Askofu Mkuu Gallagher nchini Slovenia kwa ajili ya Kongamano la Kimkakati la Bled
Vatican News
Kuanzia Agosti 31, hadi Jumanne Septemba 2, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, atakuwa nchini Slovenia kushiriki katika toleo la 20 la Jukwaa la Mkakati wa Bled, linalofanyika katika mji huo huo. Hii ilitangazwa kwenye ukurasa wa X wa Sekretarieti ya Vatican(@TerzaLoggia).
Jukwaa la Mkakati wa Bled lililoanzishwa mwaka wa 2006 ni jukwaa la mikutano kujadili masuala ya kisiasa, usalama, na maendeleo na changamoto zinazoathiri Ulaya na dunia kwa ujumla, likiwaleta pamoja washiriki kutoka tamaduni na asili mbalimbali. Mada ya toleo la mwaka huu 2025 ni "Ulimwengu Unaokimbia" na itaakisi jinsi Ulaya na Umoja wa Ulaya zinavyoweza kushiriki na kufafanua upya jukumu lao katika kushughulikia migogoro na mivutano mbalimbali ya kijiografia, kisiasa, kiuchumi na hali ya tabianchi inayokabili dunia leo.