杏MAP导航

Tafuta

Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Mhifadhi mkuu wa Nyaraka za Kanisa na Mkutubi mkuu wa Maktaba ya Kanisa Katoliki. Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Mhifadhi mkuu wa Nyaraka za Kanisa na Mkutubi mkuu wa Maktaba ya Kanisa Katoliki.  (Vatican Media)

Askofu Mkuu Giovanni Cesare Pagazzi Mkutubi Mkuu wa Maktaba ya Kanisa Katoliki

Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi alizaliwa tarehe 8 Juni 1965 huko Jimbo Katoliki la Crema, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 23 Juni 1990 akapewa daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Lodi, Italia. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko Roma na kubahatika kufundisha Taasisi kadhaa za Kanisa Katoliki Italia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi, Mratibu wa tafiti na Profesa wa Elimu kuhusu Kanisa na Jaalimu wa Taasisi ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo wa Pili, tarehe 28 Machi 2025 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Mhifadhi mkuu wa Nyaraka za Kanisa na Mkutubi mkuu wa Maktaba ya Kanisa Katoliki. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi tarehe 30 Novemba 2023 aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na kumpandisha hadhi ya kuwa ni Askofu mkuu. Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi alizaliwa tarehe 8 Juni 1965 huko Jimbo Katoliki la Crema, Kaskazini mwa Italia.

Mhifadhi mkuu wa Nyaraka za Kanisa na Mkutubi Mkuu wa Maktaba
Mhifadhi mkuu wa Nyaraka za Kanisa na Mkutubi Mkuu wa Maktaba

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 23 Juni 1990 akapewa daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Lodi, Italia. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko Roma na kubahatika kufundisha Taasisi kadhaa za Kanisa Katoliki nchini Italia. Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizobahatika kuwa nazo, Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi amekuwa ni Jaalimu katika Taasisi ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo wa Pili na pia Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya Sayansi ya Kidini ya “Sant’Agostino” Jimbo kuu la Lodi, Italia. Kuanzia mwezi Oktoba 2021 amekuwa ni Mshauri katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa.

Mkutubi Mkuu
02 Aprili 2025, 14:55