Kard.Parolin:hakuna maendeleo bila amani,kupinga kuzuka kwa silaha tena
Na Edoardo Giribaldi – Vatican.
"Hakuna jipya, kwa bahati mbaya hakuna jipya." Hivi ndivyo Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, alivyotoa maoni yake kando ya mkutano wa "Deni la Kiikolojia" uliofanyika tarehe 21 , Juni 2025, huko Campidoglio mjini Roma, juu ya muktadha wa kimataifa unaodhihirishwa na kuongezeka kwa mzozo kati ya Israel na Iran hivi karibuni. Kwa upande wake alisema: "Inaonekana kwangu kwamba hakuna maendeleo ya kutia moyo,"
Fedha za silaha zitumike kutatua matatizo ya njaa
Swali pia linahusu maandamano dhidi ya kurudisha silaha tena ambayo yalifanyika wakati huo huo katika mitaa ya Roma. "Ni vyema kuwe na uhamasishaji wa jumla ili kuepuka mbio za silaha. Ni sehemu ya ombi ambalo Papa Francisko alitoa katika Spes non confundit, au mwaliko wa kutumia fedha zinazotumiwa kwa silaha kutatua matatizo ya njaa."
Kazi ya kufuta deni
Suala la deni lilikuwa moja ya mada kuu kutoka katika mtazamo wa kijamii wa Jubilei ya 2000", alisisitiza Katibu Mkuu wa Vatican huku akikumbuka "kampeni kali pia iliyohamasishwa na Papa Yohane Paulo II kwa haki ya kijamii." Kampeni ambayo ilikuwa imetoa "tume" ambayo ilianza kazi tena katika hafla ya Jubilei 2025, "na ambayo sasa inataka kujaribu kutekeleza baadhi ya hatua ambazo zinaweza kushughulikia tatizo hili".
Kusaidia nchi maskini
"Tunahitaji kufuata masuala haya, sio tu kuyazingatia wakati maalum kama vile Mwaka Mtakatifu", aliongeza Kardinali Parolin. Wafuatilie kupitia kile kinachoitwa "ufuatiliaji", ambao unachukua mtindo wa wito juu ya suala la deni kutatuliwa kwa faida ya nchi masikini, ili rasilimali zinazokusudiwa kulipa majukumu zitumike kwa ajili ya maendeleo yao. Uingiliaji unaotarajiwa zaidi ni kuundwa kwa usanifu mpya wa kifedha katika ngazi ya kimataifa, kulingana na maono ya jumla ambayo yanaruhusu matumizi ya haki ya kijamii halisi,” alisisitiza.
Mkutano kati ya Papa Leo XIV na Meloni
Hatimaye, akirejea juu ya maadhimisho ya Jubilei ya watawala, (21-22 Juni),Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Parolin alithibitisha mkutano ujao kati ya Papa Leo XIV na Waziri Mkuu wa Italia Bi Giorgia Meloni. Bado hakuna tarehe kamili, lakini inapaswa kufanyika kabla ya Papa kuhamia huko Castel Gandolfo, uliopangwa kufanyika tarehe 6Julai 2025.
"Mtazamo mpya kuelekea ulimwengu mpya"
Wakati wa hotuba yake huko Campidoglio, Kardinali Parolin alisisitiza udharura wa kufanya kazi kwa ajili ya amani, akionesha hitaji la "mwonekano mpya kuelekea ulimwengu mpya, wenye uwezo wa kusoma kwa uangalifu changamoto na ishara zile za nyakati ambazo zinaweza kuchangia amani kwa kuchochea mazungumzo ya kijamii, kugundua tena ndani yao tumaini ambalo halikatishi tamaa".
Kurekebisha mfumo wa fedha
Kuhusiana na "usanifu mpya wa kifedha wa kimataifa" uliotajwa, Kardinali alibainisha jinsi ambavyo inawezekana kutekelezwa "sio tu kwa kuingiza vifungu vinavyozingatia mabadiliko ya hali halisi katika madeni, lakini pia kwa kuunda upya mfumo wa kifedha. Mfumo wa sasa wa kurekebisha deni lililoundwa haufanyi kazi, kwani unawakilisha nguvu zile zile za zamani na mpya, sio idadi ya watu."
Hatua tano za kushughulikia deni
Kwa Kardinali Parolin kisha alipendekeza hatua tano madhubuti za kushughulikia suala la deni la ikolojia: kupunguza matumizi katika Kaskazini ya kimataifa, "kusaidia kukabiliana na hali halisi ya "mataifa yaliyo katika mazingira magumu kupitia "msaada wa kifedha na teknolojia; “kusamehe deni la kiuchumi, kitendo kinachofafanuliwa kuwa “tendo la huruma linalorudisha tumaini; kukuza mshikamano wa kimataifa; na hatimaye "kuelimisha kwa uongofu wa ikolojia."