杏MAP导航

Tafuta

Huu ni mkutano wa Mabalozi wa Vatican, unaofanyika kila baada ya miaka mitatu, kielelezo cha umoja huku wakimzunguka Khalifa wa Mtakatifu Petro ambaye kwa sasa yuko katika nafsi ya Baba Mtakatifu Leo XIV. Huu ni mkutano wa Mabalozi wa Vatican, unaofanyika kila baada ya miaka mitatu, kielelezo cha umoja huku wakimzunguka Khalifa wa Mtakatifu Petro ambaye kwa sasa yuko katika nafsi ya Baba Mtakatifu Leo XIV.  

Mabalozi wa Vatican: Wajumbe wa Amani Na Diplomasia ya Injili

Mabalozi hawa ni madaraja kati ya Baba Mtakatifu na Makanisa mahalia na Serikali na Taasisi mballimbali na kwamba, wao ni vyombo vya majadiliano kati ya Vatican na nchi husika. Ni viongozi wanaopaswa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha: utu, heshima, haki msingi za binadamu; uhuru wa kuabudu pamoja na uhuru wa kidini; ili kujenga na kudumisha mahusiano na mafungamano ya Jumuiya ya Kimataifa. Ni mashuhuda wa amani na diplomasia ya Injili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Vatican ina mahusiano na mafungamano ya kidiplomasia yanayovuka mipaka ya kijiografia kwa kuzingatia sheria za Kimataifa na itifaki za kidiplomasia. Tangu uwepo wa nchi ya Vatican, ilipewa haki ya kidiplomasia na kwamba, Vatican ni kati ya nchi ambazo zimekuwepo kwenye medani za Kimataifa kwa miaka mingi. Lengo ni kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha utu, heshima, ustawi na maendeleo ya binadamu: kiroho na kimwili. Vatican iko mstari wa mbele katika kudumisha Injili ya familia inaofumbata Injili ya uhai; tunu msingi zinazotishiwa na utamaduni wa kifo kwa nyakati hizi. Mabalozi za Vatican ni wawakilishi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro katika mchakato wa kukuza na kudumisha umoja na ushirika; upendo na mshikamano na Makanisa mahalia. Katika nchi husika, Ubalozi wa Vatican unalenga pamoja na mambo mengine kuwa: Ni kiungo muhimu kati ya Serikali na Kanisa mahalia sanjari na kudumisha majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni. Vatican daima iko makini kusikiliza na kujibu kilio na matumaini ya Makanisa mahalia, ili kwa pamoja waweze kusimama kidete kulinda na kutetea: haki msingi za binadamu, uhuru wa mawazo pamoja na uhuru wa kidini pamoja na kutekeleza dhamana utume wake kadiri ya sheria za nchi na za Kimataifa. Mabalozi na wawakilishi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro wanapaswa kutolea ushuhuda wa ujumbe wa Injili kwa maneno na matendo yao; kati ya wakuu wa Serikali na Jumuiya za Kikristo wanazozihudumia, ili kujenga na kuimarisha umoja na mshikamano wa dhati. Kama wawakilishi wa Vatican, wanapaswa kusaidia mchakato wa ujenzi wa Kanisa mahalia, kuendelea kuwa ni viungo makini kati ya Kanisa la Kiulimwengu na Maaskofu mahalia; kwa njia ya utume huu wanajenga na kuimarisha mshikamano na umoja wa Kanisa zima.

Mkutano wa Mabalozi na Wawakilishi wa Vatican
Mkutano wa Mabalozi na Wawakilishi wa Vatican   (@Vatican Media)

Ni utume unaohitaji: sadaka, majitoleo na utayari wa kuishi na kukutana na watu kutoka katika tamaduni, hali za maisha kijamii na kikanisa. Kimsingi Mabalozi na wawakilishi wa Vatican katika nchi mbali mbali duniani ni vyombo na mashuhuda wa diplomasia ya tunu msingi za Kiinjili; wanaojisadaka bila ya kujibakiza katika kukuza na kukoleza majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni, ili kupandikiza mbegu ya haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa.Hii ni sehemu ya majibu yaliyotolewa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, katika mahojiano maalum na vyombo vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Vatican mintarafu Mabalozi na Wawakilishi wa Vatican, ambao wako mjini Vatican kama sehemu ya majiundo yao sanjari na kushiriki katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo. Huu ni mkutano wa Mabalozi na Wawakilishi wa Vatican, unaofanyika kila baada ya miaka mitatu, kielelezo cha umoja na mshikamano wa Kanisa, huku wakimzunguka Khalifa wa Mtakatifu Petro ambaye kwa sasa yuko katika nafsi ya Baba Mtakatifu Leo XIV. Mabalozi hawa ni madaraja kati ya Baba Mtakatifu na Makanisa mahalia na Serikali na Taasisi mballimbali na kwamba, wao ni vyombo vya majadiliano kati ya Vatican na nchi husika. Ni viongozi wanaopaswa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha: utu, heshima, haki msingi za binadamu; uhuru wa kuabudu pamoja na uhuru wa kidini; ili kujenga na kudumisha mahusiano na mafungamano ya Jumuiya ya Kimataifa. Mabalozi na wawakilishi wa Vatican kimsingi, wao ni wawakilishi wa shughuli za kichungaji zinazotekelezwa na Mama Kanisa kwa ajili ya Kanisa la Kiulimwengu sanjari na Kanisa mahalia. Balozi wa Vatican kwanza kabisa ni Mtu wa Mungu na Kanisa, kumbe hana budi kuwa ni mfano bora wa kuigwa, kama Kristo Yesu, Mchungaji mwema. Kwa njia hii, wanahamasishwa na Mama Kanisa kuwa karibu zaidi na watu wa Mungu wanaowaongoza; wanaitwa na kutumwa kuhudumia. Wao ni madaraja kati ya Khalifa wa Mtakatifu Petro, Kanisa la Kiulimwengu, Makanisa mahalia, Serikali husika pamoja na Taasisi za Kimataifa, ili kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini tayari kuganga na kutibu madonda yanayomwandama mwanadamu, kwa njia ya tunu msingi za Kiinjili.

Mabalozi wa Vatican ni mashuhuda wa tunu msingi za Injili
Mabalozi wa Vatican ni mashuhuda wa tunu msingi za Injili   (@VATICAN MEDIA)

Kardinali Pietro Parolin anakaza kusema, sifa kuu za Balozi wa Vatican pamoja na mambo mengine ni: Unyenyekevu unaomwezesha kuwa ni chombo na shuhuda wa tunu msingi za Kiinjili dhidi ya: chuki, vita na uhasama. Ni mtu wa sala na anayejiaminisha kwa: huruma, tunza, ulinzi na neema za Mwenyezi Mungu ili kutekeleza vyema dhamana na wajibu wake. Balozi wa Vatican ni chombo na shuhuda wa Diplomasia ya Injili, tayari kuitangaza na kuishuhudia hadi miisho ya dunia. Kimsingi Balozi wa Vatican anapaswa kuwa ni mtu wa upatanisho, ili kumsaidia Baba Mtakatifu katika utekelezaji wa dhamana na majumu yake ya kutengeneza Ulimwengu huu uwe ni mahali pazuri pa kuishi kwa kujikita katika majadiliano yanayosimikwa katika ukweli na uwazi; ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni kiongozi anayepaswa kuwa ni chombo na shuhuda wa Injili ya haki, amani na maridhiano; kiongozi mwenye uwezo wa kujadiliana na jirani zake. Mabalozi wa Vatican ni Mapadre wanaotekeleza dhamana na wajibu wao katika ari na mwamko wa Kikasisi, huku wakitumia karama na mapaji waliyokirimiwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya mchakato wa uinjilishaji. Hawa ni viongozi wanaoteuliwa kwa ajili ya huduma kwa Makanisa mahalia na hivyo kuwa ni kiungo kati ya Baba Mtakatifu, Kanisa mahalia na viongozi wa Serikali, kumbe ni watumishi wanaopaswa kufahamu fika Sheria za Kimataifa, maisha ya watu wanaowahudumia na sehemu mbalimbali ambako kuna mahitaji msingi ya watu wa Mungu. Leo hii anasema Hayati Baba Mtakatifu Francisko kuna changamoto mamboleo zinazomwandama mwanadamu mintarafu kanuni maadili na utu wema mintarafu ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, mambo yanayohitaji majiundo makini na endelevu na kwa kuzingatia mchakato wa ujenzi wa Kanisa la Kisinodi na Kimisionari.

Askofu mkuu Novatus Rugambwa afya yake ikiendelea kuimarika.
Askofu mkuu Novatus Rugambwa afya yake ikiendelea kuimarika.

Ili kutekeleza dhamana na wajibu huu msingi kuna haja ya kujenga na kukuza tabia ya ujirani mwema, utamaduni wa kusikiliza kwa makini, ushuhuda wenye mvuto na mashiko; ni watu ambao wako tayari kujibidiisha katika ujenzi wa udugu wa kibinadamu unaosimikwa katika fadhila ya unyenyekevu na upendo, ili hatimaye, waweze kufanana na Kristo Yesu, Mchungaji mwema. Rej. Mt 11:28-30; Yn 10: 11-18. Mapadre wanaoteuliwa kwa uangalifu mkubwa kutoka katika Majimbo mbalimbali wanapaswa kuandaliwa kwa umakini mkubwa ili waweze kukabiliana kwa ufanisi na changamoto mamboleo, utandawazi usiojali wala kuguswa na maisha ya wengine na hasa kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia. Taasisi ya Kipapa ya Diplomasia ya Kanisa “Pontificia Accademia Ecclesiastica, PAE” kwa muda wa takribani miaka mia tatu, imekuwa ikitekeleza dhamana na wajibu huu kama Chuo cha Diplomasia ya Kanisa. Chuo hiki kimeboreshwa kwa kusoma alama za nyakati ili kuweza kukabiliana na changamoto mamboleo zinazoendelea kujitokeza katika medani mbalimbali za Kimataifa mintarafu ari na mwamko wa Kiinjili na Mamlaka Fundishi ya Kanisa, kama chombo cha umoja na ushirika; haki na amani pamoja na ujenzi wa mshikamano na mafungamano ya kijamii na watu wa Kimataifa.

Kardinali Parolin
10 Juni 2025, 16:19