Kard.Parolin:kinachoendelea Gaza kinashutua!
Vatican News
Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican mjini Napoli kwa Juma la 75 ya Liturujia Kitaifa akijibu maswali ya waandishi wa habari pembezoni mwa sherehe za uzinduzi kuhusu shambulio la bomu lililofanywa na Israel katika hospitali ya Nasser huko Khan Younis katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya watu 20 wakiwemo waandishi wa habari 5, alisema “Tunabaki kushangazwa na kile kinachotokea Gaza, licha ya kulaaniwa na dunia nzima, kwa sababu kuna kulaaniwa kwa kauli moja kwa kile kinachotokea.”
Kardinali Parolinaliongeza kusema: “Ni upuuzi”, akibainisha kwamba inaonekana "hakuna mwanga wa suluhosho na kwamba "hali inazidi kuwa ngumu na, kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu, inazidi kuwa hatari, pamoja na matokeo yote tunayoyaona daima." Kuhusu Ukraine, Katibu Mkuu wa Vatican, alisema kwamba “siasa nyingi zinahitajika, kwa sababu kuna masuluhisho mengi ya kinadharia na kuna njia nyingi zinazoweza kuchukuliwa ili kupata amani, lakini lazima tutake kuzitekeleza kwa vitendo na kwa wazi, mwelekeo fulani wa roho unahitajika pia.”
"Kuna hitaji la tumaini ulimwenguni kote," Kardinali Parolin alisema zaidi, akisisitiza kwamba Jubilei iliyotangazwa na Papa Francisko, iliyojitolea kwa mada hii, na inapaswa kuwa wakati wa kugundua tena matumaini. Tumaini dhidi ya matumaini yote, Kardinali huyo alisisitiza, ikizingatiwa kwamba leo hii hakuna vipengele vingi vinavyotusaidia kuwa na matumaini, hasa katika ngazi ya kimataifa," kama inavyoonekana hata siku hizi" kutokana na ugumu wa kuanzisha mchakato wa amani katika hali ya migogoro." Hata hivyo, "hatuhitaji kukata tamaa" na "kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya amani na upatanisho."