviguidi kuwa Balozi wa Vatican nchini Burkina Faso
Vatican news
Baba Mtakatifu amemtua, Balozi mpya wa Burkina Faso, Mheshimiwa, Monsinyo Eric Soviguidi, ambaye hadi uteuzi huo, alikuwa ni Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Elimu, Sayansi na Utamaduni, na kumwinua wakati huo huo hadhi ya kuwa na Kiti cha Cartenza na Uskofu Mkuu.
Wadhifa wake:
Monsinyo Eric Soviguidi alizaliwa huko Abomey nchini Benin kunako tarehe 31 machi 1971. Alipewa daraja la Upadre kunako tarehe 10 Oktoba 1998, kwa ajili ya Jimbo katoliki la Cotonou. Ana shahada ya Sheria za Kanononi za Kanisa.
Alijiunga katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican kuna tarehe 1 Julai 2005 na kutoa huduma kwenye Balozi za Vatican kwa nchi kadhaa: Haiti, Ghana, Tanzania, Guatemala, Katika Kitengo Sekretarieti ya Vatican cha Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa na hatimaye alikuwa katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Elimu, Sayansi na Utamaduni kama Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican. Anazungumza pamoja na kuzungumza kifaransa, pia ni kiingereza, kiitaliano na kispanyola.