Sura za Injili:Papa asimulia mikutano ya Yesu
Vatican News
Vatican News, katika fursa ya kuelekeza Sikukuu ya Pasaka, inapendekeza tena vipindi 18 vinavyounda kipindi kinachoratibiwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano(Dicastery for Communication) kwa kushirikiana na Maktaba ya Kitume ya Vatican, Makumbusho ya Vatican na Rai-Utamaduni kilichopeperushwa wakati wa Dominika ya Pasaka 2022 kwenye Chaneli ya Kwanza ya Runinga ya Taifa Italia(RaI).
Huo ni mfululizo ambao Papa Francisko anasimulia baadhi ya matukio ya Yesu, tukio la kwanza likiwa na Matayo, mtoza ushuru. Kwa njia hiyo Wahusika wa mpango huo ni Andrea Tornielli na Lucio Brunelli, studio na upigaji picha ulisimamiwa na Renato Cerisola, muziki wa asili na Michelangelo Palmacci.
“Wakati ambapo Papa anaendelea kupata nafuu na hatusikii sauti yake, hii ni namna ya pekee ya kuisikia tena na kusikiliza katika kurasa zenye kupendeza zaidi za mafundisho yake ambamo anazungumza juu ya Yesu,” anaeleza hayo Dk. Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Vatican.