Mlango Mtakatifu wa Wafamasia,Madaktari na Wafanyakazi wa Afya
Na Fabrizio Peloni – Vatican.
Huku miale ya kwanza ya jua ikianza kuchomoza kupitia Uwanja wa Pia, Karibu na Jengo la Baraza la Kipapa la Mawasiliano na kufukuza ukungu usio wa kawaida uliokuwa umeifunika jiji la Roma, ilikuwa jumuiya za kazi za Famasi ya Vatican na Kurugenzi ya Afya na Usafi (Dsi) ya mji wa Vatican ili kuzindua, Jumamosi tarehe 5 Aprili 2025 mfululizo mrefu wa maandamano ambayo yalivuka Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Vatican kwa ajili ya Jubilei ya Wagonjwa na Ulimwengu wa Kiafya. Wafanyakazi wa vyombo hivyo viwili vya Vatican walitumia fursa ya ukaribu wa maeneo yao ya kazi na Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika mahali pa kuanzia ambapo maandamano ya sala yalipitia (Via della Conciliazione), njia ya Conciliazione.
Aliyeongoza wajumbe hao - ambao Dominika waweze kushiriki kwa wingi zaidi katika Misa ya kuhitimisha Jubilei ya kitengo hicho - alikuwa mkurugenzi wa Famasia ya Vatican Ndugu Thomas Binish Mulackal, mratibu wa mpango huo, pamoja na Profesa Andrea Arcangeli na Dk. Luigi Carbone, mkurugenzi na makamu mkurugenzi wa DSI. Mtawa wa Kihindi wa Shirika la Hospitali, la Mtakatifu Yohane wa Mungu (Fatebenefratelli) alisisitiza "uzuri wa kuanza siku kama nyingine nyingi kwa njia hiyo, ambayo ilitufanya turudi mahali pa kazi na mioyo yenye amani na iliyojaa matumaini.” Akikumbuka utume wa hali ya juu "uliokabidhiwa na Mungu kwa wafanyakazi wa afya, kuhusiana na dhana kwamba tumaini halikatishi tamaa", alisema kuwa "kwetu hii inamaanisha kuwa tiba haitokani na dawa tu, bali pia na zaidi ya yote, kwa kusikiliza na kutoa tabasamu letu kwa wale watu ambao wanapaswa kukabiliana na ugonjwa kila siku".
“Kuvuka Kizingiti mlango Mtakatifu kwa pamoja ilikuwa uzoefu mkubwa, ingawa mfupi, wa maombi ya pamoja kwa walio dhaifu zaidi, na wale ambao wamekusudiwa kuwatazama wagonjwa kitaaluma," Profesa Arcangeli alisema katika suala hili. Kushiriki nafasi sawa "kwenye njia ambayo ilituleta sisi na wenzetu kwenye Mlango Mtakatifu, ilikuwa uzoefu wa nguvu kutoka kwa mtazamo wa kiroho, na tuna hakika kwamba itaturuhusu kutoa huduma bora zaidi ya utunzaji kwa wengine ambao wanajikuta katika hali dhaifu", walitoa maoni Alessandra Ottavianelli na Elena Fontana, kabla ya kurudi nyuma ya dawati la Duka la dawa wakiwa wamevaa makoti yao meupe.