Makardinali wako kwenye kikanisa cha Sistine!
Na Angella Rwezaula.
Hatimaye Extra omnes! Wote nje! Na mlango umefungwa na Mshehereheshaji wa Liturujia za kipapa! Hata hivyo jioni hii tarehe 7 Mei 2025, baada ya kuingia katika Kikanisa cha Sistine wakiimba litania, kwa maanadamano Maneno yafuatayo ya kiapo cha Makardinali wapiga kura 133, iliyosomwa katika Kanisa la Sistine kuanzia kwa Kardinali Pietro Parolin, anayeongoza Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa lugha ya Kilatini:
“Sisi, sote na kila mmoja wa Makardinali wateule waliopo katika uchaguzi huu wa Papa Mkuu, tunaahidi, tunafanya na kuapa kuzingatia kwa uaminifu na kwa uadilifu Maandiko yote ya Katiba ya Yohane Paulo. II, Universi Dominici Gregis, iliyotolewa tarehe 22 Februari 1996. Vivyo hivyo, tunaahidi, kuchukua na kuapa kwamba yeyote kati yetu, kwa mwelekeo wa kimungu, atachaguliwa kuwa Papa wa Roma, atajitolea kutekeleza kwa uaminifu huduma ya Petro(Petrinum) ya Mchungaji wa Kanisa la ulimwengu wote na hatakosa kuthibitisha na kutetea kwa bidii haki za kiroho na za kimwili, pamoja na uhuru wa Makao Matakatifu. Zaidi ya yote, tunaahidi na kuapa kuzingatia kwa uaminifu mkubwa na kwa kwa wote wawe makleri na hata walei, usiri wa kila jambo ambalo kwa namna yoyote ile linahusu uchaguzi wa Papa wa Roma na juu ya kile kinachotokea mahali pa uchaguzi, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhusu uchunguzi; kutokiuka usiri huu kwa njia yoyote ile wakati au baada ya uchaguzi wa Papa mpya, isipokuwa idhini ya wazi imetolewa na Papa mwenyewe; kamwe kutounga mkono au kupendelea uingiliaji wowote, upinzani au aina yoyote ya uingiliaji kati ambayo mamlaka ya kiulimwengu ya utaratibu na kiwango chochote, au kikundi chochote cha watu au watu binafsi, wanaweza kutaka kuingilia uchaguzi wa Papa wa Roma”.
Makardinali wateule binafsi, kwa mujibu wa utaratibu wa utangulizi wa Daraja hizo tatu – za maaskofu, mapadre, mashemasi - walikuwa kiapo, daima katika lugha ya Kilatini, kwa maneno yafuatayo:
"Na mimi, N. Kardinali N., naahidi, nitajifunga na kuapa", na, akiweka mkono wake juu ya Injili, aliongeza: "Basi nisaidie Mungu na Injili hizi Takatifu."
Wa kwanza kula kiapo alikuwa Kardinali Parolin. Wakati huo huo, umati mkubwa umekusanyika tangu asubuhi ya leo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na unatazama kwenye bomba la moshi juu ya paa kikanisa cha Sistine. Skrini kubwa zinafuatilia ufunguzi wa moja ya wakati wa ishara katika maisha ya Kanisa mmoa mahali alipo kuzungukia maeneo ya Vatican anaona: kuchaguliwa kwa Papa. Tayari yuko katikati ya makadinali 133, na ulimwengu utamjua hivi karibuni ni nani ma maongozi ya roho Mtakatifu.