杏MAP导航

Tafuta

Ask.Mkuu Auza:Papa azungumzia juu ya AI,amani,familia,uhamiaji!

Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Ulaya alikutana na Papa Leo XIV,Mei 23:"Tuligusia masuala yote makuu pamoja naye.” Pamoja na vita nchini Ukraine,askofu mkuu alisema,baadhi ya mipasuko imefichuliwa,hasa juu ya suala la ulinzi."Kuhusu uhamiaji,Kanisa linadumisha msimamo wa mshikamano,wa kusaidia zaidi ya wahanga wote wa vita na biashara haramu ya binadamu.”

Na Luca Collodi – Vatican.

Ulikuwa ni mkutano wa kina zaidi na ndivyo  alieleza Askofu Mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican wa Umoja wa Ulaya, katika mutano kwenye Jumba la Kitume la Vatican alikutan na Baba Mtakatifu Leo XIV mjini Vatican. "Yalikuwa mabadilishano ya haraka sana ya maoni, lakini wakati huo huo mazungumzo makali sana," alisema Askokofu  Mkuu akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican.

Mheshimiwa Auza, ulizungumza nini na Papa?

Tuligusa masuala yote makuu: tulizungumza juu ya Akili Nunde, maombi ya kufutwa kutoka katika kitabu cha Ubatizo, masuala yanayohusiana na uhamiaji, familia, hali ya idadi ya watu, hasa katika sehemu ya magharibi ya Jumuiya ya Ulaya.

Je, Umoja wa Ulaya una nguvu ya umoja kuwa daraja la amani katika mgogoro wa Urusi na Kiukraine?

Nimeanza utume wangu katika Umoja wa Ulaya, ingawa nimeishi miaka 18 huko Ulaya, katika nchi tano na kama Balozi wa Kitume. Kwa hiyo ninajibu kutokana na kile tulichoona na kusikia katika majuma ya  mwisho, hasa kwa kuwasili kwa utawala mpya wa Marekani ambao unadai zaidi kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya ulinzi wa Ulaya.

Baadhi ya mipasuko imefichuka, mipasuko midogo midogo, hasa kwenye masuala madhubuti kama vile asilimia ya Pato la Taifa au ya bajeti ya kila mwaka ya kila nchi kwa ajili ya ulinzi, yaani ni kiasi gani nchi inaweza kuchangia katika kuulinda Muungano

Bila shaka, hili kimsingi si suala la Umoja wa Ulaya bali ni suala la NATO, kwa sababu kuna wanachama wengi wa NATO ambao si sehemu ya Umoja huo. Ni suala kuu kabisa kwa Ulaya na mambo kama bajeti ya kitaifa yanajitokeza kama kikomo. Kiukweli, Ulaya ni eneo la amani, kwa hivyo watu karibu hawakufikiria tena juu ya uwezekano kwamba nchi inaweza kushambulia au kupigana vita na nchi nyingine huru barani Ulaya.

Tatizo la idadi ya watu linaibuka Ulaya na suala la uhamiaji linajiweka kwenye mjadala ...

Masuala haya mawili hakika yana uhusiano wa karibu sana. Suala la uhamiaji linagusa suala la idadi ya watu, linagusa suala la kazi, linagusa suala la haki za kimataifa na suala la kisiasa. Tumeona jinsi hivi karibuni na sio hivi majuzi tu - katika chaguzi kila mara kuna maeneo haya ya utaifa zaidi ambayo yamefanya suala la uhamiaji kuwa moja ya mambo  msingi ya sera zao. Hili pia linagusia suala la kushuka kwa kiwango cha kuzaliwa. Katika uhamiaji, Kanisa lina nafasi maalum na muhimu kama suala la kibinadamu, la mshikamano, la kusaidia watu, hasa wahanga wa vita, biashara ya binadamu na kadhalika. Kwa upande mwingine, Kanisa pia linaheshimu kanuni, sheria, siasa za nchi mbalimbali. Kusawazisha hizi mbili ni changamoto kubwa.

Mazungumzo kati ya dini yapo wapi?

COMECE yenyewe ina uhusiano wa kufanya kazi na Makanisa ya Kiorthodox, na Makanisa ya Kiprotestanti. Ninaamini kwamba kuna usikilizaji zaidi wakati sisi sote tunajiwasilisha pamoja juu ya masuala ambayo tuna msimamo sawa. Bila shaka, kuna masuala ambayo hatuwezi hata kujionesha kama moja: Ajenda ya 2030, uhamiaji na wakimbizi, Mkataba wa Paris… Nadhani kuhusu mambo haya tunaweza kuwa na nguvu ya ushawishi zaidi ikiwa tutawasilisha misimamo yetu kama nguvu moja.

Mnamo tarehe 24 Mei 2025 ni kumbukumbu ya miaka kumi ya Laudato si’. Mazingira pia ndio kitovu cha mjadala kati ya nchi za Ulaya...

Ninadhani ni lazima kitu kifanyike. Nilikuwa mkuu wa ujumbe wa Vatican katika mazungumzo juu ya Mkataba wa Paris na mapokezi katika Jumuiya ya kimataifa yalikuwa makubwa sana. Ikiwa kumbukumbu itatumika, wakuu wa nchi wapatao 38 katika hotuba zao za ufunguzi walinukuu Laudato si’, huku wakimtaja Baba Mtakatifu. Na wakuu wa nchi kamwe hawatajwi! Hiki ni kidokezo tu cha kusema ni kiasi gani cha waraka huu umeibua shauku kati ya serikali kwa sababu sote tuko kwenye mtumbwi mmoja na lazima tukabiliane na matatizo haya kwa pamoja kwa sababu yanatuhusu sote. Kwa Kanisa ni sharti la kimaadili, ni sharti la kidini: ikiwa tunamwamini Mungu muumba wetu, katika wito wetu wa kimsingi wa kuwa waumbaji pamoja kwa maana kwamba Bwana anatukabidhi uumbaji wake huu, msingi huu ni muhimu sana.

24 Mei 2025, 16:17