Jubilei ya Kiti kitakatifu,Sr Riva:Uzuri wa Msalaba utatukomboa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Jubilei ya Kiti kitakatifu Vatican, Jumatatu tarehe 8 Juni 2025, Sr Maria Gloria Riva Mtawa wa Jumuiya ya Wamonaki ya Waabuduo Sakramenti Takatufu Milele, alitoa tafakari kwa uwepo wa Baba Mtakatifu XIV, katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, mara baada ya Ibada ya kitubio katika fursa hiyo ya Jubilei ambapo akianza tafakari yake alimkumbuka Hayati Baba Mtakatifu Francisko na kwa kuungana na Askofu Rino Fisichela, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, aliyemfikiria yeye kama Mtawa katika tukio hilo kubwa ambalo linahusu mji wa Vatican, na Curia Romana nzima, lakini zaidi ya yote kwa upendo mkubwa, na kwa heshima ambayo Bwana ameruhusu kuzungumza mbele ya Baba Mtakatifu Leo XIV.
Sr Riva alisisitiza kuwa Kanuni ya Mtakatifu Agostino inawahusisha sana ambamo Yeye aliyelimishwa, shukrani kwa Mtumishi wa Mungu Giuseppe Bartolomeo Menochio, Mkuu wa kwanza wa shirika lao. Sr Riva alisema kuwa walijaribiwa na zaidi kwa Papa Le wa wakti ule yaani Papa Leo wa XII ambaye kwa miaka 200 iliyopita aliweza kugusa na kutangaza na kupelekea Jubilei ya mwaka 1825. Kwa hiyo, Sr alipenda kumsalimia na kuelezea shukrani zake na kuwasalimia makardinali wote na wajumbe wote wa Curia Romana na viongozi wakuu wa Vatican.
Mwongozo wa tumaini
Sr Riva aliendelea jinsi ambavyo kwa miaka 10 anaishi katika Jamhuri ya Mtakatifu Marino: thamani ya nchi ndogo sana, katika Ulimwengu ulio na utandawazi leo hii ni muhimu sana, thamani ambayo haiwezi kuacha hivi na kulinda nguvu zote za lazima. Ni nchi hizi ndogo ambazo kwa namna yake na maadhimisho yake ya kiutamaduni, yanatunza uhai wa tumaini katika ulimwengu wenye hatari ya kupoteza mizizi yake ya kihistoria. Tunaweza kusema, kwa kutumia lugha ya kawaida, ndiyo wanaoshikilia kamba ya matumaini. Nukuu hii siyo bahati mbaya. Kwa hakika, Sr Riva alielezea fikira zao kwenye nukuu ya kibiblia inayoonesha neno Tumaini: "tikva" (????????), neno ambalo mzizi wake lina neno kav, yaani, "kamba" au, kwa usahihi kabisa, "uzi." Kav anapendekeza picha ya kamba, isiyolegea, lakini iliyonyoshwa kati ya miti miwili. Kwa hiyo, katika Kiebrania cha kibiblia, mtu ambaye, akiwa na mizizi katika maisha yake ya nyuma, anaweza kujizindua kuelekea siku zijazo kwa kuishi wakati uliopo katika mvutano, na ana matumaini.
Usipoteze mizizi yako
Sr Riva aliuliza swali: “Je, sisi leo, katika Kanisa letu hili, katika Taifa hili dogo ambalo Kanisa ni sehemu yake kubwa, tunawezaje kuweka mvutano huu hai kati ya wakati uliopita na ujao? Usawa kati ya wakati uliopita na ujao ndio mzizi mkuu wa Matumaini. Leo tunahatarisha kuishi katika kulilia yaliyopita, kwa siku za nyuma ambazo hazipo tena, na hivyo inasababisha tamaduni ya kijadi ambayo mara nyingi imetenganishwa na usasa, au kukimbia kuelekea wakati ujao ambao haujafika, tukianguka katika wakati ujao wa udanganyifu, usio na uwezo wa kutoa ufumbuzi wa kweli kwa changamoto za sasa. Zamani, kiukweli, pamoja na uchungu wake na utukufu wake, iliwezekana kuwakilisha chanzo kikuu cha kuishi wakati uliopo katika mvutano ufaao.
Katika hili Sr Riva alikumbusha kazi ya kisanii ya Chirico yenye kichwa: “Kurudi kwa mtoto mpotevu.” Alieleza kwamba Giorgio de Chirico, Mgiriki kwa utamaduni na mtoto wa tajiri ya kiitalia, alifika Italia akiwa na miaka 18 na kujiunga na Harakati ya waamini iliyoendana na waingiliaji kati wa Vita vya Kwanza vya Kidunia. Walakini, mnamo 1917 alipolazwa hospitalini huko Ferrara, alielewa kuwa hakuna vita inayoweza kutoa wakati ujao na tumaini. Kwa hivyo, mnamo 1922, alijichora picha moja kama “Mwana Mpotevu,” mtu aliyejitengeneza mwenyewe, mwana wa (mannequin), mwenye mabega mapana, ya pembe nne na vifundo vya miguu nyembamba ambavyo vinaacha mandhari ya Mediterania na, pamoja na hayo, maagizo ya utamaduni wa Kikristo wa asili ya Kigiriki-Kilatini, kuelekea huko Ferrara nyekundu, katika minara yake na bustani zake mbele. Lakini kwa wakati huo huo katika Mfano wa Injili, jambo lisilo la kawaida lilitokea, ambapo alipata hali ya kuchanganyikiwa kwa baba ambaye, aliyechorwa kama sanamu ya Kigiriki, ikaacha msingi wake wa kumwendea (taz. Sanamu, Meubles et Généraux Il meccanica del pensiero, 277-278). Kwa njia hiyo ndiyo, maana wakati uliopita inakuja kukutana nasi na maswali yake, si kutufanya tushindwe bali kutuzindua tena katika sasa, tukitazamia wakati ujao kwa matumaini.
Kutumaini ni kuishi umilele
Hata sisi, kama vijana tunaishi katika ulimwengu mahali ambapo hata maendeleo yanaweza kuwa mtaji mkubwa lakini hata kuwa na hatari kubwa. Katika ulimwengu ambalo fursa zinazotokana na vyombo vya mawasiliano ya kijamii vinalisha aina mpya za maisha ya kijamii, kiutaduni, lakini lazima kuwa makini! Vyombo hivi vinapaswa kutazamwa kama vilivyo na kuhitaji hasa ambapo matunda yake yasiache mizizi yake, na si kujitupa katika mbio kuelekea mahali ambapo hakujulikani, lakini kujua kuelekeza , kama alivyoandika Askofu mkuu wa Hippo: “Si kukumbea kama inavyotakiwa, ikiwa ni kudharau mahali ambapo lazima kukimbilia (Taz. Mtakatifu Agostino:Unabii wa haki ya 8.19).”
Sr. Maria Gloria Riva alisema: “sisi tunadharau mahali ambapo tunapaswa kukumbilia: mbiu za Yohane na Petro kuelekea Kaburi tupu la Kristo (Yh 20,4), na ni moja ya mbio ambazo Kanisa na ulimwengu vinaweza kupitia bila woga. Ni mbio ambazo anayejua kuwa tumaini linakaa kwenye maisha ya kweli, yake ya milele. Umilele uko mbele yetu, upo mbele ya yule anayeamini na ambaye haamini, na mbele ya ubinadamu. Ikiwa tunafanya kazi pamoja kwa ajili ya mwelekeo mfupi na unafiki, tunafanya kazi bure. Hii inahitaji kufanya kazi katika mwelekeo mkubwa wa maisha ambayo hayafi: kuishi kwa kujiuliza kila siku, ikiwa kile ambacho tuko tunafanya kinaendana na uthabiti wa ukweli ule ambao ni upendo na umilele (Mt. Agostino katika Maungamo Kitabu 7,10.16): Haya ni matumaini: Kutumaini ni kuthibitisha ukweli ambao unaheshimu maisha, kuanzia kutungwa kwake hadi mwisho; kwa kuheshimu hadhi ya kila mtu, mbali na imani yake au utaifa wake; ambaye anaheshimu matumini na utamaduni maalum kwa kila mtu, utajiri mkubwa wa ulimwengu.
Je, ni nini, baada ya yote, maana ya kina ya Jubile ikiwa si kutusaidia kufikiria kuhusu mambo ya mwisho? Sr Riva aliuliza. Sote tumeguswa na ufupi wa kuwepo na sote tuna wajibu wa kujiuliza kuhusu maana ya maisha yetu. Maswali kama haya yanaweza kusababisha usumbufu kwa roho, hisia ya kutostahili au kutofaulu, lakini ni katika nyakati kama hizo kwamba mtoto mdogo ambaye, kulingana na Charles Peguy, ni tumaini, anajidhihirisha (Rej. Charles PÉGUY : Mlango wa fumbo la wema wa pili). Ndiyo, ikiwa imani na upendo ni muhimu kwetu kuishi uhusiano na Mungu na wanadamu, tumaini ni muhimu kwetu kuelewa njia ya historia.Umuhimu wa Peguy ni ule wa kuturudisha kwenye uhusiano wa kina kati ya tumaini na unyenyekevu. Wanyenyekevu ndio wenye nguvu kweli kweli, wenye uwezo wa kutazama maisha, kama Victor Hugo alisema, bila kutazama kwa mazoea lakini kwa macho ya kustaajabisha (Rej. Charles PÉGUY: Veronica. Mazungumzo ya kihistoria...). Unyenyekevu pia hushinda nguvu za adui mkuu wa mwanadamu ambaye ni Mwovu na ambaye hushambulia kwa usahihi mahali ambapo utakatifu ni mkuu zaidi na ambapo (ambapo kuhusu Nchi ya Vatica) nguvu ya Kristo imejidhihirisha kwa wingi zaidi kwa wale wanaomtumaini. Kwa hiyo ni lazima tujizatiti kwa unyenyekevu ili kutambua, kwa macho ya ajabu, hatua ndogo lakini za uhakika za matumaini.
Sakramenti ya Ekaristi ya matumaini yetu
Mwanzilishi wetu, Mwenyeheri Maria Magdalene wa Umwilisho, aliandika kwamba maneno ya mwisho ya mtu mtakatifu ndiyo ya muhimu sana kukumbuka; wale ambao huweka tumaini la wale waliobaki. Hivyo maneno ya mwisho ya Kristo yalikuwa yale ya Karamu ya Mwisho. Aliunganisha imani katika Baba na tumaini la uzima wa milele na upendo kati yetu. Kwa hiyo tumaini limeunganishwa kwa karibu sana na shauku kuu ya Yesu: kwamba “wote wawe wamoja.” Ekaristi ni viaticum ya matumaini ya uzima wa milele na inafunga pamoja kwa namna ya ajabu yaliyopita, ya sasa na yajayo. Tunajua pia kwamba katika Ekaristi umoja wa watu wote unaoneshwa na kutolewa. Hata hivyo, kujua hili haitoshi, ni lazima tuamini na kulithibitisha kwa uwepo wetu wote kama wanaume na wanawake wa amani na umoja. Ni kwa vipi basi tunaweza kushinda ndani yetu macho tuliyozoea na kukuza mtazamo wa unyenyekevu wa kustaajabisha? Sr Maria Gloria Riva, alieleza kuwa katika wakati wa dhiki kuu (kama ile ya Napoleon pamoja na kutekwa nyara kwa Papa Pio VII na uharibifu wa Curia Romana). Yesu alionesha kwa Mwanzilishi wetu, kwa hakika mji wa Roma kama mahali pa kuanzia kazi yake.
Papa, ambaye wakati huo alikuwa akiishi (Quirinale -Ikulu ya sasa ya Italia), alielewa umuhimu wa msingi huu na alitaka monasteri yetu ya kwanza kuwa karibu naye. Na ingawa Mama Maria Magdalene aliyehamishwa huko Firenze angeweza kuanzisha Shirika lake huko, Yesu alitaka kwamba kutoka Roma, kutoka katikati ya Ukristo, mwaliko mkubwa wa kuweka mtazamo wa kuabudu juu ya Ekaristi utokee na kutoka hapo upate nguvu, sala na mwanga wa kuongoza ubinadamu na Kanisa, kama Mtakatifu Agostino ambaye bado angesema, kati ya mateso ya ulimwengu na faraja ya Mungu. (rej. Mtakatifu Agostino katika Dei, XVIII, 51, 2: PL 41, 614). Kutazama kuelekea Sakramenti Takatifu zaidi, kama kumtazama yule nyoka wa kale wa shaba, kunaweza kutuponya kutokana na uovu, kunaweza kusafisha mitazamo yetu na kutufanya tuwe na uwezo wa kutoa unabii. Hatupaswi kuogopa, tuna mshirika mkuu katika Mungu. Anatupenda kwa upendo wa milele na atatuhurumia daima (Taz. Yer 31:3).
Tunachopaswa kufanya ni kujiachilia kuumbwa naye na kutekeleza baada ya muda maangazio ambayo Roho Mtakatifu hututolea kwa usahihi kwa njia ya Ekaristi na Bikira Maria, ishara ya matumaini ya hakika. Nukuu ambayo mara nyingi hutumiwa vibaya ni ya Fyodor Mikhailovich Dostoevsky: uzuri utaokoa ulimwengu. Nukuu hii sio sahihi kwa sababu Mfalme Myskin katika riwaya maarufu ya Kirusi The Idiot (mjinga)kweli anauliza swali la kushangaza: ni uzuri gani utaokoa ulimwengu? Mfalme huyu kiukweli, anajikuta mbele ya Kristo Aliyekufa wa Holbein, kazi ya kutisha ambapo Kristo aliyepakwa rangi ya ukubwa wa maisha anawasilisha uso wenye macho na ncha zilizozama ambazo tayari zinaonesha ishara za majaraha ya seli katika tishu hai(nekrosisi.) Kwa hiyo swali ni zito. Uzuri gani utatuokoa? Je, uzuri wa msalaba utaokoa ulimwengu? Uzuri wa kushindwa? Ndiyo, msalaba bado unaweza kutuokoa, msalaba uliokaribishwa na kutolewa. Tumeishi kwa miaka migumu kati ya kashfa na mabishano, lakini katika ishara hii kubwa bado tunaweza kushinda. Uzuri huu mkubwa wa kupoteza utatuokoa. Matumaini hutokea pale ambapo machozi ya uchungu na toba huirutubisha nafsi katika unyenyekevu na upya wa maisha.
Ishara ya tumaini hakika
Pia tuna mshirika mwingine mkubwa, Malkia wa uzuri: Bikira Maria. Kwa hivyo Sr Riva aliacha mfano wa picha moja ya mwisho ya Mama wa Bandari ya Lligat, iliyochorwa na Salvador Dalì, baada ya mlipuko wa bomu la atomiki. Ishara ya mkasa ambayo sayansi na mbinu iliyojitenga na maadili inaweza kutusababishia Maria ambaye ana sura ya mke wa Gala, chanzo cha faraja kubwa kwa msanii huyo. Katika uchoraji, ishara za uharibifu zinaweza kuonekana kila mahali: Eneo ambalo Maria amesimama ni la kale lakini limevunjika kabisa; vivyo hivyo taasisi zetu, za kale lakini mara nyingi zina dalili za kuzorota. Samaki, ambayo ni ishara ya Kikristo, imelala ambayo sasa imekufa na milima imesimamishwa juu ya maji. Wakati huo huo, hata hivyo, msanii ametawanya kazi hiyo na ishara za kuzaliwa upya kama vile yai katikati ya upinde, malaika wenye mikono iliyonyooshwa na wanawake wajawazito (sawa na Bikira Maria). Msanii huyo, katika wakati huo mfupi wa imani inayokaribia, alitaka kuthibitisha kwamba Maria anatulinda katika kushindwa kwetu na katika uwezo wetu anapomlinda Mtoto anamweka magotini.
Utumbo wa huruma wa Maria na Mtoto wa Kimungu unawakilishwa na vibao vilivyo wazi kama Milango ya matumaini ya Jubilei. Ikiwa katikati ya tumbo la uzazi la Maria kuna Yesu, katikati ya tumbo la Mtoto wa Mungu kuna Mkate wa Ekaristi. Akiutazama mkate huu, Kristo anashikilia vitu viwili vilivyoning'inizwa mikononi mwake: ulimwengu na neno: hekima ya kibinadamu na hekima ya kimungu. Hivyo Yesu anatufundisha kugundua upya njia za matumaini kwa kukazia mitazamo yetu kwanza kwenye Mkate wa Ekaristi, ili kupata nguvu kutoka zamani ili kutafsiri mambo ya sasa kwa njia ya asili na kubeti juu ya siku zijazo na hatimaye, kutumaini msaada wa bidii wa Maria, Salus Populi romani, Ianua Coeli, mlango wa matumaini na Faraja. Naam, Maria, Mama wa Faraja na Matumaini, utuombee, alihitimisha Mtawa huyo yalifuatia maandaamano na Baba Mtakatifu Leo akiwa na Msalaba kuelekea Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.