Lillestr?m,
Vatican News
Jukwaa ambalo linalenga kuwa jukwaa la majadiliano ya kimataifa na shirikishi kwa utawala wa Mtandaoni na ndilo IGF 2025, ambalo lnafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27 Juni 2025 na ambapo linaweka wazo la mtandao wazi na salama katikati ya mjadala, kwa manufaa ya ubinadamu. Miongoni mwa hotuba zilizopangwa pia ilikuwa ni ya Monsinyo Lucio Adrian Ruiz, Katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasliano aliyeongoza ujumbe wa Kiti kitakatifu, lakini pia unaojumuisha mhandisi Francesco Masci, mkurugenzi wa Kurugenzi ya Teknolojia ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano.
Matokeo ambayo yanahusu hali ya kibinadamu
"Hatuwezi kutenganisha tafakari ya teknolojia na ile ya ubinadamu": alisisitiza Monsinyo Ruiz ambaye alikumbuka jinsi mabadiliko yanayoendelea, kutokana na akili Unde (AI), "ya kina na ya haraka" na kwamba yanabadilisha maisha na kazi ya watu. "Athari zake huenda zaidi ya uvumbuzi wa kiufundi: zinahusu hali ya binadamu, utamaduni na maana ya kuishi pamoja," alisisitiza. Katibu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano alikumbuka hati ya Papa Francisko ya Antiqua et Nova, iliyochapishwa mnamo Januari, ambayo inakaribisha "kutazama mpya kwa utambuzi, si kupinga mabadiliko, lakini kujaribu kuakisi kwa hekima ya kale, yenye uwezo wa kuongoza teknolojia kuelekea wanadamu, haki na mwisho wa kuunga mkono."
Wajibu wa kimaadili wa AI
Ikumbukwe kwamba AI si somo la kufikiri bali "ni zao la werevu wa kibinadamu na hivyo lazima liambatane na wajibu wa kimaadili". Monsinyo Ruiz hata hivyo aliorodhesha faida za kutumia Akili Unde hasa kwenye elimu hata kama "haiwezi kuchukua nafasi ya uhusiano kati ya mwalimu na mwanafunzi ambamo maadili, fikra makini na uhuru wa ndani hupitishwa." Mfano mwingine ni kwamba katika huduma ya afya ambapo inaweza kusaidia utambuzi lakini si kuchukua nafasi ya kusikiliza na huduma; katika mawasiliano hatari ni kwamba "ukweli na uhalisi" unazidi kuwa tete; katika siasa kuongeza ubaguzi na katika uwanja wa kijeshi "silaha za uhuru hazikubaliki." Juu ya mazingira ikiwa tunaweza kuchangia uendelevu, tunahitaji "teknolojia inayoheshimu nyumba yetu ya kawaida ya pamoja."
Hekima ya moyo
Kwa njia hiyo ni mwaliko wa kufanya kazi kwa uvumbuzi unaounganisha maarifa na dhamiri, uhuru na wajibu, haki na mshikamano, ambao una "hekima ya moyo". "Vatican alisisitiza Monsinyo Ruiz - inataka utawala wa kimaadili. Wakati ujao wa kidijitali utakuwa wa kibinadamu wa kweli ikiwa pia ni wa haki, unaojumuisha watu wote, wa uhusiano na muhimu kiroho. Kwa sababu hiyo, leo hii tunapyaisa Mtandao na teknolojia zote zinazoibuka kuongozwa na maadili ya pamoja, sheria za kawaida na ufahamu kwamba mwanadamu ndiye katikati, ndio kusudi lake na moyo wake”.