Bartholomew I,tuzo ya Laudato Si’:kila tendo dhidi ya mazingira ni dhambi kubwa!
Vatican News
Katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum mjini Roma, kulifanyika Hafla ya kutoa Tuzo ya Laudato Si kutoka Shirika la Ndugu Wadogo Wafransikani (OFM), tarehe 29 Mei 2025 kwa Patriaki wa Kiekumene wa Costantinopoli, Bartholomew I, Mtaalimungu Leonardo Boff, Mtandao wa Kikanisa wa Amazonia (REPAM) na Harakati Laudato si’. Tuzo hiyo inatambua uongozi wa kipekee kama Patriaki Bartholomew I wa kiikolojia, hasa ushawishi wake mkubwa kwa Papa Francisko. Msukumo wake ulikuwa msingi wa mipango miwili mikuu: Waraka wa Laudato Si’ na kuanzishwa kwa “Siku ya Kuombea kazi ya Uumbaji Ulimwenguni,” inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Septemba. Kwa njia hiyo Wakati wa sherehe hiyo, ilibainika kuwa Papa Francisko alitaja kwa uwazi kuwa ni “Patriaki wa Kijani” katika juhudi zote mbili.
Katika hotuba yake ya kukubalika, Patriaki wa Kiekumene aliakisi hatua muhimu ya kiekumene iliyowakilishwa na kupitishwa kwa Kanisa Katoliki kwa sherehe ya Septemba 1. Shukrani kwa maana yake ya kina ya ishara na mizizi ya zamani katika tamaduni ya Kiorthodox, umaarufu unaokua wa siku hiyo unahimiza madhehebu mengine mengi ya Kikristo kuiunganisha katika kalenda zao za kiliturujia. Patriaki Bartholomew I alichukua jukumu muhimu katika kukuza na kusaidia maendeleo haya ya kiekumene, kama ilivyokubaliwa wakati wa hafla hiyo. Kisha alitoa kauli yenye nguvu: “Ikiwa hakuna uongofu wa kweli wa kibinadamu, mgogoro wa kiikolojia hauwezi kutatuliwa. Kitendo chochote cha kibinadamu kinachoharibu mazingira lazima kihesabiwe kuwa dhambi kubwa."
Sherehe ya kihistoria
Sherehe hiyo, ambayo pia ilimtukuza Leonardo Boff, REPAM, na Harakati ya Laudato Si’, iliambatana na kumbukumbu tatu muhimu: kumbukumbu ya miaka 800 ya Utunzi wa Wimbo wa Sifa kwa Viumbe, ukumbusho wa 10 wa Laudato Si', na ukumbusho wa 1700 wa Mtaguso wa Kwanza la Nicea. "Tuzo hizi sio shukrani tu lakini ishara za wito wa ulimwengu kwa uongofu wa ikolojia," alisema Padre Massimo Fusarelli(OFM) Mkuu wa Shirika la Wafransiskani. "Kila mpokeaji anawakilisha mwelekeo wa kipekee wa ahadi hii ya pamoja," aliongeza, akiwahimiza wote "watambue uumbaji kama zawadi kutoka kwa Mungu na kumsifu Yeye pamoja na viumbe vyote."
Uongofu unaohitajika
"Ni heshima kubwa kupokea utambuzi huu kwa kujitolea kwetu kwa ikolojia fungamani ," Patriaki Bartholomew alisema, akisisitiza kwamba tuzo hiyo ni ya Kanisa zima la Constantinopoli. Alikumbuka kwamba mapema kama miaka ya 1980, Ukristo wa Kiorthodox ulikuwa ukitoa wasiwasi juu ya shida ya hali ya tabianchi, ambayo imekuwa mbaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Na akirejea waraka wa kihistoria wa Mtangulizi wake Patriaki Dimitrios wa 1989, aliwakumbusha waliohudhuria kuwa: “Leo, tunashuhudia ukiukwaji wa asili, ambao unatumiwa vibaya si kutimiza mahitaji ya msingi ya kibinadamu bali ili kutosheleza tamaa zinazoendelea kukua za kibinadamu, zinazochochewa na falsafa kuu ya jamii ya matumizi ya hovyo. "Tangu uchaguzi wetu mwaka wa 1991, tumejaribu kuongeza ufahamu miongoni mwa Wakristo na wasio Wakristo kuhusu mgogoro wa mazingira na uhusiano wake na haki ya kijamii. Tumesisitiza mwelekeo wa kiroho wa mgogoro huu na kutoa wito wa kugunduliwa upya kwa maono ya Ekaristi ya uumbaji." "Kanisa la kwanza lilielewa wazi umuhimu wa uhusiano wa mwanadamu na uumbaji," Patriaki Bartholomew alisema. "Lakini katika historia yote, wanadamu na, nyakati fulani, makanisa yenyewe yameshindwa kufahamu uhusiano wa ndani na usioweza kuvunjwa kati ya Muumba, uumbaji, na viumbe vyote vilivyoumbwa.”
Kutoka kwa bwana hadi ndugu
“Changamoto kubwa ni kuhama kutoka kwa mawazo ya ‘mabwana wanaonyonya maumbile hadi kufikia hatua ya kuchoka, hadi yale ya ‘kaka na dada’ wanaotendeana—na viumbe vyote—kama ndugu,” alisema Leonardo Boff alipopokea tuzo yake. "Uangalifu ni mshikamano wa Kikristo unaoenea kwa viumbe vyote vya asili."
Na kwa Askofu Rafael Cob García wa Vikariate ya Kitume ya Puyo alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya REPAM. Yeye alirejea Juu ya Mwaka wa Jubilei 2025 akisema kuwa: “Tunatembea tukiwa wasafiri wenye tumaini kuelekea mbingu ambayo Mungu ametuahidi.” Lorna Gold, mkurugenzi mtendaji wa Harakati ya Laudato Si’, naye alikubali tuzo hiyo kwa niaba ya shirika lake alisema kuwa: "Tuko katika hatua ya mabadiliko ya kiikolojia ambayo imekuwa shida kubwa ya dhamiri," alisema. "Kama watu wa imani, lazima tuungane ili kubadilisha wakati huu wa giza kuwa Kairos-wakati wa fursa takatifu."