杏MAP导航

Tafuta

Sakramenti ya Upatanisho na Mungu Sakramenti ya Upatanisho na Mungu  (? Mirek Krajewski)

Kozi ya XXXV ya Toba ya kina ya Sakramenti ya upatanisho kuanzia 24-28 Machi 2025

Katika tukio la Kozi ya XXXV ya 'Foro Interno' yaani ‘Toba ya ndani’ kuanzia tarehe 24-28 machi 2025 iliyoandaliwa na Idara ya Toba ya Kitume kama ilivyo kwa kila mwaka,kwa mwaka wa Jubilei 2025 inaongozwa na mada:“Hakuna njia bora ya kumjua Mungu kuliko kujiruhusu kupatanishwa naye, tukitamani msamaha wake,”ambayo ni maneno ya Papa Francisko,inakusudia kutoa muda wa mafunzo kwa waungamishi katika muktadha huo na msamaha na amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 24 hadi 28 Machi 2025 katika Jumba la Kansela, mjini Roma, imeanza Kozi ya 35  ya  'Foro Interno' yaani Toba ya kina ya Sakramenti ya upatanisho ambayo iliyoandaliwa na Idara ya Toba ya Kitume. "Hakuna njia bora ya kumjua Mungu kuliko kujiruhusu kupatanishwa naye, tukitamani msamaha wake: Kwa hiyo tusiikane Kuungama, bali tugundue tena uzuri wa sakramenti ya uponyaji na furaha, uzuri wa ondoleo la dhambi!" ambayo ni maneno ya Papa Francisko.    Kozi hiyo inawalekea mapadre na wahusika wote wa Madaraja matakafu ambayo inafanyika kwa njia mbili, ya uwepo na kupitia mtandaoni.

Fursa mwafaka ya kujifunza masuala ya maadili, nidhamu na toba

Kwa wanaopenda kushiriki, lazima wajiandikishe katika Toovuti ya: . Ushiriki wa ana kwa ana, katika Basilika ya  Mtakatifu Lorenzo - Damaso iliyounganishwa na Jumba la Kansela, ya Toba ya Kitume ikiruhusu nafasi zenye viti  vya kukaa zaidi (viti 500). Washiriki waliosajiliwa watakuwa wanapokea kiunga cha matangazo ya moja kwa moja kupitia barua pepe muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo. Hii ni fursa ya kuwapatia mapadre wapya na walio karibu na Daraja takatifu la upadre namna ya kutafakari na kujifunza kwa njia ya malezi juu ya sakramenti ya Kitubio.  Kozi hiyo ina ushiriki wa kipekee na masuala ya maadili na kanuni, pia kutoa sasisho kubwa juu ya nidhamu ya toba, juu ya usimamizi sahihi wa sakramenti ya Kitubio na juu ya kazi maalum na uwezo Toba ya Kitume ambayo pia ni Huduma ya Kitume. 

Mada katika toleo hili la XXXV: Jumatatu 24 Machi 2025

Saaa 9.30 Jumatatu alasili, tarehe  24 Machi 2025, Jubilei: safari ya huruma, matumaini na uwongofu kwa wote itafunguliwa na Mkuu wa Idara ya Toba ya Kitume,  Kardinali Angelo De Donatis; saa 10.15 jioni mada ni :''kushughulikia mambo yaliyo ndani ya agenda ya uwezo wake  wa Idara ya  Toba ya Kitume, itakayotolewa na Askofu Mkuu  Krzysztof Józef Nykiel Afisa mkuu wa Toba ya kitume; wakati saa 17. 10 jioni: Udhibiti, ukiukwaji na vikwazo kwa uangalifu wa muungamishi na mwenye kutubu, itakayotolewa na Mosninyo Giuseppe Tonello Mshauri Mkuu wa Toba ya Kitume   saa 11: 55 jioni ni Mjadala saa 12.15 jioni, litakuwa Hitimisho.

Jumanne tarehe 25 Machi  2025 

Saa 9.30 alasili, mada zitakuwa ni: Chapa ya Sakramenti na siri. Uwiano kati ya toba ya ndani na toba ya nje itatolewa na  Monsinyo Giacomo Incitti Mkuu wa masuala ya Sheria ya Idaya ya Toba ya Kitume (Canonist) saa 10.15 jioni:  Muungamishi  na mwenye kutubu: haki na wajibu katika sakramenti ya Kitubio, na Padre Davide Cito, Profesa wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu; saa 11.10 jioni: Uzoefu wa ungamo: kategoria na masharti maalum ya wanaotubu na Padre Luis Martín Rodríguez Muñoz, O.F.M. Rais wa Toba huko Laterano.

Jumatano tarehe 26 Machi 2025

Saa 9.30 alasili, maada itakuwa ni sanaa ya kuungamisha: vidokezo na mkakati, na Padre Marco Panero, S.D.B., Mshauri  Idara ya Toba ya kitume.  Saa 11.15 jioni: Kiongozi wa kiroho katika malezi ya kikuhani, na Padre  Jaime Emilio González Magaña, S.I. Mkuu wa Taalimungu katika Idara ya Toba ya Kutume;  saa 11.10 jioni:  Uwajibaki kimaadili na kisheria katika muktadha wa Akili mnemba na Padre Ján ?a?ok, S.I. wa chuo kikuu cha Trnava, mjadala na kuhitimisha

Alhamis 27 Machi 2025

Saa 9.30 alasili, mada itakuwa ni: Liturujia ya upatanisho: toba, msamaha na malipizi na Padre Massimo Marelli, S.I. wa kitivo cha Taalimungu, Chuo kikuu cha Kipapa cha  Sardegna; saa 10.15 jioni: Zawadi ya kupata rehema kamili: Historia na maanda yake, na Padre  Andrea Cavallini wa Chuo Kikuu cha Gregorian;  Kupumzika kidogo na meza ya mduara ikiongozwa na  Askofu Mkuu Krzysztof Józef Nykiel, Afisa Mkuu wa Toba ya Kitume, na Washiriki wote wanaoweza kuingilia kati kwa maswali pia na kuhitimiswa kwa Kozi hiyo na Kardinali  Angelo De Donatis.

Jubilei ya Wamisionari wa Huruma na Kushiriki: Masaa 24 kwa Bwana 28-29 Machi 2025

Katika mkutadha huo, wa kozi, yao itafuatia, hata Jubilei ya Mapadre waliopewa jukumu kama “Wamisionari wa Huruma”, (Missionari della Misericordia) kuanzia tarehe 28 hadi 30 ambapo  na ndani ya Jubilei yao watashiriki pia Toleo la 12 lilioanzishwa tangu mwaka 2014, Baba Mtakatifu la Masaa 24 kwa akili ya Bwana. Baba Mtakatifu Francisko alichagua kwa toleo la XII  la masaa 24 kwa Bwana  kwa kauli mbiu muhimu sana katika mwaka huu wa Jubilei ya Kawaida ya 2025: “Wewe ni tumaini langu”kutoka Zaburi ya 71:5.

Toleo la Toba ya Ndani "Foro Interno"
24 Machi 2025, 14:41