Kard.Parolin:Mtakatifu Monica awe mlinzi wa mama wote na kumkabidhi wanawake wanaoteswa!
Na Tiziana Campisi - Roma.
"Ningependa Mtakatifu Monica atangazwe kuwa 'Mlinzi wa wanawake, wake na akina mama wote,' kwa sababu maisha yake yalikuwa ni taswira hai juu ya ufundishaji." Haya ndiyo yalikuwa ni matakwa yaliyotolewa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa vatican wakati wa Ibada ya Misa Takatifu aliyoiongoza alasiri tarehe 27 Agosti 2025 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Agostino huko Campo Marzio, jijini Roma kwenye kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Monica Mama wa Askofu wa Hippo.
Walioadhimisha misa pamoja na Kardinali Parolin walikuwa ni Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino, Padre Alejandro Moral; Padre Joseph Farrell; Pronvinci wa Kiagostinai wa Italia, Padre Gabriele Pedicino; na Watawa wa mashirikia mengine. Basilika katika moyo wa mji ilikuwa imejaa wakati wa Liturujia ya Ekaristi iliyotanguliwa na Masifu ya jioni. Kwa mamia ya waamini waliokuwepo, Kardinali Parolin alimfafanua Monica kama kielelezo cha “mke na mama” kisha akaelekeza mawazo yake “kwa akina mama waliofiwa na watoto wao,” kwa wale waliotelekezwa na watoto wao, na wale ambao watoto wao “wamepotea katika dimbwi la dawa za kulevya,” au ni “wasio na kazi,” “gerezani,” “katika vita,” “wagonjwa,” na pia “mama ambao wana jambo la kumwomba Mungu kwa ajili ya watoto wao,” akiwakabidhi kwa Mtakatifu. "Lakini pia ningependa kukabidhi kwa Mtakatifu Monica wanawake wote wanaonyanyaswa na wanaume," Kardinali aliongeza, akiwahimiza watoto wa wakati wetu kutambua "zawadi isiyo na thamani" ya mama zao.
Kardinali Parolin katika sala kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Monica (ANSA)
Njia ya kufundisha ya Mama wa Mtakatifu Agostino
Katika Mahubiri hayo, Kardinali Parolin alikumbuka sifa za Monica, ambaye "alimbadilisha mume na mwanawe," hivyo akifundisha kwamba "wakati mtu hawezi kuzungumza juu ya Mungu kwa mume na watoto wake, lazima azungumze juu yao kwa Mungu." Hii ni kweli pia leo hii, Katibu Mkuu wa Vatican alisisitiza, akizungumzia vijana wengi walio mbali na imani. Wakati mtu hawezi kuzungumza nao juu ya Mungu, lazima azungumze juu yao kwa Mungu, alirudia, tena akionesha Monica kama mfano wa kuiga: "Siri ya ufundishaji wake iko katika imani yake katika ufanisi wa sala." “Ninahisi ujitoaji wa kipekee kwa Mtakatifu huyu,” Kardinali alisema kwamba siri ya ibada hiyo inashirikishwa na waamini wengi, kwa sababu “inakuja kwa kawaida” kumshirikisha Monica “na mama zetu, ambao hawakutupatia uhai wa kimwili tu, bali pia walitutunza, walitulea tukiwa Wakristo, na kusindikizana nasi hatua kwa hatua katika maisha yetu kwa upendo na sala zao.
Wakati wa Masifu ya jioni
Ushirikiano wa Kardinali Parolin kwa Shirika la Mtakatifu Agostino
Mwishoni mwa maadhimisho hayo, Kardinali Parolin alihusishwa na Shirika la Mtakatifu Agostino kwa "hangaiko lake la wazi" na "sifa za ajabu alizopata kutoka Shirika hilo.” Kwa ushirika wake, Kardinali alijiunga "katika Familia ya Agostino kwa kifungo cha pekee cha ushirika wa imani," akawa "mshiriki, katika maisha na baada ya kifo, katika faida za kiroho zinazotokana na Misa Takatifu, sala, sadaka, na kazi nzuri zinazofanywa na kaka na dada wa Shirika hilo mahali, popote walipo duniani." Kitendo hicho ni "utambuzi wa wale ambao wametoa huduma ya kustahiki hasa kwa Shirika la Mtakatifu Agostino na ambao wamefungwa kwa urafiki maalum." "Kwa kuguswa sana" na "hisia," Kardinali Parolin alishukuru Shirika la Agostinian na kuahidi kuombea familia ya Kitawa hiyo, kwa Papa, na kwa watu wote watawa, ili waendelee "kuishi uwazi huo kwa Kanisa ambao umekuwa na sifa kila wakati." Kardinali Parolin pia aliwaalika kutumikia Kanisa na wabatizwa wote.
Kardinali Parolin anapokea hati ya ushirika.
Kuwepo kwa Kanisa, ni tabia ya Waagostinian
"Tunaunda Familia moja ambayo Baba yake ni Mtakatifu Augustino," alisema Padre Moral, ambaye alitia saini Hati ya ushirika wa Kardinali Parolin, iliyosomwa na Katibu mkuu wa Shirika hilo, Padre Pasquale Di Lernia. "Umoja wa Familia hii lazima uimarishwe na ushirikiano wa washiriki wake wote, ili umoja wa nafsi na moyo kuelekea Mungu uliowekwa na Agostino katika Kanuni uweze kulindwa na kuongezeka kwa uaminifu miongoni mwa watoto wake." Mtawa huyo aidha alibainisha kwamba, "Shirika la Mtakatifu Agostino, lililoanzishwa miaka 781 iliyopita kwa mpango maalum wa Kiti cha Kitume, daima limedumishwa kama lengo lake, lengo na dharura msingi: upatikanaji wa mahitaji ya Kanisa na uaminifu kwa Papa Mkuu." Kipengele hiki kinakamilisha vipengele vingine vitatu vinavyounda hali ya kiroho ya Shirika: mambo ya ndani, maisha ya jamii, na ushirikishwaji wa kijamii na daima amewaunga mkono na kuwaongoza watawa "katika utume wa aina mbalimbali na wenye matunda mengi katika mabara matano, katika mstari wa mbele na daima katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu."
Kardinali Parolin na wakonselebranti.