杏MAP导航

Tafuta

2025.05.03 Jubilei ya watoto wa METER 2025.05.03 Jubilei ya watoto wa METER 

Siku ya Watoto Waathirika,Hija kupitia Mlango Mtakatifu

Chama cha Meter kilichoanzishwa na Padre Fortunato Di Noto kilisherehekea hafla yake ya 29 ya kila mwaka kwa kuandamana na baadhi ya manusura wa unyanyasaji kuvuka mlango Mtakatifu wa Kanisa la Mtakatifu Petro.Ushuhuda:"Ni muhimu nyuma yako kuwa na safari ya imani,vinginevyo,huwezi kuifanya peke yako."

Vatican News

Ni vigumu kuelezea wakati ambapo maumivu yanapata ujasiri wa kufanya njia yake. Hasa linapokuja suala la majeraha ambayo hayafanyi kelele, lakini kukaa kimya kwa miaka, huku yakijichimbia ndani ya mwili na roho. Hata hivyo, jumuiya inapokuwa ni mbebaji wa mchakato huu, inaweza kuwa nyumba ya pamoja yenye uwezo wa kukaribisha, kulinda na kusindikiza hata kupita Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro na baadhi ya manusura wa dhuluma na nyanyaso. Haya ndiyo yaliyojiri Jumamosi tarehe 3 Mei 2025, katika maadhimisho ya Siku ya XXIX ya Watoto Wahanga, iliyohamasishwa na Chama cha METER, kilichoanzishwa na Padre  Fortunato Di Noto, ambao waliandaa hija ya jijini Roma katika muktadha huu wa Jubilei ya Matumaini.

Jubilei ya chama cha METER
Jubilei ya chama cha METER

Tukio ambalo kila mwaka linaunga mkono na kuzingatia wale ambao, katika maisha, walianza na mpando. Pia ni kwa mara ya kwanza kwa chama, pamoja na kundi la waathirika wa unyanyasaji na kunyonywa- ikiwa ni pamoja na kesi zilizotokea ndani ya Kanisa kufanya ishara hii muhimu katika Mwaka Mtakatifu ambao unahamasisha mada kuu ya Matumaini yasiyo katisha tamaa. Na chaguo la kufanya hivyo katika muktadha wa Jubilei ni wenye nguvu, ambapo tumaini haliepukiki, bali ni thabiti kabisa. Hata zaidi kwa sababu vidonda vingine vinabaki milele, alisisitiza Padre  Fortunato akizungumza na  vyombo vya habari vya Vatican, na kwa sababu alisema “unyanyasaji daima ni mbaya huku  mwanzilishi wa Meter, akimnukuu Papa Francisko ambaye alifafanua unyanyasaji kamamauaji ya kisaikolojia ambayo mtu huharibiwa.

Jubilei ya chama cha METER
Jubilei ya chama cha METER

“Na bado, ikiwa kuna mtu anayesikiliza, kulinda na kusindikiza, kama ilivyo kwa Chama chetu,   basi majeraha hayo yanaweza kuwa nyufa za mwanga. Hapa ndipo inaibuka nguvu ya kupita  Mlango Mtakatifu, ambayo kwa hiyo inakuwa ishara ya safari yenye jina na uso, iliyofanywa kwa ukaribu, kusikiliza, msaada wa kisheria na kisaikolojia, kiroho, na  kulinganisha. Ya uwepo wa mara kwa mara. Na kwa sababu alisisitiza Padre Fortunato akitumia neno analotumia kuwaita walionusurika kuwa “mmoja wetu aliyeokolewa, kila mara anarudia: Sikujiokoa peke yangu.”

Jubilei ya chama cha Meter
Jubilei ya chama cha Meter

Kando ya njia hii, bado kuna changamoto ya kila wakati ya dijitali. "Leo hii faragha mara nyingi inahakikishwa kwa mnyanyaswaji zaidi  ni mtoto.” Chama cha Meter  kimekuwa kikitoa onyo kali  juu ya hili kwa miaka, na malalamiko rasmi, ripoti, vikao vya Bunge na katika ngazi ya Ulaya. Lakini watoa huduma za sever huhakikisha kutokujulikana zaidi kuliko ufuatiliaji.” Kwa njia hiyo  alisisitizia juu ya uwepo wa vita sana kwamba “Tukio la siku mbili jijini Roma ni kilio, lakini pia ni mwanga. Sio tu kwa upande wa waathirika, lakini kwa kila mtu: kuwa pamoja, kuwapo, mitandaoni. Hii inabadilisha mambo. Alihitimisha kwa kusali kwamba “ “Bwana, tusaidie kutumaini kwako: utusaidie kwa nguvu za Roho Mtakatifu katika kujitolea kuwalinda na kuwalinda wadogo katika Kanisa na katika jamii.”

 

04 Mei 2025, 13:54