Jimbo Kuu la Roma,Kard.Reina:sala na kufunga kwa ajili ya amani,Agosti 22
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Baldo Reina aliandika barua kwa Jimbo Kuu la Roma kwamba Baba Mtakatifu alitoa mwaliko wa kuishi Ijumaa tarehe 22 Agosti 2024 katika kumbu kumbu ya Maria Malkia wa Amani, kama siku ya kufunga na sala kwa ajili ya kuomba Bwana zawadi ya amani. “Jimbo letu, linakaribisha wito na kuwaelekea waamini wote. Katika kipindi kilichogubikwa na migogoro na ghasia, tunamkabidhi kwa imani Bikira Maria, machozi ya wanaoteseka, uchungu wa wasio na hatia, na matumaini kwa wale wote wanasubiri haki na upatanisho.” Kwa njia hiyo, “mwaliko ni kwa kila jumuiya, parokia, familia na waamini binafsi kushiriki katika siku hii: kufunga, kuishi kwa upatanisho na imani na umwilisho wa sala ugeuke kuwa ishara ya muungano wetu na kujitolea kwa ajili ya amani, Bwana, Mfalme wa amani atusaidie kuwa wajenzi wa maelewano na wa matumaini kati ya watu. Na Maria Malkia wa Amani, ambaye Kanisa linamkumbuka hasa katika siku hii, atuombee na kutusindikiza katika safari ya ubinadamu kuelekea upatanishao na umoja,” anahitimisha barua Kardinali Reina.
Kanisa la Italia linaunga mkono wito wa Papa
Kanisa Katoliki nchini Italia, nalo linaunga mkono mwaliko wa Baba Mtakatifu Leo XIV ambaye mara baada ya Katekesi yake tarehe 20 Agosti 2025, aliwaalika “waamini wote kuishi siku ya tarehe 22 Agosti 2025 kwa kufunga na sala, ili kumuomba Bwana atujalie amani na haki na kukausha machozi ya wale ambao wanateseka kwa sababu ya migogoro inayoendelea.” Kwa njia hiyo katika mwaliko huo, wa Maaskofu wa Italia uliotiwa zaidi na Kardinali Matteo Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia na Askofu Mkuu wa Bologna anakumbusha maneno ya Papa kwamba: “ kuomba zawadi ya amani na upatinisho dunia inayoendelea kujeruhiwa na Vita nchi Takatifu, Ukraine, na sehemu mbali mbali za dunia.” Kwa hiyo “ Tuunge wito huo wa Baba Mtakatifu kuhusu: Kuendelea kwa hali za vurugu, chuki, na kifo ambacho hutulazimisha kuzidisha maombi yetu kwa ajili ya amani ya kupokonya silaha na kupokonywa silaha, tukimsihi Bikira Maria mwenyeheri, Malkia wa Amani, kuondoa hofu ya vita kutoka kwa kila watu na kuangazia akili za wale walio na majukumu ya kisiasa na kidiplomasia, "alisema, akikumbuka kwamba "amani ya kila siku sio amani ya kiroho, sio njia ya amani ya kila siku, ishara, ambayo huunganisha uvumilivu na ujasiri, kusikiliza na kuchukua hatua. Na ambayo leo hii zaidi ya hapo awali, inahitaji uwepo wetu mtazamo na kuizalisha.