杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo XIV amemteua PadrI Michel Guillaud, kutoka Jimbo Kuu Katoliki Lyon Ufaransa, kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Constantine nchini Algeria. Papa Leo XIV amemteua PadrI Michel Guillaud, kutoka Jimbo Kuu Katoliki Lyon Ufaransa, kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Constantine nchini Algeria.   (AFP or licensors)

Askofu Michel Guillaud Jimbo Katoliki la Constantine, Algeria!

Askofu Michel Guillaud alizaliwa tarehe 24 Juni 1961 mjini Villeurbanne, Ufaransa. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadri tarehe 1 Julai 1990. Katika maisha na huduma yake ya kichungaji, Padre Guillaud amewahi kushika nafasi mbalimbali, zikiwemo: Mwalimu wa Somo la Kiislam katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lyon, Amekuwa Padre mlezi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lyon. Amekuwa ni Katibu mkuu wa CERNA kuanzia Mwaka 2025 hadi 2025.

Na Sarah Pelaji, -Vatican

Papa Leo XIV amemteua Padre Michel Guillaud, kutoka Jimbo Kuu Katoliki Lyon Ufaransa, kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Constantine nchini Algeria. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Guillaud alikuwa Msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo. Wasifu wa Askofu Mteule: Monsinyo Michel Guillaud alizaliwa tarehe 24 Juni 1961 mjini Villeurbanne, Ufaransa. Baada ya masomo kutoka katika Chuo Kikuu cha Lyon, alipata Shahada ya Uzamili katika Taalimungu. Baadaye alisomea Shahada ya Uzamili katika Masomo ya Kiislamu (Islamolojia) katika Taasisi ya Kipapa ya Masomo ya Kiarabu na Kiislamu (PISAI), mjini Roma. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadri tarehe 1 Julai 1990 akawa Padri wa Jimbo Kuu Katoliki Lyon, nchini Ufaransa Katika maisha na huduma yake ya kichungaji, Padre Guillaud amewahi kushika nafasi mbalimbali, zikiwemo: Mwalimu wa Islamolojia katika Chuo Kikuu   cha Kikatoliki cha Lyon, Amekuwa Padre mlezi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lyon.

Askofu Michel  Guillaud wa Jimbo Katoliki la Constantine, Algeria
Askofu Michel Guillaud wa Jimbo Katoliki la Constantine, Algeria

Mnamo mwaka 2006-2014, alikuwa Paroko wa Parokia ya Batna, Paroko wa Constantine mwaka 2014-2016 na Skikda 2016 hadi alipoteuliwa na Papa Leo XIV kuwa Askofu. Amekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Constantine kati ya mwaka 2020-2024 na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki wa Afrika ya Kaskazini (CERNA) (2015-2025.) Kuanzia mwaka 2024, alihudumu kama Msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo. Uteuzi huu unakuja kama sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma ya kichungaji na uwepo wa Kanisa Katoliki katika eneo la Afrika Kaskazini. Askofu Michel Guillaud alizaliwa tarehe 24 Juni 1961 mjini Villeurbanne, Ufaransa. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadri tarehe 1 Julai 1990. Katika maisha na huduma yake ya kichungaji, Padre Guillaud amewahi kushika nafasi mbalimbali, zikiwemo: Mwalimu wa Somo la Kiislam katika Chuo Kikuu   cha Kikatoliki cha Lyon, Amekuwa Padre mlezi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lyon.

Askofu Michel
11 Julai 2025, 15:26