ACN "Itazindua Biblia maalum ya Watoto katika muktadha wa Jubilei 30 Mei hadi Mosi Juni
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika muktadha wa Jubilei ya Familia, watoto, bibi na Babu kuanzia tarehe 30 Mei 2025 hadi tarehe Mosi Juni 2025, Toleo Maalum la Bibilia ya Watoto litazinduliwa, lililohaririwa na Maria Lazano ambalo lilichapishwa kwa asili yake kunako 1979. Tukio lenyewe litafanyika tarehe 31 Mei 2025, wakati Mfuko wa Kipapa wa Kanisa Hitaji utagawa nakala 10,000 za Biblia kwa lugha tano (kiitaliano, kiingereza, kispanyola, kifaransa na kireno) kwa washiriki wakati wa Tamasha la Familia na Mkesha wa sala katika Uwanja wa Mtakatifu Yohane huko Laterano, Roma.
Biblia imetafsiriwa kwa lugha 190
Baada ya miaka 45, ACN iliamua kupyaisha mchoro wa Biblia. Michoro yake asili, ambayo ilipendwa sana na wasomaji, na uhai unaovutia. “Wakati maudhui yanabaki kuwa aminifu kwa ujumbe asili, toleo hili jipya linalenga kurahisisha matumizi yake katika familia, katika katekesi na katika maisha ya kila siku, hasa katika mazingira ambayo upatikanaji wa nyenzo za kidini ni mdogo,” alisema hayo Padre Anton Lässer, Mkuhsika wa chama cha Kipapa cha Mfuko wa Misaada kwa Kanisa la Kimataifa hitaji (ACN). Biblia ya Mtoto imetafsiriwa katika lugha zaidi ya 190, na nakala zaidi ya milioni 51 zimechapishwa ulimwenguni pote.