Kard.Semeraro,Wenyeheri wapya wanatufundisha thamani ya msamaha na upendo kwa wote!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ni siku nane zimepita, Kanisa la Poland linajitajirisha kwa zawati ya wenyeheri wapya 16. Katika kutangazwa kuwa mwenye heri Padre Stanis?aw Streich, kulikofanyika Jumamosi iliyopita,Mei 24 huko Poznań, inafuatia leo hii ya Kristofora Klomfass na wenzake 14, watawa wa kike wa shirika la Mtakatifu Caterina. Ndivyo alivyoanza mahubiri yake, Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, kwa niaba yake Baba Mtakatifu, wakati wa Misa ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu huyo na wenzake 14 kuwa wenyeheri huko Braniewo nchini Poland, Jumamosi tarehe 31 Mei 2025. Kardinali Semeraro alisema, wenyeheri hawa waliteseka sana kwa ajili ya ushuhuda wa imani katika muktadha wa mapambano ya itikadi ambayo barani Ulaya katika wakati wao ilipanda mateso na vifo, vurugu na uharibifu. Katika muktadha wa kipindi hicho cha miaka 80 iliyopita, mwishoni mwa Vita ya pili ya dunia, Kardinali Semeraro alipenda hata kwa siku hiyo kwa kutangazwa kwa wenyeheri 15 watawa wa kike kufanya kumbukumbu ya waathirika wengi wa migogoro na kwamba sala iinuliwe kwa ajili ya amani ulimwenguni kote, kwa namna ya pekee wazo la vita ambavyo vinaendelea nchi ya karibu na Poland.
Kardinali Semeraro aliomba kupaza sauti kwa mara nyingine na Mtakatif Paulo VI ambaye Papa Leo XIV alipenda kumnukuu kwa mara nyingine katika Sala yake ya kwanza ya Malkia wa Mbingu kuwa “Kamwe pasiwepo na vita”(Rej Regina Caeli, 11 Mei 2025) hasa mahali ambapi vinawakumba kwa ukatili wasio na hatia, wengi wao wakiwa watoto. Aligeukia somo lililosikika awali kutoka Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi, Kardinali Semeraro alisema katika hili kuna ufupisho wa maisha na kifo cha Wenyeheri wapya. Katika sababu ya upendo huu moyo umeshikilia wema, ili kutumia kielelezo cha Paulo kwa sababu anagundua ukweli mkuu wa historia, ambayo wema unashida daima ubaya. Kwa ujasiri huo Wenyeheri wetu wapya wamejiweka mbele ya wale ambao wakati huo walionekana kuwa na nguvu zaidi na ambao, kwa kulewa na kupenda mali, waliweka mahali pa Mungu mmoja wa kweli, sanamu dhaifu za wanadamu, badala ya ujumbe wa kiinjili wa upendo wakaweka itikadi ya chuki na vurugu. Ni nini matokeo ya mgongano huu usio na usawa? Wenyeheri leo hii wanathibitisha tena kwa ushuhuda wao thamani ya kudumu ya Mungu na wema, huku wauaji wao wanakumbukwa kwa ukatili tu wa uovu walioutenda.
Sr Kristofora Klomfass na wenzake, kinyume na wauaji wao na kitovu cha kiitikadi ambacho walitoka, wanathibitisha milele kile ambacho Papa Benedikto XVI aliandika katika Waraka wake wa Caritas in Veritate kwamba: "Wakati Mungu anaanza kupatwa, uwezo wetu wa kutambua mpangilio wa asili, kusudi na 'nzuri' huanza kutoweka" (CV, 18). Kwa maana hiyo, tunapaswa kutoa maana ya pekee ya kuimba siku ya leo, pamoja na Bikira Maria, Mkuu wa sifa na shukrani kwa Mungu anayetazama unyenyekevu na kuutukuza, anafanya mambo makuu kwa wale wanaotumaini upendo wake, anawaita heri maskini wa roho.Kardinali Semeraro aidha alipenda kurudia pamoja na umati huo yale maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, mwana mtukufu wa taifa hilo, ambaye katika tafakari yake ya katekesi juu ya Magnificat wimbo wa sifa wa Maria alisema: “Kwa usomaji wake wa hekima wa historia, Maria anatutambulisha ili kugundua vigezo vya tendo la ajabu la Mungu. Yeye, akipindua hukumu za ulimwengu, anakuja kusaidia maskini na wadogo, kwa hasara ya matajiri na wenye nguvu na, kwa njia ya kushangaza, huwajaza wema wanyenyekevu, ambao huweka uhai wao kwake " (Katekesi, 6 Novemba 1996) na kuachwa katika Mungu. Katika ushuhuda wa Wenyeheri wetu wapya, kigezo hiki kinadhihirika kwa namna yakuigwa mfano. Kweli wenye nguvu ni wale ambao wamejifunza kusema pamoja na mtume: Tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu, Yesu Kristo (rej. Flp 4:13).
Sr Kristofora Klomfass na wenzake 14 wanatupatia somo maalum leo. Kwanza kabisa, wanapinga utamaduni wa chuki na migawanyiko, ambao umeenea sana katika jamii ya leo. Kwa hakika ni mashahidi wasadikisho wa uwepo wa Mungu katika historia, mbele ya wale ambao, wakimkana Mungu na neno lake la ukweli na uzima, wanakanyaga utu wa mwanadamu. Leo, pamoja na kusherehekea kutangazwa kwao kuwa wenyeheri, historia yao haichochewi kulipiza kisasi au kuomba fidia kutoka katika haki ya binadamu, bali kupokea utoaji wa kile walicho nacho ambacho ni cha thamani zaidi: msamaha, upendo na huruma kwa kila mtu. Sauti za dhamiri ambazo haziwezi kunyamazishwa, manabii wa amani daima duniani na wa ubinadamu waliopatanishwa na wenye usawa, wanatuletea kila mmoja wetu maneno mawili: msamaha na uongofu. Wanatualika tusamehe, yaani, kutuondolea huzuni ya chuki na hasira. Wanatuhimiza tugeuke na kuongoka: katika mazingira yetu ya kuishi, tukichagua kila siku amani, udugu, heshima kwa uhuru wa wengine, utulivu katika mahusiano ya kibinadamu. Tuwasherehekee Wenyeheri hawa wapya, tusiache mafundisho na mifano yao ianguke njiani! Katika kila enzi ya historia ya Kanisa, na vile vile kwa njia kuu katika miongo ya hivi karibuni, wafia imani ni mashahidi wakuu wa ufalme wa Mungu na wa thamani ya Injili yake. Hata katika wakati wetu - kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyothibitisha katika giza la karne iliyopita, kama Papa Francisko alivyosisitiza katika robo hii ya kwanza ya milenia mpya - kuna mateso ya kweli ya Wakristo, yanayofanywa kwa silaha tofauti.
Kardinali Semeraro aliendelea kusema kuwa Mateso ya hila zaidi, wakati mwingine, yamepigana na silaha za utamaduni na mawasiliano ya kijamii. Hatua mbaya, ya uwongo na ya dhihaka, ambayo mara kwa mara hufurika nyumba na familia, akili na dhamiri. Kupinga utamaduni huu leo ??ni mauaji ya kweli ya kila siku, ahadi isiyo na matokeo kwa wale wote wanaofanya kazi ya elimu inayoitikia kikamilifu ujumbe wa Kristo na kwa ajili ya kukuza ubinadamu halisi. Ndiyo, leo tunahitaji mashahidi waaminifu, kama Wenyeheri wapya, ili kuimarisha imani iliyo dhaifu mara nyingi, kuwasha upya mwali wa matumaini katika jumuiya zetu za Kikristo, kupanua upeo wa mioyo yetu kwa ukubwa wa upendo wa kimungu. Kwa kuhitimisha Kardinali Semerarto aliomba kujikabidhi kwa Bikira Maria. Kardinali aliomba kuomba naye sala ya wimbo wa Ziara, ambayo imeadhimishwa tarehe 31 Mei. Vile vile aliongeza "Si kwa bahati kwamba leo ni sikukuu ya mlinzi wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Catherine, ambapo Wenyeheri wapya wanatoka. Mama wa Kristo na Mama yetu, Malkia wa Mashahidi, Msaada wa Wakristo na Malkia wa Poland, atimize ndani yetu wito ambao Mungu anatutolea sisi kumfuata Kristo kwa uaminifu na unyenyekevu, kutumaini kazi ya Mungu, kuwa watakatifu jinsi anavyotaka sisi.”