杏MAP导航

Tafuta

2025.05.21,Bingwa wa Olimpiki Letsile Tebogo pamoja na wanariadha wa Vatican. 2025.05.21,Bingwa wa Olimpiki Letsile Tebogo pamoja na wanariadha wa Vatican. 

Wanariadha Vatican,kutoka Jubilei ya Michezo msukumo wa matumaini

Katika fursa ya tukio la Jubilei ya tarehe 14 Juni 2025,utafanyika Mkutano wa kimataifa katika Chuo cha Kipapa cha Augustinianum ambapo Kardinali de Mendonca na wanariadha 4 wa kimataifa miongoni mwao ni wa Olimpiki ya mita 200 huko Paris watashiriki.

Na Giampaolo Mattei na Angella Rwezaula – Vatican.

Jubilei ya Michezo imeratibiwa kwa siku ya Jumamosi 14 na Dominika 15 Juni 2025. Siku mbili zitafunguliwa kwa mkutano wa kimataifa kuhusu "Msukumo wa matumaini" ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Saa 3.00 asubuhi katika Ukumbe wa Augustinianum, kupitia njia ya Paolo VI. Kwa mtindo wa mazungumzo na ushuhuda wa "chini-chini," Kardinali José Tolentino de Mendonça na Mwenyekiti wa Baraza hilo na Thomas Bach, Rais   anayemaliza muda wake  wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki  walio madarakani hadi tarehe 23 Juni, watazungumza kwanza.

Wanariadha wanne watashirikisha historia zao. Sergio Conceição, Mreno, kocha wa Milan na mwanasoka wa zamani wa Porto, Lazio, Parma na Inter na pia katika timu ya taifa ya nchi yake. Letsile Tebogo (umri wa miaka 22 mnamo 7 Juni), bingwa wa Olimpiki katika mita 200 kwenye Michezo ya Paris 2024, gwiji wa kweli katika Botswana yake na Afrika yote.Tarehe 29 Agosti iliyopita alikutana na Papa Francisko akishiriki, hasa, kumbukumbu ya mama yake aliyefariki kutokana na saratani. Valentina Vezzali, mmoja wa walinzi hodari zaidi katika historia na medali zake tisa za Olimpiki (dhahabu sita) na ubingwa wa ulimwengu 26 (dhahabu kumi na sita). Amelio Castro Grueso, pia mpiga uzio, mhusika mkuu wa Timu ya Wakimbizi ya Olimpiki ya Walemavu kwenye Michezo ya Paris.

Mcolombia, mama yake aliuawa alipokuwa na umri wa miaka 16. Alipoteza matumizi ya miguu yake katika ajali ya gari na kuwezekana katika mchezo, lakini juu ya yote kwa imani, njia ya ukombozi katika maisha. Mazungumzo hayo yatahusisha Giampaolo Mattei, rais wa Riadha Vatican; Padre wa Hispania Litus Ballbé Sala (mshindi wa medali ya Olimpiki ya magongo huko London 2012); Paola Gigliotti (Sentiero Frassati); mtawa wa Kisalesia Francesca Scialbetta na mpiga picha Giovanni Zenoni. Wasimamizi watakuwa Novella Calligaris, mwandishi wa habari wa Rai News 24 na nyota wa kuogelea asiyesahaulika, na Alessandro Gisotti, naibu mkurugenzi wa uhariri wa vyombo vya habari vya Vatican.

22 Mei 2025, 16:44