Kurudi Nicea kama ndugu
Tume ya Kitaalimungu ya Kimataifa tarehe 3 Aprili 2025 imechapisha hati inayoongozwa na kauli mbiu: "Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Mwokozi,” katika kumbukizi ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kiekumene wa Nicea uliofanyika kunako mwaka (325-2025.) Hati hiyo ni ya Mkutano huo uliopita katika historia inayotangaza imani katika wokovu kwa njia ya Yesu Kristo na katika Mungu Mmoja mmoja, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni Sura nne za hati hiyo katika ishara ya kuhamasisha Umoja wa Kikristo na sinodi katika Kanisa. Katika Muktdha wa hati hiyo Mhariri wetu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ameandika tahariri yake akikazia kwamba "kurudi Nikea ni kama ndugu" ambapo anaakisi umuhimu wa Mtaguso wa kwanza kiekumene katika hati ya Tume ya Kimataifa ya Kitaalimungu. Ifuatayao ni tahariri yake:
Andrea Tornielli
Kurudi Nicea miaka 1700 baadaye, wakati wa Jubilei ya 2025, ina maana kwanza kabisa kukutana tena kama ndugu na Wakristo wote wa ulimwengu: ungamo la imani lililoibuka kutoka katika Mtaguso wa Kwanza wa kiekumene, kiukweli linashirikishwa siyo tu na Makanisa ya Mashariki, Makanisa ya Kiorthodox na Kanisa Katoliki, lakini pia ni kawaida kwa jumuiya za kikanisa zilizozaliwa kutokana na mageuzi ya Kanisa. Inamaanisha kukusanyika pamoja kama ndugu ili kuzunguka kile ambacho ni muhimu kweli kweli, kwa sababu kinachotuunganisha ni chenye nguvu zaidi kuliko kile kinachotugawanya: “Sote kwa pamoja, tunaamini katika Mungu wa Utatu, katika Kristo mwanadamu wa kweli na Mungu wa kweli, katika wokovu katika Yesu Kristo, kulingana na Maandiko yanayosomwa katika Kanisa kwa maongozi ya Roho Mtakatifu. Kwa pamoja, tunaamini katika Kanisa, ubatizo, ufufuko wa wafu, na uzima wa milele.” Hili ndilo jambo kuu la hati “Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Mwokozi” iliyochapishwa na Tume ya Kimataifa ya Kitaalimungu katika fursa ya kuadhimisha kumbukizi ya Nikea.
Mtaguso wa kwanza wa kiekumene ulikuwa, miongoni mwa malengo yake, ya kuamua tarehe ya pamoja ya kusherehekea Pasaka, suala lenye utata ambalo tayari lilikuwa katika Kanisa la karne za kwanza: Wengine waliiadhimisha pamoja na Pasaka ya Kiyahudi siku ya 14 ya mwezi wa Nisani, wengine waliiadhimisha Dominika iliyofuata Pasaka ya Kiyahudi. Nikea ilikuwa muhimu katika kutafuta tarehe ya pamoja kwa kuanzisha tarehe ya sherehe ya Pasaka kama Dominika inayofuata ya mwezi kamili wa kwanza wa majira ya kuchipua. Hali ilibadilika katika karne ya 16, kwa marekebisho ya kalenda ya Gregory XIII: Makanisa ya Magharibi leo hii huhesabu tarehe kulingana na kalenda hiyo, wakati wale wa Mashariki wanaendelea kutumia kalenda ya Julian iliyotumiwa katika Kanisa lote kabla ya mageuzi ya Gregorian. Lakini ni jambo la maana na la kinabii kwamba hasa katika kumbukizi la Nikea mwaka huu, Makanisa yote ya Kikristo yanasherehekea Pasaka siku hiyo hiyo, Dominika tarehe 20 Aprili 2025. Ishara na matumaini ya kufikia haraka iwezekanavyo ili kuanzisha pamoja tarehe inayokubaliwa na wote.
Pamoja na mkutanao ule wa kiekumene, kuna kipengele cha pili kinachofanya kurudi huko Nikea kuwa wakati unaofaa. Tayari katika muongo wa mwisho wa karne iliyopita, Kardinali wa wakati huo Joseph Ratzinger alionesha kwamba "Uariani mpya" ndio changamoto halisi kwa Ukristo, yaani, kuongezeka kwa ugumu wa kutambua umungu wa Yesu kama inavyothibitishwa katika imani ya Kikristo ya Kanisa: anazingatiwa kuwa mtu mkuu, mwanamapinduzi, mwalimu wa kipekee, lakini si Mungu. Hata hivyo, kuna hatari nyingine, ambayo pia imesisitizwa katika hati mpya, nayo ni kinyume kabisa na ile ya kipekee, yaani, inafanya iwe vigumu kuukubali ubinadamu kamili wa Kristo. Yesu anayeweza kupata uchovu, hisia za huzuni na kuachwa, pamoja na hasira. Mwana kiukweli alichagua kuuishi ubinadamu wetu kikamilifu. Ndani Yake, katika ubinadamu unaooneshwa kila wakati, katika kujiruhusu "kujeruhiwa" na ukweli, katika kuguswa kwake na mateso ya wale alikutana nao, katika kusema ndiyo kwa maombi ya maskini walioomba msaada, tunaona kuoneshwa kwa nguvu maana ya kuwa mwanadamu na wakati huo huo tunaona kuakisi nguvu za mungu ambaye aliamua kujishusha na kujiweka mtupu ili kutuweka pamoja na kutuokoa.