Katika moja ya nguzo za Mtakatifu Petro,imewekwa Sanamu ya kukumbusha ukarimu
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Kando kando ya hatua za ndani za Nguzo za Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican karibu na bafu za Maskini na Zahanai ya Mama wa Huruma, vyombo muhimu vilipendwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya watu walio katika mazingira magumu zaidi, sanamu iliyoundwa na msanii Timothy Paul Schmalz wa Canada iliwekwa Jumanne tarehe 15 Aprili 2025. Hili lilitangazwa katika taarifa kwa vyombo vya habari Vatican na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambayo ilibanisha kwamba ufungaji huo wa sanamu wenye kichwa: “Kuweni Wakarimu", ni tafsiri inayoonekana kutoka aya ya Waraka kwa Waebrania: “Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo wengine waliwakaribisha Malaika pasipo kujua” (Ebr 13:2). Sanamu hii ya shaba inaleta uhai wa Maandiko Matakatifu kupitia sanaa, ikiruhusu watu kuwa na uzoefu wa kimwili na Maandiko. Mgeni, ambayeanaonekana kuishi kama mtu asiye na makao, akiwa na vitu vyake vilivyowekwa kwenye begi na fimbo inayoonesha safari ndefu, anakukaribisha ukae karibu naye.
Maana ya kazi ya kisanii
Mgeni huyu anabadilika kuwa malaika unapotazama upande wa pili wa sanamu: ukali wa nguo zake unakuwa laini, mfuko anaobeba hubadilika kuwa mbawa na kofia inageukua kuwa nywele! Kusudi la sanamu hiyo linakumbuka ujumbe uliomo katika Maandiko: sisi sote tunaalikwa kufungua mioyo yetu kwa sababu ni hapo tu ndipo tutapata uwezekano wa kuwaona wengine jinsi walivyo, watu wenye ubinadamu wao. Papa Francisko, wakati wa Katekesi ya tarehe 13 Novemba 2024, alikumbusha kwamba "kumgusa mtu maskini, kusaidia maskini, ni sakramenti katika Kanisa." Kwa kusindikizana na watu wasio na makazi, kiukweli, tunatoa "uso thabiti kwa Injili ya upendo. Kwa kuwapa makazi, chakula, tabasamu, kwa kunyoosha mikono yako bila kuogopa kuchafuliwa nao kunarudisha heshima yao na hii inagusa moyo wa ulimwengu wetu ambao mara nyingi haujali.”