Jubilei ya vikundi vya Bendi za Muziki na Burudani za watu,zaidi ya 10elfu wajiandikisha kutoka nchi 90
Vatican News
Zaidi ya watu elfu kumi, wanaotoka zaidi ya nchi 90, watashiriki katika Jubilei ya Bendi na Burudani Maarufu ya watu jijini Roma Jumamosi ijayo tarehe 10 na Dominika 11 Mei 2025. Tukio maalum kwa bendi za kijeshi, taasisi, watu, wengine kutoka vijijini, michezo, shule na vyuo, pamoja na aina zote zinazohusiana na burudani maarufu duniani kote.
Mpango
Jubilei ya Bendi na Burudani Maarufu za watu itahusisha zaidi ya washiriki elfu 13, wengi wao kutoka nchini Italia, lakini pia kutakuwa na vikundi vingi kutoka Amerika, Malta, Poland, Hispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Brazil, Mexico, Australia, Argentina.
Siku ya Jumamosi tarehe 10 Mei 2025, kuanzia saa 2.00 asubuhi masaa ya Ulaya hadi saa kumi na mbili jioni, hija zilizandaliwa kwenye Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro zitafanyika kwa washiriki wote hao. Kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 jioni masaa ya Ulaya, itawezekana kuhudhuria tukio kubwa la bendi litakalokuwa katika viwanja 31 katikati jiji la Roma, likiwa na maonesho ya bendi na vikundi zaidi ya 100 kutoka ulimwenguni kote. Orodha ya maonyesho, pamoja na eneo lao, wakati wa kuanza na kikundi cha bendi kilichopo, inaweza kuiona kupita kwenye tovuti rasmi ya Jubilei na kwenye programu: Iubilaeum25.
Misa na Askofu Mkuu Fisichella
Hatimaye, Dominika tarehe 11 Mei 2025, Misa Takatifu itafanyika saa 4:00 asubuhi katika Uwanja wa Cavour, itakayoongozwa na Askofu Mkuu Rino Fisichella, mwenye jukumu la kuandaa Jubilei ya 2025. Kuingia kwa uwanja huo kutawezekana kuanzia saa 2:00 asubuhi na sherehe haihitaji aina yoyote ya tiketi. Mwishoni mwa adhimisho la Ekaristi, mahujaji wataendelea kwa maandamano hadi Uwanja wa Mtakatifu Petro, wakiwa na ala zao za muziki na sare zao. Wakati wa safari, bendi zinazoshiriki zitafanya kwa vipande vilivyochaguliwa kwa uhuru, wakitembea kwa hija kuelekea Uwanja wa Mtakatifu Petro.