Dk.Paolo Ruffini ashinda Tuzo ya Shirika la Mawasiliano na Utamaduni la Paoline Odv
Vatican News
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, Dk. Paolo Ruffini, ametunukiwa Tuzo ya Paoline 2025, iliyotolewa na Shirika la Mawasiliano na Utamaduni la Paoline Odv kwa waendeshaji wa vyombo vya habari ambao wamejipambanua kwa kutoa usemi bora zaidi wa ujumbe wa Papa kwa Siku ya Mawasiliano ya Kijamii duniani. Tuzo hiyo inapokelewa tarehe 27 Mei 2025.
Dk Ruffini ni kielelezo cha umuhimu wa mtazamo wa mawasiliano
Kama ilivyoelezwa katika sababu ya Tuzo hiyo inabainisha kuwa “kwa Dk. Ruffini ni kielelezo cha umuhimu mkubwa katika mtazamo mzima wa mawasiliano ya Vatican na kwa ujumla zaidi katika ulimwengu wa vyombo vya habari vya Kikatoliki. Kupitia uzoefu wa kina katika uwanja wa mawasiliano, wa kilimwengu na wa kidini, ameunda mtindo wa kujumuisha na wa mazungumzo, akiimarisha ulinganisho wa mawazo. Kazi yake daima imekuwa na alama ya uaminifu kwa ujumbe wa kiinjili, kusikiliza na kutafsiri ishara za nyakati."
Kozi ya mafunzo:Shiriki kwa upole tumaini mioyoni mwenu
Tuzo hiyo itatolewa na Sr. Paola Fosson, rais wa Chama cha Mawasiliano na Utamaduni cha Shirika la Mtakatifu Paulo(Odv,) Jumanne tarehe 27 Mei 2025 jijini Roma, katika Chuo Kikuu cha Lumsa, wakati wa kozi ya mafunzo juu ya mada: "Shiriki kwa upole tumaini lililo mioyoni mwenu" iliyohamasishwa na Shirika la Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Lazio, Jumuiya ya Waandishi wa Habari wa Kiitaliano(UCSI) ya Lazio na Jumuiya ya Wakatoliki wa Italia(WeCa) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Lumsa, Jumuiya ya Mawasiliano na Utamaduni ya Paoline(Odv,) Shirikisho la Juma la Kikatoliki la Italia (FISC) ya Lazio na Ofisi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Katoliki wa Mkoa wa Lazio.