Roma,Jiji la Matumaini:Maeneo ya Jubilei ya Vijana 2025!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Ni muhimu kuona maneo makuu matatu ya makutaniko ya vijana Kutoka Ulimengu mzima katika hija yao ya matumaini kuanzia tarehe 28 Julai hadi tarehe 3 Agosti 2025.
Awali ya yote wamekutaniko yao yameanzia katika Uwanja wa Mtakatifu Petro tarehe 29 Julai 2025 na kuendelea....
Uwanja mwingine mkubwa ni ule wa Cicrus Maximo, jijini Roma wenye historia ya kipindi cha Kati, mahali ulipangwa kwa ajili sehemu ya kufanyia toba.
Na hatimaye katika Uwanja mkubwa sana ulioko huko Tor Vergata, unaowakilishwa na onesha la Tanga kubwala la Vela Calatrava mahali ambapo vijana watafanya mkesha kuanzia tarehe 2 hadi 3 Agosti 2025 wakisubiri kuhitimishwa kwa misa takatifu. Hata hivyo kutwa nzima ya tarehe 2 kutakuwa na Tamasha la vyombo vya muziki. Uwanja huo uliandaliwa kunako Jubilei ya Mwaka Mtakati 2000 na sasa baada ya miaka 25 utaona umati ule ule kutoka ulimwenguni kote.