Padre Francesco Ielpo(OFM) ni Msimamizi mpya wa Nchi Takatifu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua Padre Francesco Ielpo, O.F.M., kuwa Msimamizi wa Nchi Takatatifu na Mkuu wa Conventi ya Mlima Sion. Uteuzi wake unathibitisha kumaliza muda wake Padre Francesco Patton ambaye amekuwa msimamizi wa Nchi Takatifu tangu mwaka 2016, akiwa mkuu wa Shirila la Wafransiskani walioko Israel, Palestina, Syria, Jordan, Lebanon, Cyprus na Rhodes. Ni katika habari iliyowasilishwa asubuhi ya Jumanne tarehe 24 Juni 2025, kwa barua rasmi iliyotumwa na Mkuu wa Shirika la Wafransiskani, Fra Massimo Fusarelli (OFM).
Wasifu wake(CV)
Padre Francesco Ielpo, ni mzaliwa wa italia huko Lauria Jimbo la Potenza(PZ) tarehe 18 Mei 1970. Alijiunga kwa dhati katika Shirika la Wafransiskani la Ndugu Wadogo mnamo mwaka 1998; wakati mwaka 2000 alipewa daraja la Upadre. Katika utume wake ameshikilia nyadhifa mbalimbali kama vile: Mwalimu wa Dini (1994-2010); Mkuu wa Taasisi ya Franciscanum ya Luzzago huko Brescia (tangu 2000); Mjumbe wa Baraza la Kitaifa la FIDAE (Shirikisho la Taasisi za Shughuli za Kielimu) (2006-2010); Mkuu wa Kanda ya Lombardia (2007-2010); Paroko wa Mtakatifu Antonio wa Padova huko Varese (2010-2013).
Kuanzia Septemba 2013 hadi 2016 alikuwa Kamishna wa Nchi Takatifu ya Lombardia, akiendelea na jukumu hilo kutoka 2016 hadi 2023 kwa Kanda ya Kaskazini mwa Italia. Tangu 2014 amekuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama cha Pro Terra Sancta. Na wakati huo tangu 2022 Rais wa Mfuko wa Nchi Takatifu, Mjumbe wa Nchi Takatifu kwa Italia, Mjumbe Mkuu wa urekebishaji wa Kanda za Campania, Basilicata na Calabria.