Jubilei ya Vijana:Monstrance wa Piergiorgio Frassati na Don Bosco utatumika kwa mkesha wa vijana
Vatican News
Monstrance itakayotumika leo usiku wakati wa Ibada ya kuabudi Ekaristi kwenye mkesha wa Jubilei ya Vijana na Papa Leo XIV ina historia ndefu. Hii Inatoka Turino, kutoka katika Kikanisa cha kuabudu daima cha Parokia ya Mtakatifu Abate, nje kidogo ya kaskazini mwa jiji hilo. Hapo awali, ilitumika katika Kanisa la Mapadre wa Sakramenti Takatifu, ambao kwa zaidi ya karne wameongoza Ibada ya Kudumu ya kuabudu, kituo cha kweli cha kiroho cha jiji la Torino nchini Italia.
Kabla ya tukio hilo, kijana, Mwenyeheri Piergiorgio Frassati, ambaye atatangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 7 Septemba 2025, alisali kwa Yesu katika Ekaristi, pamoja na Carlo Acutis, mtume mwingine wa Ibada ya Ekaristi takatifu. Kabla ya monstrance inayotumiwa na Baba Mtakatifu Leo XIV, walisali pia kwa Mtakatifu Yohane Bosco, mtume wa vijana na mwanzilishi wa Shirika la Kisalesian, na sasa lililoenea duniani kote likijuliakana kama shirika la vijana.
Mtakatifu Joseph Benedikto Cottolengo, mtume wa upendo, aliye karibu na mdogo kabisa, ambaye alitoa uhai kwa wingi wa kazi za upendp kwa jina la Mungu-Upendo; Mtakatifu Yosefu Cafasso, aliyeelezwa na Papa Pio XI kama: "Lulu ya mapadre wa Italia," ambaye alitumia maisha yake yote kuungamisha na kutoa mafunzo kwa waungamaji wazuri. Miongoni mwa waliotubu walikuwa ni Don Bosco mwenyewe, Padre Cottolengo, na Padre Joseph Allamano, ambaye pia alitangazwa kuwa Mtakatifu mnamo tarehe 20 Oktoba 2024 na Papa Francisko.
Kisha, walioomba mbele ya Yesu, katika Monstance hiyo hio , walikuwa Mtakatifu Leonard Murialdo, mwalimu wa vijana wafanyakazi, Mwenyeheri Anna Michelotti, akiwahudumia wagonjwa; Ndugu Luigi na Giovanni Boccardo, Mapadre wa mfano; na Mwenyeheri James Alberion, mwanzilishi wa shirila la familia kuu ya Mtakatifu Paulo, nabii wa mawasiliano. Kwa hiyo, ni kundi la watakatifu wanaotuambia umuhimu wa ukuu wa Mungu na kurudi kwenye Ibada Yake,kimsingi wakimtambua kuwa Yesu yu hai na yumo katika Sakramenti Takatifu na kwa hiyo ni kumpenda ndani ya kaka na dada zetu.