Askofu Msaidizi Simon Peter Kamomoe Jimbo Katoliki Wote, Kenya
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumamosi tarehe 5 Julai 2025 amemteuwa Askofu Msaidizi Simon Peter Kamomoe wa Jimbo kuu la Nairobi, Kenya kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Wote nchini Kenya. Itakumbukwa kwamba Askofu Msaidizi Simon Peter Kamomoe wa Jimbo Katoliki la Wote alizaliwa tarehe 26 Novemba 1962 huko Gatundu, Wilaya ya Kiambu, Jimbo kuu la Nairobi.
Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 18 Juni 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Nairobi. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 13 Februari 2024 akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Nairobi, Kenya. Na ilipo gota tarehe 5 Julai 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Wote, lililoko nchini Kenya.