Baraza la Kipapa la Mawasiliano
Na Alessandro Di Bussolo – Vatican.
Baraza la Kipapa la Mawasiliano linaitwa "kujenga madaraja, wakati watu wengi wanainua kuta - kuta za itikadi; kukuza ushirika, wakati wengi wanachochea migawanyiko; kushiriki katika changamoto za wakati wetu, wakati wengi wanapendelea kutojali,"alisema hayo Papa Francisko, katika Mkutano wake wa mwisho na Baraza hili la Kipapa la Mawasiliano tarehe 31 Oktoba 2024. Naye Papa Leo wa XIV , katika Mkutano wake wa kwanza ()na timu ya mawasiliano ya Vatican baada ya kuchaguliwa kwake, aliwaalika “kuendeleza mawasiliano ambayo hayatafuti maafikiano kwa vyovyote vile, yasiyojifunika kwa maneno ya uchokozi, hayakumbatii kielelezo cha ushindani, na kamwe hayatenganishi utafutaji wa ukweli na upendo ambao tunapaswa kuutafuta kwa unyenyekevu.” Baadaye, wakati wa ziara yake katika kituo cha Masafa mafupi ya utangazaji cha Radio Vatican huko Santa Maria di Galeria, Papa Leo XIV alikumbuka kazi yake ya kimisionari katika bara la Amerika ya Kusini na Afrika, akielezea matangazo ya masafa mafupi ya Radio Vatican, ambayo hufikia mahali ambapo vituo vingine vinapata shida kufikia - kama "ya thamani kubwa", na kuthibitisha tena thamani ya kimisionari ya mawasiliano.
Vidokezo vya Kihistoria
Baraza la sasa, lilianzishwa awali kama Sekretarieti ya Mawasiliano na Papa Francisko kupitia barua ya kitume ya Motu Proprio () yaani(“Muktadha wa sasa wamawasiliano”) wa tarehe 27 Juni 2015, Baraza hili lilipewa dhamana ya kupanga upya mfumo mzima wa mawasiliano ya Kiti Kitakatifu. Hatua kwa hatua ilijumuisha vyombo vyote vya mawasiliano vilivyojitenga hapo awali kama vile: Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Makao matakatifu, Vyombo vya Habari vya Vatican, Huduma ya Picha, Osservatore Romano, Nyumba ya Uchapishaji wa Vitabu, Vatican, Radio Vatican, Kituo cha Televisheni cha Vatican, na Huduma ya Mtandao ya Vatican. Changamoto ilikuwa kuunganisha vyombo tisa kwa pamoja—vilivyoainishwa na mila na desturi za karne nyingi—katika mfumo mmoja wa uhariri na utawala, chini ya Baraza moja ndani ya Curia Romana.
Vyombo vya habari vya Vatican, Kongwe zaidi vilianzishwa na Papa Sixtus V kunako tarehe 27 Aprili 1587, kwa njia ya Barua ya kitume Eam semper, chini ya jina "Stamperia vaticana" ("Vatican printing house"). Fazeti la Osservatore Romano, la kila siku la Kiitaliano la Makao Makuu matakatifu, lilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 1 Julai 1861. Leo, hii linachapisha matoleo mbalimbali ya kila mwezi katika lugha nyingi kuu za kisasa. Nyumba ya Uchapishaji wa Vitabu Vatican (LEV) ambacho ni chombo rasmi cha uchapishaji cha Makao Makuu ya Matakatifu ya Vatican, ilianzishwa mnamo mwaka 1926. Tarehe 31 Mei 2005, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican wa wakati huo, Kardinali Angelo Sodano aliipatia hakimiliki ya kipekee kwa maandiko ya Papa.
Radio Vatican ilizinduliwa na Papa Pio XI kunako tarehe 12 Februari 1931 kama kituo cha utangazaji cha Mji wa Vatican. Marekebisho hayo yalileta mageuzi ya vyombo vya habari kwa utayarishaji wa uandishi wa habari, na kuhitimisha kwa taarifa za wakati halisi kwenye wavuti kupitia tovuti ya Vatican News, iliyotumika tangu Desemba 2017, na uwepo katika majukwaa makubwa ya mitandao ya kijamii. Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Makao Matakatifu, ilianzishwa kunako mwaka 1939, ikisambaza habari rasmi kuhusu Papa na shughuli mbalimbali za Kiti kitakatifu cha Kitume. Hapo awali ilikuwa sehemu ya Gazeti la Osservatore Romano, na ilipata uhuru wakati wa Mtaguso wa Pili wa Vatican (1962-1965), ikijiimarisha kama "Ofisi maalum ya waandishi wa habari."
Moja ya studio za Radio Vatican
Tarehe 30 Januari 1948, Pio XII alianzisha Tume ya Kipapa ya Utafiti na Tathmini ya Kikanisa ya Filamu kuhusu Mambo ya Kidini au Maadili. Mnamo 1959, pamoja na Motu Proprio(), yaani Mchungaji Mwema, Papa Yohane XXIII aliibadilisha kuwa ofisi ya kudumu ya Kiti Kitakatifu, iliyounganishwa na Sekretarieti ya Vatican. Kisha, tarehe 2 Aprili 1964, kwa Barua ya kitume ya Motu Proprio ya , Papa Paulo VI aliiunda upya tena kama Tume ya Kipapa ya Mawasiliano ya Kijamii, akiikabidhi jukumu la kufuatilia na kutathmini nyanja za sinema, radio, televisheni, na magazeti ya mara kwa mara na ya kila siku, kwa kuzingatia Majisterio ya Papa.
Tume ya Kipapa ya Mawasiliano ya Kijamii—iliyopewa hadhi baadaye kuwa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijami, ilipewa jukumu la kuandaa barua ya ya kichungaji Communio et progressio kuhusu Ushirika na maendeleo ya jamii ya wanadamu ambayo hujumuisha madhumuni ya msingi ya mawasiliano ya kijamii na vyombo vyake, kama vile vyombo vya habari, sinema, radio na televisheni(yaliyochapishwa mwaka 1971 na kusasishwa na nyongeza ya Aetatis novae- kadiri enzi mpya inavyokaribia, mawasiliano yanapata upanuzi mkubwa ambao unaleta sana tamaduni za ulimwengu kwa ujumla mwaka 1992) pamoja na kutangaza Siku ya Mawasiliano Duniani, iliyoanzishwa mwaka 1967.
Kituo cha Televisheni cha Vatican (CTV) kilianzishwa mwaka 1983 na Papa Yohane Paulo II ili kuandika huduma ya kichungaji ya Papa na shughuli za Kiti kitakatifu cha Kitume, kupitia picha za televisheni. Kila rekodi, programu, au makala iliyotayarishwa tangu 1984 huhifadhiwa kwenye kumbukumbu iliyo na vyumba vinavyodhibitiwa hali halisi yake.. Kwa kuundwa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, uzalishaji wa vipindi vya Talevisheni ya Vatican (CTV) sasa unaitwa Vatican Media. Hali hiyo hiyo inatumika katika Huduma ya Picha za Osservatore Romano, iliyoanzishwa mwaka 2006 na inayoundwa na wapiga picha, watunza kumbukumbu, na mafundi wanaoandika shughuli za Papa na mamlaka ya Makao Makuu Matakatifu kupitia upigaji picha. Kumbukumbu ya kidijitali ya huduma inapatikana kwa wachapishaji na magazeti na pia kwa watu binafsi.
Hatimaye, tarehe 25 Desemba 1995, Huduma ya Mtandao ya Vatican ilizinduliwa kwa kujumuisha na kuchapishwa mtandaoni kwa ujumbe wa Noeli wa Mtakatifu Papa Yohane Paul II kwenye tovuti mpya iliyoundwa wakati huo . Leo hii, wafanyakazi wa kiufundi na wa hali halisi ni sehemu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano.
Umahiri
Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium, inawajibika kwa mfumo mzima wa mawasiliano ya Kiti kitakatifu na kuunganisha na vyombo vyote vya Kiti Kitakatifu katika Tasnia ya Mawasiliano, ili mfumo mzima ujibu kwa uthabiti mahitaji ya utume wa Uinjilishaji wa Kanisa, katika muktadha unaodhihirishwa na uwepo na maendeleo ya vyombo vya habari vya kidijitali, na muingiliano. Ili kufanya hivyo, hutumia miundo ya uzalishaji, ubunifu wa kiteknolojia, na aina za mawasiliano zinazopatikana kwa sasa na zile zinazoweza kuendeleza siku zijazo.
Pamoja na kazi zake za uendeshaji, pia inachunguza na kuendeleza vipengele vya kitaalimungu na kichungaji vya shughuli za mawasiliano za Kanisa. Kwa maana hiyo inafanya kazi, ikiwa ni pamoja na katika ngazi ya elimu, ili kuhakikisha kwamba mawasiliano hayapunguzwi kwa dhana za kiteknolojia na za ala. Inaongeza mwamko kwa waamini kuhusu wajibu wao wa kuhakikisha kwamba, njia nyingi za mawasiliano zinapatikana kwa ajili ya utume wa kichungaji wa Kanisa, katika huduma ya maendeleo ya ustaarabu na maadili. Inafanya hivyo hasa katika maadhimisho ya Siku ya Hupashanaji Habari Duniani. Kwa ajili ya shughuli zake, Baraza la Kipapa la Mawasiliano linatumia uunganisho na miundombinu ya mtandao wa Mji wa Vatican, kwa mujibu wa sheria maalum na ahadi za kimataifa zinazofanywa na Kiti Kitakatifu. Inafanya kazi kwa ushirikiano na Sekretarieti ya Vatican na kuunga mkono taasisi nyingine za Curia Romana na ofisi na taasisi zinazohusiana na Makao Makuu na Gavana wa Mji wa Vatican katika shughuli zao za mawasiliano.
Ili kujua mengi unaweza kutembelea tovuti ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambapo unaweza kubonyeza hapa: