Maelfu ya watu wameshiriki Mkesha wa miaka 20 tangu kifo cha Yohane Paulo II
Padre Pawe? Rytel-Andrianik na Artur Hanula - Vatican.
"Tunakumbuka wakati huo wakati watu walipiga magoti hapa kwenye uwanja huu. Wengine walikuwa wakilia, wengine walikuwa wakishangaa kwa nini ameondoka, kwa sababu ilionekana kuwa angeendelea kukaa nasi milele," alisema hayo Askofu Mkuu Tadeusz Wojda akikumbuka matukio ya miaka 20 iliyopita. "Leo tunakumbuka tukio hili la kumshukuru Mungu kwa upapa huu mkuu na mkuu sana. Ni mojawapo ya matukio makuu zaidi katika historia ya upapa," aliongeza. Kielelezo katika kumwiga Kristo na kielelezo cha uhodari kama vile Mkuu wa Kanisa la Gdańsk alivyokazia, “Yohane Paulo wa Pili, akiwa mshirika wetu mkuu, alituacha sana, na zaidi ya yote alituonesha njia ya kwenda kwa Kristo” na jinsi ya kutembea pamoja na Yesu katika maisha ya kila siku, licha ya dhiki, kuwatumikia wengine. Alisisitiza hayo katika mkesha wa usiku tarehe 2 Aprili 2025 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, kukumbuka kifo cha Mtakatifu Yohane II kilichokea miaka ishirini iliyopita. Askofu Mkuu Wojda alisema kuwa: “Alikuwa mtu wa sala, mtu wa upendo, mtu wa huduma ya daima kwa wengine,” Mtakatifu Yohane Paulo wa II pia alikuwa ni kielelezo cha ujasiri. "Katika ulimwengu wa leo, wakati mwingine inaonekana kuwa ngumu sana kukiri imani yetu. Tunakosa ujasiri, tunakosa nguvu. Wakati mwingine raha za maisha, wakati mwingine masuala mengine hurahisisha sana mtu kumsahau Mungu, alisema Rais wa Baraza la Maaskofu wa Poland. “Na hii ndiyo sababu ni muhimu kurudi kwa Papa Yohane Paulo II sio kama hisia, lakini zaidi ya yote kama mafundisho.
Sala kwa ajili ya Amani na kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko
Washiriki wa mkesha huo waliombea amani duniani, hasa nchini Ukraine, Nchi Takatifu na nchi zote za Afrika."Tunataka pia kumwomba Papa Francisko afya, ili aweze kurejesha nguvu zake na kuendelea kuliongoza Kanisa letu," Askofu Mkuu Wojda alihimiza. Pia aliomba kuombea familia na kwa sababu "tukiungwa mkono na mafundisho ya Yohane Paulo II, tunajua jinsi ya kuchagua yaliyo ya kweli, tunajua jinsi ya daima kusimama upande wa neno la Mungu na mapenzi ya Mungu. Kwa hili tunamwomba Mtakatifu Yohane Paulo II pia kwa ajili ya nchi yetu, ambayo pia iko katika shida".
Washiriki wa mkesha katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Washiriki elfu kadhaa Wakazi wa Roma na wawakilishi wa uhamiaji wa Poland walikusanyika kwa wingi kwenye mkesha huo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Tafakari wakati wa sala ya rozari iliongozwa na na kuwa na nukuu kutoka kwa mafundisho ya Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili. Tukio hilo lilihudhuriwa, miongoni mwa mengine, na Balozi wa Jamhuri ya Poland anayewakilisha nchi yake mjini Vatican, Bwana Adam Kwiatkowski, Balozi Mdogo wa Roma Bartosz Skwarczyński na Maaskofu wa Poland: Askofu Mkuu Tadeusz Wojda, Askofu Mkuu Stanis?aw Budzik, Askofu Mkuu Wiktor Skworc na Askofu Artur Miziński.
Katika mkesha huo pia alishiriki Profesa Miros?aw Kalinowski, Gambera wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Yohane Paulo II huko Lublin, Poland. Mkutano wa maombi uliandaliwa kwa ushirikiano wa Ubalozi na Shirika la Mtakatifu Stanis?aw, Bikira na Shahidi wa Roma, Ofisi ya Huduma ya Kichungaji ya Watu wa Kaskazi wanaokusanyika kwenye Patakatifu pa Mama Yetu wa Msaada wa Kudumu kwenye Njia ya Merulana Roma na katika Kanisa la Mtakatifu Nikolai huko Ostia, pamoja na Mfuko wa Vatican wa Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili. Kwaya iliyoongoza ilikuwa ni ya “Gaudium Poloniae” ya kanisa la Mtakatifu Stanis?ao, Roma.