Tume ya Ulinzi wa Watoto wakutana na Papa:Songa mbele katika utume!
Vatican News.
Saa ya mazungumzo na Papa Leo XIV, wakati wa kutafakari, mazungumzo na upya wa "dhamira isiyo yumbayumba ya Kanisa katika kulinda watoto na watu walio katika mazingira magumu”. Haya ndiyo tunayoyasoma katika taarifa kwa vyombo vya habari ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto iliyoakisi Mkutano wa tarehe 5 Juni 2025 katika Jumba la Kitume pamoja na Papa. Taarifa hiyo inabinisha kuwa “Fursa ya kuendelea na safari iliyofanyika kwa unyenyekevu na matumaini, kadiri ya utume ambao Baba Mtakatifu Francisko aliukabidhi kwa Tume hiyo alipoianzisha mwaka 2014, kwa lengo la kuendeleza na kukuza viwango vya ulinzi wa watu wote na kulisindikiza Kanisa katika kujenga utamaduni wa uwajibikaji, haki na huruma.”
Mipango ya majaribio
Taarifa kwa vyombo vya habari inarejea kile ambacho kimefanywa katika miaka miwili iliyopita, kwa kufanya mchakato mpana wa kutengeneza seti ya miongozo ya ulimwengu kwa ajili ya kuwalinda watu, kwa mashauriano ya karibu na viongozi wa Kanisa, wataalamu wa kulinda, walionusurika na unyanyasaji na wafanyikazi wa kichungaji ulimwenguni kote. Juhudi za sinodi ambazo ziliongoza kwa rasimu ya mfumo, iliyojaribiwa na kuboreshwa kupitia programu za majaribio huko Tonga, Poland, Zimbabwe na Kosta Rika ambazo ziliipatia Tume maarifa muhimu katika nyanja za ulinzi wa kiutendaji, kiutamaduni na kitaalimungu. Miongozo ya kina ya kitaalimungu, yenye msingi katika Maandiko, katika mafundisho ya Kikatoliki ya kijamii na katika majisterio ya Papa Benedikto XVI, Papa Fransisko na Papa Leo XIV ili waweze kuzalisha uwongofu wa kweli wa moyo na ili ulinzi uwe sio tu hitaji, lakini tafakari ya wito wa Injili ya kulinda mdogo kati yetu,” taarifa hiyo imebainisha.
Kuanzisha mipango ya kumbu kumbu
Papa pia aliarifiwa kuhusu maendeleo ya Mpango wa Kumbukumbu, uliopewa jina la sala ya kale kwa Bikira Maria, mpango wa maendeleo ulioundwa kusaidia makanisa ya mahalia, hasa katika Nchi za Kusini mwa Ulimwengu, katika jitihada zao za kulinda watoto wadogo na kuwatunza waathirika wa nyanyaso. Unatoa jibu la kivitendo na la kichungaji kwa wito wa Papa Francisko kwa kila Kanisa mahalia kuwa mahali usalama kuliko yote. Kwa msaada wa kifedha kutoka katika Mabaraza ya Maaskofu, Mpango wa Kumbukumbu hufanya kazi kupitia nguzo nne:
1. Kuunda miundombinu ya ulinzi: ofisi mahalia zinazotoa usaidizi kwa waathiriwa, kuhakikisha mbinu za kuripoti, na kutoa ufikiaji wa huduma za kisheria, kisaikolojia na kichungaji.
2. Kuzuia kupitia elimu: kutoa mafunzo na usaidizi wa utekelezaji wa itifaki zinazokuza mazingira salama na utamaduni wa matibabu na heshima.
3. Ushirikiano wa kimataifa: kujenga mitandao baina ya mabara kwa ajili ya kubadilishana maarifa na ushirikiano wa pamoja, chini ya kanuni ya "Kanisa Moja la Ulinzi wa Watoto."
4. Mawasiliano ya kimkakati: ili makanisa mahalia yawasiliane vyema, yakikuza ulinzi na kukuza uwazi.
Ripoti ya Mwaka ya 2024: Haki ya Ubadilishaji
Tume pia ilisasisha kwa Papa juu ya maendeleo na athari za Ripoti ya Mwaka, iliyopendekezwa kwa mara ya kwanza na Papa Francisko mwaka 2022, ambayo inalenga kutathmini uwezo wa kulinda wa makanisa mahalia, kutoa mapendekezo ya vitendo kulingana na hali halisi ya kila eneo. Ripoti ya Mwaka mwaka huu inatoa uchunguzi makini wa haki ya uongofu kwa njia ya fidia. Hii ni pamoja na utafiti wa kina wa kichungaji-kitaalimungu na ukusanyaji wa takwimu juu ya mazoea ya sasa ya malipo katika Kanisa la ulimwengu wote. Kitabu kipya cha mwongozo juu ya fidia, kutokana na uzoefu wa maisha ya waathirika, na walio katika mazingira hatarishi kinatayarishwa ili kuongoza makanisa mahalia katika kujibu kwa haki na huruma.
Ripoti inahusisha uboreshaji wa mbinu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kikundi kilichopanuliwa cha kuzingatia waathirika na walio katika mazingira magumu, na michango ya moja kwa moja kutoka kwa waathirika katika kanda zote nne za Tume. Takwimu ya Kanisa katika ngazi ya nchi pia inatokana na mchakato wa mapitio ya Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto, ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya uwazi zaidi kupitia data za nje. Tume pia inaakisi ushirikiano unaoendelea na washirika wa Umoja wa Mataifa ili kuboresha upatikanaji wa takwimu za kuaminika juu ya kuenea kwa unyanyasaji, ikitoa wito kwa taasisi zaidi ya Kanisa kuwekeza katika mfumo bora wa ukusanyaji wa takwimu kwa hatua zaidi za msingi wa ushahidi.
Uchambuzi katika nchi 22 na mashirika mawili ya kitawa
Ripoti ya mwaka huu inatoa mapitio na uchunguzi kwa nchi 22 na mashirika mawili ya kitawa ikiwa ni pamoja na kutambua mwelekeo na changamoto za kikanda, na inajumuisha mapitio ya kitaasisi ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Sehemu ya mwisho imejitolea kwa mbinu ya awali ya Tume ya Mapitio ya Harakati za Walei, iliyojaribiwa kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, na matokeo ya kwanza ya mapitio ya Harakati ya Wafocolare.
Wito wa Kulinda kwa Huruma
Wakati wa kusikilizwa, Tume ilisisitiza dhamira yake ya umoja na ushirikiano wa wanachama wake. Barua iliyotiwa saini na wanachama wote baada ya Mkutano Mkuu wa Machi 2025 ilisisitiza haja ya kuendelea katika mamlaka, utawala na mbinu za kazi, kuthibitisha uhuru wa Tume na jukumu lake kama mshauri wa kuaminiwa wa Papa. Taarifa hiyo inatoa shukrani kwa Mabaraza ya Kipapa ya Curia Romana kwa ushirikiano wao unaokua katika huduma hii muhimu. Matumaini ni kuwasilisha Mfumo wa mwisho wa Miongozo ya Kiulimwengu kwa Papa Leo XIV ifikapo mwisho wa mwaka. Wakati huo huo, dhamira ya kusikiliza, kutembea na waathirika na waokokaji na kuunga mkono kila Jumuiya ya kikanisa katika jitihada zake za kuwalinda watu wote wa Mungu kwa huruma inathibitishwa tena.