杏MAP导航

Tafuta

Vatican na Japan zinapania kuimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia kwa kujikita katika kutafuta, kulinda na kudumisha haki na amani duniani. Vatican na Japan zinapania kuimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia kwa kujikita katika kutafuta, kulinda na kudumisha haki na amani duniani.  (AFP or licensors)

Kardinali Parolin: Maonesho ya Dunia Nchini Japan: Uzuri na Matumaini

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anaeleza jinsi uzuri na matumaini vinavyoweza kuwa dawa dhidi ya hali ya kukata tamaa na hofu, katika ya Siku ya Kitaifa ya Vatican kwenye Maonesho ya Dunia 2025 huko Osaka, Japani, Kardinali Pietro Parolin, alitoa salamu maalum kwa watu wote wa Japani kwa niaba ya Papa Leo XIV. Miaka 80 ya ujenzi wa pamoja wa jamii: Ingawa nchi hizi mbili zina mizizi tofauti ya kitamaduni na kidini kwa muda mrefu zinafahamiana.

Na Sarah Pelaji, -Vatican

Katika Siku ya Kitaifa ya Vatican katika Maonesho ya Dunia nchini Japani, Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anaeleza jinsi uzuri na matumaini vinavyoweza kuwa dawa dhidi ya hali ya kukata tamaa na hofu, katika ya Siku ya Kitaifa ya Vatican kwenye Maonesho ya Dunia 2025 huko Osaka, Japani, Kardinali Pietro Parolin, alitoa salamu maalum kwa watu wote wa Japani kwa niaba ya Papa Leo XIV. Miaka 80 ya ujenzi wa pamoja wa jamii: Ingawa nchi hizi mbili zina mizizi tofauti ya kitamaduni na kidini, Kardinali Parolin alieleza kuwa kwa muda mrefu zimeamua kufahamiana zaidi na kuthamini sifa za kila moja. Miaka 80 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili inaungwa mkono na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao kwa jamii ya Kijapani.

Expo Osaka, Japan 2025
Expo Osaka, Japan 2025   (ANSA)

Katibu Mkuu wa Vatican alisisitiza pia hamu ya pamoja ya Vatican na Japan ya ujenzi wa amani, uthabiti na juhudi za pamoja za kudhibiti usambazaji holela wa silaha. Alikumbusha kumbukumbu ya miaka 80 tangu kutokea kwa mlipuko wa mabomu Hiroshima na Nagasaki kama tukio la kihistoria lililochangia kujenga juhudi za pamoja kwa ajili ya kujenga amani. “Mwaka huu, maadhimisho kadhaa muhimu yanatufanya tukumbuke historia ndefu ya mahusiano kati ya Kiti Kitakatifu na Japani. Kwa mfano, miezi hii tunakumbuka miaka 470 tangu Mjapani wa kwanza Mkatoliki, Bernard wa Kagoshima, alipokutana na Papa Paulo IV mwaka 1555. Mnamo mwezi Machi, tuliadhimisha pia miaka 440 tangu ujumbe wa kwanza wa Kijapani kufika Ulaya ujulikanao kama Ubalozi wa Tensho ambao ulifika Roma kisha kuonana na Papa Gregori III. Mwaka huu pia tunaadhimisha miaka 410 tangu Ubalozi wa Keicho ulipokutana na kuzungumza na Papa Paulo V mwaka 1615. Mikutano hii ya kihistoria ilikuwa mwanzo wa uhusiano wa kidiplomasia ambao umedumu kwa muda mrefu na ambao tunatarajia utaimarika zaidi siku zijazo,” amesema Kardinali Parolin.

EXPO Osaka 2025: Uzuri na Matumaini ni chanda na pete
EXPO Osaka 2025: Uzuri na Matumaini ni chanda na pete   (AFP or licensors)

Uzuri ni lugha ya ulimwengu wote: Akiangazia maadili ya pamoja, maudhui ya Banda la Vatican katika Maonyesho ya Dunia yanatilia mkazo mambo mawili muhimu ambayo ni uzuri na matumaini ambayo Kardinali alieleza kuwa na umuhimu mkubwa katika muktadha wa sasa wa dunia. Akizungumza kuhusu uzuri, alisema kwamba uzuri husaidia kuponya moyo na majeraha katika nyakati ngumu. Unakuwa dawa dhidi ya kukata tamaa, lugha ya ulimwengu wote inayowaunganisha watu na kukuza mshikamano kati ya Mataifa. Kardinali Parolin alieleza umuhimu wa kuthamini maonesho yote ya uzuri ikiwa ni pamoja na uzuri wa kijamii unaotokana na juhudi za mshikamano, miradi ya kujitolea na maamuzi ya upatanisho na msamaha. “Kwetu sisi, Kristo ndiye kielelezo kikuu cha uzuri wa Kimungu, uzuri unaopita mwonekano wa nje na kufikia mioyo na roho za watu. Kristo Yesu pia ni tumaini la mwanadamu, kwa kuwa kwa njia ya maisha, mateso na kifo chake alifungua njia ya wokovu na upyaisho kwa wanadamu wote. Uzuri na tumaini ni maadili ambayo tunataka kuyashirikisha kwa dunia nzima kwa imani kwamba, kutoka kwayo kunaweza kuchipua mustakabali bora kwa wote,” alieleza Kardinali Parolini. Matumaini kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi: Akiendelea na maudhui ya Banda la Vatican, Kardinali Parolin alisema kuwa matumaini yamefungamanishwa kwa karibu na wazo la uzuri. Kwa Wakristo matumaini yamejikita katika imani kwa Mwenyezi Mungu na upendo wake kwa wanadamu. Matumaini siyo thamani ya binafsi wala hayaleti ubinafsi au kujitenga tena hayahusiani na mafanikio ya mtu binafsi. Matumaini yanahitajika katika nyakati hizi za sasa kuliko wakati mwingine wowote, kwani tupo kwenye ulimwengu uliojaa vurugu na changamoto za Kimataifa hivyo kusababisha watu wengi kuishi kwa hofu na kukosa matumaini ya maisha yao huko mbeleni. “Ni kwa matumaini tu tunaweza kupata tiba dhidi ya hofu na kupata msukumo wa kutafuta suluhisho na kuchukua hatua za pamoja za kutafuta amani na kurejesha tumaini,” alisisitiza Kardinali.

Kard. Parolin
02 Julai 2025, 16:49