Kard.Parolin,Burundi:huduma kwa wema wa pamoja ili wote waishi kwa hadhi
Vatican News
Maadhimisho ya Sherehe ya Kupalizwa kwa Bikira Maria tarehe 15 Agosti, sanjari na kuinuliwa hadhi ya Basilika Ndogo ya Parokia ya Mtakatifu Anthoni wa Padua, ambayo ndani ya eneo lake kuna Madhabahu ya Kitaifa ya Maria, ya Jimbo kuu la Gitega nchini Burundi ni katika, Maadhimisho yaliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican na yaliohudhuriwa na Maaskofu wa nchi hiyo, Balozi wa Vatican nchini Burundi na msaidizi wake wa kidiplomasia, mamia ya mapadre, watawa wa kike na kiume na maelfu ya waamini kutoka majimbo yote ya nchi ili kushuhudia tukio hili adhimu la adhimisho la Misa Takatifu. Serikali ya Burundi iliwakilishwa na Rais Évariste Ndayishimiye.
Misa katika Madhabahu ya Kitaifa ya Maria huko Mugera
Madhabahu ya Maria ya Mugera, ambako watu wanasali kwa Mama Yetu wa Lourdes, inayoadhimisha siku ya kuwekwa wakfu kwa Burundi kwa Bikira Maria, Malkia wa Amani, iliyokabidhiwa tarehe 15 Agosti 1961, ambapo Mwenyezi Mungu alitoa neema nyingi kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria, imeendelea kuwa ni mahali ambapo maelfu ya waamini wanafanya hija yao kwa ajili ya nchi na zawadi kwa ajili ya dunia kila mwaka. Hija inayoendelea kila mwaka imeendelezwa wakfu kwa Bikira ambacho ni kielelezo cha kukua kwa imani ya Kanisa la Burundi, la kutaka kutafuta hifadhi chini ya ulinzi wa Mama wa Mbinguni na kuongozwa kwa njia yake na Mwanawe, Yesu Kristo. Kinachoshangaza zaidi kuhusu mahali patakatifu pa Mugera ni jinsi kijiwe kidogo chenye mawe ya Kiafrika, kilichokusudiwa kufanana na lile la Lourdes, kinaweza kuvutia umati mkubwa wa mahujaji wanaokuja Mugera kupata tumaini na kusali kwa Mama yao wa Mbinguni na kuleta amani duniani na kuangaza akili za serikali kuchagua njia za amani kwa ulimwengu.
Kwa mhubu wa Kardinali parolini alisisitiza kuwa Waamini wote wa nchi hii pendwa, ambayo imejua majaribu mengi bado haijakata tamaa, wadhihirishe imani yao hapo ili watu wenye mapenzi mema waendeleze juhudi zao kwa ujasiri na bila ubinafsi kufikia amani inayotarajiwa sana. Kwa sababu hiyo, Kardinali Parolin, katika homilia yake, aliwasihi kwa nguvu tena kuvuka masilahi ya kibinafsi na, kwa bidii iliyofanywa upya, kutumikia wema wa wote ulimwenguni pote. Hii ni ili katika maeneo ya vita, ambako watu wengi wamevumilia majaribu na magumu kwa muda mrefu, watu waweze kutamani tena kuishi kwa heshima na usalama.
Baraka ya Mnara katika Kumbukumbu ya Nuncio Courtney
Hata hivyo tarehe 14 Agosti 2025 Katibu Mkuu wa Vatican alisafiri kwenda Minago kubariki mnara kwenye eneno ambapo, mnamo tarehe 29 Desemba 2003, Balozi wa Vatican Askofu Mkuu Michael Courtney, Askofu Mkuu wa Ireland, aliuawa kwa kuviziwa wakati akirejea nyumbani. Kardinali Parolin alikumbuka kwamba, Askofu Mkuu Courtney alitembea na watu wa Burundi katika miaka ngumu na daima alifanya kazi kwa upatanisho na amani, akishirikiana na kila mtu kwa uvumilivu na ustahimilivu ili kuwasilisha maono ya uwezekano wa amani, na kujifanya kuwa karibu na kila mtu, bila kujali maisha yake mwenyewe.
Kardinali Parolin hatimaye, alirudia maneno ambayo Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alimkumbuka Askofu Mkuu Courtney aliyosema mnamo tarehe 1 Januari 2004: kwa Wakristo, "kutangaza amani maana yake ni kumtangaza Kristo ambaye ni 'amani yetu,' ina maana ya kutangaza Injili yake, ambayo ni 'Injili ya amani'; inamaanisha kuwaita kila mtu kwenye baraka ya kuwa 'wapatanishi.' Monsinyo Michael Aidan Courtney, mwakilishi wangu kama Balozi wa Kitume nchini Burundi, pia alikuwa shahidi wa 'Injili ya amani.' Aliuawa kwa kusikitisha siku chache zilizopita alipokuwa akitekeleza azma yake ya kukuza mazungumzo na upatanisho. Tumwombee, tukitumaini kwamba kielelezo chake na dhabihu yake itazaa matunda ya amani katika Burundi na ulimwenguni pote.
Historia ya Basilika Ndogo ya Mugera
Kitendo cha kutoa jina la Basilika kwa Kanisa la Parokia ya Mugera, kama ilivyokuwa imesikika wakati wa tukio hilo, kiliidhinishwa mnamo tarehe 12 Septemba 2024, na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti, Kardinali Arthur Roche. Katika hafla hii, Rais wa Jamhuri alieleza matumaini yake kwamba Basilika hii itakuwa mahali pa kukutana na neema za Mwenyezi Mungu. Aliwataka Warundi kujiandaa kuchangia shughuli yoyote inayohusiana na urekebishaji wa usanifu wa kanisa hilo. Tangazo la kuinuliwa kwa Kanisa la Mugera hadi hadi hadhi ya la basilika limefungua ukurasa mpya katika historia ya Burundi, hasa ya kiutamaduni na kiroho, kama ilivyokuwa kwenye eneo hilo, katika eneo la zamani la kifalme, ambapo Vatican ilijenga parokia ya kwanza ya Burundi mnamo mwaka 1899, ambapo kabla ya hapo, Mugera ilikuwa katikati ya utambulisho wake wa kisiasa na kiroho.
Kanisa la Mugera, ambalo sasa limetangazwa kuwa Basilika Ndogo na Vatican, linajulikana kwa Madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Amani wa Mugera, iliyoko ndani ya wilaya yake ya parokia. Likiwa limeambatanishwa na Jimbo Kuu la Gitega na lililo katika jimbo la kisiasa la Gitega, liko katika sehemu muhimu katika historia ya Kanisa Katoliki nchini Burundi. Mahali hapo palikuwa sio tu mji mkuu wa kisiasa na kiroho na kituo cha kufanya maamuzi cha Burundi kabla ya ukoloni, lakini pia Kanisa kuu la kwanza la Kanisa kuu nchini Burundi na misheni ya pili ya Kikatoliki katika historia ya Burundi, iliyoanzishwa kama Kanisa na wamisionari wawili, Padre Van der Burgt na Van der Wee, mnamo Februari 11, 1899, baada ya kanisa la Muyaga huko Cankuzo (18989).
Mugera kwa hiyo daima pamekuwa mahali patakatifu. Ilikuwa hapo ambapo Warundi katika enzi ya kabla ya ukoloni walikusanyika ili kuomba "Imana" (Mungu), hivyo basi ikatokea usemi wa "Imana za Mugera." Hali ya kiroho ilikazia mfumo tata wa imani na desturi zinazohusishwa sana na ibada ya Imana, yaani mungu mkuu zaidi, na pia roho za asili na mababu. Miaka iliyofuata (1920-1944) ilitiwa alama na uwongofu mkubwa wa Warundi katika kipindi cha historia ya Kanisa Katoliki nchini Burundi.
Ingawa jengo la Kanisa la Mugera sasa ni Basilika, lilianza kama ujenzi wa nyasi mnamo 1908, wakati wa utawala wa Mfalme Mwezi Gisabo, mwana wa Mfalme Ntare Rugamba, wote mzaliwa wa Mugera. Hatua kwa hatua, mwaka wa 1922, paa ilibadilishwa na kuwa la vigae, na minara miwili ikajengwa. Madhabahu ya Maria ya Mugera hukaribisha maelfu ya mahujaji kutoka k nchini kila mwaka kuabudu hapo kwa karibu kila ifikapo tarehe 15 Agosti katika Maadhimisho ya Kupalizwa kwa Bikira Maria. Hapo pia ndipo Burundi ilipowekwa chini ya ulinzi wa Maria, juu ya kupalizwa kwa Bikira Maria kunako mwaka 1961, wakati wa sherehe iliyohudhuriwa na Mwanamfalme Louis Rwagasore. Kuinuliwa kwa Mugera hadi Hadhi ya Basilika ndogo kwa hiyo kunaweza kuleta manufaa chanya ya kiuchumi, kutokana na kufurika kwa mahujaji wapya kutoka eneo hilo na duniani kote.