Jubilei 2025:Ondoleo la madeni kiekolojia
Vatican News
Ujumbe wa mada ya"Jubilei 2025: msamaha wa deni la ikolojia", ”, uliotiwa saini na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu ulichapishwa tarehe 24 Juni 2025, ambao unaweza kupakuliwa katika lugha 5. Hati hiyo inaelezea jinsi ambavyo deni la kifedha na deni la kiikolojia leo hii linawakilisha pande mbili za sarafu moja. Wakati kwa upande mmoja, nchi zinazoendelea zimelemewa leo na deni la kiuchumi ambalo lina mizizi ya mbali na kwamba janga hilo limezidi kuwa mbaya, pia zinakabiliwa na athari mbaya zaidi za mzozo wa tabianchi, licha ya kutokuwa miongoni mwa wahusika wakuu wa hilo.
Kufutwa kwa deni la nchi masikini aidi ni ishara ya haki
Lakini nini maana ya deni la kiikolojia hasa? Ujumbe huo unaakisi jinsi uchumi ulioendelea zaidi kiviwanda, ndio wasanifu wakuu wa shida ya tabianchi, pia kutokana na unyonyaji wa maliasili za nchi masikini, ambazo hata hivyo hazina "rasilimali za kiuchumi na miundombinu zinazohitajika kurekebisha au kuguswa," na hivyo kuzidisha mzozo wa kiuchumi na shida ya mazingira, na matokeo yasiyoweza kuepukika kwa maendeleo ya watu. Kwa mtazamo huu, kufutwa kwa deni la kifedha ambalo linazielemea nchi maskini zaidi hakupaswi kuonekana kama ishara ya mshikamano na ukarimu, bali kama ishara ya haki ya kurejesha.
Mpango huu ni ujenzi mpya wa muungano kati ya watu
Mpango kama huo hautakuwa kitendo cha kuadhibu, lakini badala yake ni viaticum kwa ujenzi wa muungano mpya kati ya watu, ambao una haki ya kijamii na kujali uumbaji moyoni. Ukisukumwa na Jubilei ya Matumaini na kuongozwa na maneno ya Baba Mtakatifu Leo XIV, Vatican kwa kanuni za Mafundisho Jamii, inapyaisha dhamira yake ya kichungaji kwa haki ya kiikolojia, kijamii na kimazingira. Kwa sababu hiyo, waraka unaalika Makanisa mahalia kukuza, katika mazingira tofauti ya kijamii, uwongofu muhimu wa ikolojia, "binafsi na jumuiya".
Ikumbukwe kwamba kazi hii imetumia uchambuzi wa pamoja wa CAFOD() Shirika la misaada la kimaendeleo la Kikatoliki, Mtandao wa Haki na Ikolojia wa Kijesuit - Afrika (JENA) na , ambao ulipelekea kuchapishwa kwa waraka wa Kuziba Mgawanyiko wa Kaskazini-Kusini: Wajibu wa Pamoja wa Haki ya Kiuchumi na Ikolojia.