Jubilei ni Utamaduni:Safari ya matumaini.Rembrandt na Burnand,Roma!
Vatican News
Kuanzia tarehe 8 Aprili hadi tarehe 25 Mei 2025, Kanisa la Mtakatifu Marcel njia ya Corso, jijini Roma litakaribisha maonyesho yenye kauli: “safari ya matumaini. Rembrandt na Burnand jijini Roma,” katika kuonesha kuwa “Jubilei ni Utamaduni’ yaliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Maonesho hayo yaliyotayarishwa na Padre Alessio Geretti, yanajikita kuweka wazi kazi mbili zenye umuhimu mkubwa kuhusu: Mitume Petro na Yohane, wanaokimbia pamoja kuelekea katika Kaburi la Kristo, asubuhi ya Ufufuko, wa Bwana wetu Yesu Kristo iliyochorwa na Eugène Burnand(1898) na nyinginge inahusu kujionesha kwa Yesu katika “Chakula huko Emau, iliyochorwa na Rembrandt Harmenszoon Van Rijn (1629). Picha mbili hizi ni muhimu sana zilizochorwa ulimwenguni zikionesha siku ya Pasaka, yaani siku ya ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo kutoka katika wafu.
Kazi ya Burnand: Mitume Petro na Yohane wakimbia kwenda Kaburini
Kazi ya Eugène Burnand, iliyo kwenye ukumbi wa Paris nchini Ufaransa ni uwakilishi wa picha ya mitume Petro na Yohane ambao walikimbia kulekea katika Kaburi asibuhi ya Pasaka. Mwanga wa jua unaoangazia eneo hilo unaashiria tumaini na kuzaliwa upya, ukipitisha mkazo wa kipekee wa kiroho. Kazi hiyo, iliyonunuliwa na Serikali ya Ufaransa, sasa imeoneshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Luxembourg, ambako inaendelea kuwavutia wageni na ujumbe wake wenye nguvu wa imani.
Kazi ya Rembrandt: ufunuo wa Yesu kwa mitume huko Emau
Kazi nzuri ya Rembrandt Harmenszoon Van Rijn, kwa upande mwingine, inasimulia historia ya wakati wa ufunuo wa Kristo mfufuka aliyotekwa kwenye mchezo wa nguvu wa mwanga na vivuli. Tukio hilo, ambalo linaelezea mkutano wa wanafunzi wawili pamoja na Yesu, linaonesha hisia kali ya kidini, ikionesha kutoonekana na fumbo la umungu. Kazi hii ya Rembrandt, ambayo haiwezi kuonekana sana nchini Italia, ni muhimu sana katika muktadha wa Jubilei. Kwa hiyo Michoro hiyo miwili itakayooneshwa jijini Roma, inatoa tafakari ya kina juu ya imani, tumaini na nguvu ya sanaa katika kusambaza ujumbe wa juu zaidi wa kiroho.
Kutembelea maonesho kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku
Tukio la uzinduzi wa tarehe 8 Aprili 2025, lililopangwa kufanyika saa 12:00 jioni, masaa ya Ulaya, bila malipo. Maonesho hayo, kuanzia tarehe 9 Aprili 2025 na kuendelea, yatakuwa wazi kwa wageni bila malipo kila siku kuanzia saa 2.00 asubuhi masaa ya Ulaya, hadi saa 2.00 usiku masaa ya Ulaya katika Kanisa la Mtakatifu Marcel njia ya Corso, kwenye Uwanja wa Mtakatifu Marcel n. 5, jijini Roma.