杏MAP导航

Tafuta

2025.07.11 Bustani ya Borgo Laudato Si 2025.07.11 Bustani ya Borgo Laudato Si 

Kipindi cha Uumbaji:“Ishara za uekumene katika Siku ya Uumbaji

Maadhimisho yatakayofunguliwa Septemba 1,yametiwa msukumo mwaka huu na maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kiekumene wa Nicea na ujumbe wa Papa kwa Siku hiyo,ambao mada yake-Mbegu za Amani na Matumaini iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko.

Vatican News

Tarehe Mosi  Septemba 2025  ni Siku ya Kuombe kazi ya Uumbaji. Wakristo Ulimwenguni wataungana katika maombi kwa sababu katika Kipindi cha kazi ya Uumbaji ni fursa ya kujiunga na juhudi nyingi za wale wanaofanya kazi ulimwenguni kote kwa ajili ya uongofu wa kiikolojia. Kipindi cha Kazi ya Uumbaji ni mpango wa kiekumene unaoadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 1 Septemba hadi tarehe 4 Oktoba, katika sikukuu ya Mtakatifu Fransisko wa Assis, na kuhamaishwa na kuungwa mkono na mashirika mbalimbali, yakiwemo Harakati  la Laudato Si', Baraza la Makanisa Ulimwenguni, Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni, na Usharika wa Kianglikan.

Borgo Laudato Si
Borgo Laudato Si

Mnamo 1989, Patriaki wa Kiekumeni Dimitrios I alitangaza Septemba 1 kuwa Siku ya Kuombea Kazi ya Uumbaji kwa Wakristo wa Kiorthodox. Baadaye, Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) lilirefusha sherehe hiyo hadi tarehe 4 Oktoba. Mnamo mwaka 2015, Papa Francisko alichapisha Waraka wa Kitume wa  Laudato Si' yaani “Sifa kwa Bwana” inayohusu utunzaji bora wa Mazingira, Nyumba yetu ya Pamoja na baadaye akaanzisha "Siku ya  Maombi Ulimwenguni  kwa ajili ya Utunzaji wa kazi ya Uumbaji." Katika Ujumbe uliochapishwa katika hafla hiyo kwa mwaka 2025, mada yake ni: "Mbegu za Amani na Matumaini," iliyochaguliwa na Papa Francisko. Zaidi ya hayo, Papa Leo XIV alitangaza Amri ya Misa kwa ajili ya Utunzaji wa Uumbaji, Missa pro custodia creationis, na yeye mwenyewe aliadhimisha Misa hiyo  tarehe 9 Julai 2025 katika Bustani ya Borgo Laudato Si' huko Castel Gandolfo.

Utunzaji wa kazi ya Uumbaji
Utunzaji wa kazi ya Uumbaji

Ili kuhuisha maadhimisho ya mwaka huu 2025, Baraza la Makanisa Ulimwenguni, ambacho ni chombo kinacholeta pamoja Makanisa ya Kiorthodox na Kiprotestanti, limetoa hata  video mpya kuhusu historia na ishara ya siku hii. Mabaraza mengi ya Maaskofu, hasa kusini mwa Ulimwengu, yanahimiza Parokia zao kusherehekea Siku hii kwa Misa kwa ajili ya Ulinzi wa kazi ya Uumbaji, kama itakavyokuwa nchini Ufilipino, kulingana na uthibitisho wa Monsinyo Gerardo Alminaza, Askofu wa Mtakatifu Carlos, na katika nchi nyingine za Amerika ya Kusini, kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu wa, Baraza la Maaskofu la Amerika ya Kusini(CELAM) Askofu  Estrada Herrera Lizardo, Askofu Msaidizi wa Cuzco. Mwaka 2025 ni kumbukumbu ya miaka miwili muhimu, awali ya yote kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea na kuchapishwa kwa  Waraka wa Laudato Si' baada ya miaka kumi iliyopita. Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WWC) limependekeza Siku ya kuombea Kazi ya  Uumbaji kama fursa ya kukumbuka umuhimu wa Imani katika Mungu, "Muumba wa mbingu na dunia," "ambaye kupitia yeye vitu vyote viliumbwa."

Mpango wa "Kipindi cha kazi ya Uumbaji" unaratibiwa kimataifa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni, linaloongozwa na Askofu Heinrich Bedford-Strohm, kwa ushirikiano na makanisa na washirika mbalimbali wa kimataifa. Ibada kwa njia ya  mtandaoni ya kuadhimisha Siku ya Uumbaji huandaliwa kila mwaka na kamati ya kiekumene na itawashirikisha Kardinali Fridolin Ambongo, rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar(SECAM), Askofu Atahualpa Hernandez, wa Kilutheri wa Colombia, na Mchungaji Hyunju Bae wa Kanisa la Presbyterian la Korea.

31 Agosti 2025, 19:05