Maaskofu wa Ulaya:amani ya haki na ya kudumu inahitajika kwa vita vya Ukraine!
Vatican News
Amani ilikuwa, mojawapo ya mada kuu zilizojadiliwa katika Mkutano wa Baba Mtakatifu Leo XIV aliokutana nao mjini Vatican tarehe 23 Mei 2025 kwa urais wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu ya Umoja wa Ulaya (COMCE). Katika mkutano huo “ilikuwa na umuhimu mkubwa kwetu, kwa sababu ilifanyika siku chache baada ya kuchaguliwa kwa Papa Leo na zaidi ya mwezi mmoja baada ya kifo cha Papa Francisko,” alisema hayo Askofu Crociata. Papa alitaka zaidi ya yote kutusikiliza kwa uhuru, bila kutoa maoni yoyote katika hatua hii, na katika hili tuliona umakini mkubwa kwa upande wake kwa taasisi ya Ulaya, iliyozaliwa kama mpango wa amani, na kwa utendaji wake." Leo hii inakabiliwa na wakati mgumu wa makabiliano na utawala mpya wa Marekani, ambao ulichukua madaraka mwanzoni mwa mwaka, na pia na mabadiliko ya mtazamo katika maoni ya umma, ambayo yanaona kuenea kwa matukio ya wasiwasi kama vile ushabiki ambao mara nyingi unakuwa kinyume na kanuni kuu za Umoja wa Ulaya", alisema rais wa Comece.
Gharama za vita ambazo zina uzito juu ya wadhaifu zaidi
Naye Mmoja wa makamu wa rais wa Comece, Askofu Mkuu Antoine Hérouard, alisema kuwa walipata msisitizo wa Papa Leo XIV kuhusu matokeo ya kiuchumi na kijamii ya mzozo wa Kiukraine juu ya maisha ya watu. Fedha zaidi za kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama haziwezi kuendana na misaada kidogo kwa wale wanaoteseka au wanaoishi katika shida.” Ukweli halisi ambao umejidhihirisha, kwa mfano, na kuongezeka kwa bei ya nishati.
Kwa mujibu wake alisema "Hatukuingia kwa undani, lakini sote tulisimama kufikiria hitaji la kufikia haraka amani ya haki. Ulinagnifu kati ya amani na haki ni ya msingi." Makamu mwingine wa rais, Askofu Rimantas Norvila wa Lithuania, aliakisi jinsi ambavyo bado hatuoni masuluhisho madhubuti, leo nchi zote za Ulaya lazima zijisikie zinahusika katika lengo la kusimamisha vita haraka iwezekanavyo". Uhamiaji pia ulikuwa miongoni mwa mada za kutafakari wakati wa Mkutano. Makamu mwingine wa rais, Askofu wa Ureno Nuno Brás da Silva Martins, alizungumza kuhusu hilo katika mkutano na waandishi wa habari. Kwa upande mmoja, "kuna haja ya Ulaya kuwakaribisha wahamiaji pia ili kukabiliana na kupungua kwa idadi ya watu", lakini kwa upande mwingine, kutokuwa na uwezo fulani wa kuunganisha wale wanaowasili kwenye mipaka yetu ni dhahiri. Ni tatizo linalohusu heshima kwa mtu katika hadhi yake yote", na ambalo linahusisha mada ya mizizi ya Kikristo ya Ulaya.
Msisitizo wa Papa Leo XIV wa kusindikizana na vijana na kueneza imani
"Mengi zaidi ya hayo, Papa Leo XIV alisisitiza kusindikizana na vijana na kusambaza imani katika familia. Askofu Crociata na Hérouard waliakisi hilo. Wakati Czeslaw Kozon, Askofu wa Copenhagen, na mwakilishi kama makamu wa rais wa Comece pia wa Mabaraza ya Maaskofu ya Skandinavia, wote waliweka mkazo, hasa, juu ya kujifuta kutoka katika orodha ya kumbu kumbu za ubatizo. Kwa mujibu wao wanabainisha kuwa ni jambo ambalo linaongezeka katika nchi nyingi, kama vile Ubelgiji na Uholanzi. Mbali na suala la watoto kuwashutumu wazazi wao kwa kuwawekea chaguo la imani, pia kuna suala la kuingilia Serikali katika maisha ya Kanisa na katika mpangilio wa miundo ya Kanisa, jambo ambalo linahatarisha kutilia shaka uhuru wa kidini.
Na hapo walisema kuna haki na wajibu wa wazazi kuwafundisha watoto wao. Hivi karibuni kunaweza hata kuwa na uamuzi wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu juu ya hatua hii, kwa sababu watu ambao wanataka kufuta usajili wao, mara nyingi kwa sababu za kiitikadi, pia hufanya hivyo kwa kutumia sheria za Ulaya juu ya usindikaji wa data za kibinafsi." Kwa hiyo, Padre Manuel Barrios Prieto, katibu mkuu wa COMECE, alisema kwa vitendo, ikiwa badala ya maelezo ya shauku tu ya kutokuwa mfuasi wa Kanisa Katoliki ('kutobatizwa') pembezoni mwa jina, tunapaswa kuelekea kwenye kufutwa kiukweli katika orodh ya kitabu cha ubatizo, hii kwa hakika itasababisha shambulio la uhuru wa Kanisa na ukosefu wa heshima wa uhuru wa Kanisa.”