Vita,silaha mpya,msaada mdogo wa kimataifa:matokeo kwa Afrika
Andrea Tornielli
Vita vilivyoanza na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine hadi sasa vimesababisha mamia ya maelfu ya waathirika na uharibifu wa sehemu kubwa ya nchi. Lakini mzozo ambao ulizuka katikati mwa Ulaya pia umeleta athari zingine kwa ulimwengu ambao ulikuwa unajitahidi kupata nafuu kuanzia dharura ya Uviko, hasa barani Afrika, bara ambalo tayari limekumbwa na maovu kama vile ufisadi ambao sasa umeenea na deni la umma ambalo limefikia viwango visivyoweza kutegemewa. Picha halisi ya ukosefu wa utulivu duniani imesababisha mashindano ya silaha, ambayo katika baadhi ya matukio yameambatana na kupunguzwa kwa fedha zinazokusudiwa kusaidia nchi zinazoendelea. Katika kumbukizi ya miaka ya mitatu ya vita, tunakumbuka pia waathiriwa hawa wa dhamana kwa ushuhuda wa wafanyakazi wa afya na waendeshaji wa Madaktari na Afrika (CUAMM), shirika la kwanza la Italia linalojitolea kukuza na kulinda afya ya watu wa Kiafrika.
"Uhusiano na vita na hasa na vita vya Ukraine upo juu ya yote kwa sababu mzozo umezidisha hali ya mfumuko wa bei" alielezea Giovanni Putoto, anayehusika na programu na utafiti wa uendeshaji wa CUAMM, ambaye kwa sasa yuko Msumbiji. "Kisichoonekana na kinachochukuliwa kuwa rahisi ni kwamba katika Afrika Mataifa hayana uwezo wa kifedha wa kulinda familia na biashara na hii ilionekana kwa usahihi wakati wa mfumuko wa bei uliosababishwa na vita vya Ukraine na kuongezeka kwa bei ya malighafi." Putoto, ambaye husafiri mbali na mbali katika Bara la Afrika alitoa mfano wa nchi ya Sierra Leone kwamba: “Kutokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta, matumizi ya mtandao wa kitaifa wa magari 90 ya wagonjwa yamepungua kwa karibu nusu. Mambo yakienda vizuri, majuma mawili kwa mwezi hufanya kazi." Mfumuko wa bei na deni la umma vina uzito mkubwa kwenye bajeti za mataifa ya Afrika. "Hapa Msumbiji, asilimia 73 ya matumizi ya umma ni ya mishahara, na si mishahara mikubwa wala wafanyakazi si zaidi ya idadi ya watu. Asilimia 20 hulipa riba ya deni.
Ni asilimia 7 tu, au hakuna chochote, huenda kwenye gharama za uendeshaji wa huduma za afya, elimu, na huduma nyingine za umma. Matokeo yake ni kwamba hospitali hazina pamba, hazina dawa ya kusafisha vidonda au damu, hazina sindano na kwa bahati mbaya mara nyingi hazina dawa muhimu pia." Uamuzi wa utawala mpya wa Marekani wa kuliondoa shirika la USAID kwa ajili ya misaada ya kimataifa umeathiri hali hii ambayo tayari ni hatari. “Ufadhili wa madawa ulidumishwa - alielezea Putoto - lakini wafanyakazi wote walifukuzwa kazi, watu 5000 walirejeshwa nyumbani Ethiopia. Dawa za kuokoa maisha zimehakikishwa, lakini chombo kizima cha usimamizi wao kinakosekana, kile cha wafanyakazi ambao zaidi ni wa mahalia."
Msimamizi wa programu ya CUAMM alikumbuka kwamba “Ethiopia iko katika hali ya kawaida, Msumbiji inajitahidi sana. Deni limeongezeka mara tatu ikilinganishwa na miaka ishirini iliyopita. Wizara ya Afya lazima iwasilishe maagizo ya Wizara ya Uchumi na haiajiri wafanyakazi. Mwaka jana (2024), madaktari 24 waliajiriwa kote Msumbiji kwa idadi ya watu milioni 27. Itakuwa si sahihi kuhusisha hali hii na vita vya Ukraine pekee. Lakini si vibaya kusema kwamba mzozo huu ulichangia kuzorota kwa jumla kwa hali barani Afrika." Serikali za Kiafrika siku zote zimekuwa zikitumia pesa nyingi katika kununua silaha, sasa taswira ya ukosefu wa utulivu wa kimataifa, pamoja na mbio za silaha za nchi za Magharibi, imesukuma nyuma na sio tu sera za ulinzi wa mazingira lakini pia zile za ushirikiano.
Katika mkutadha wa Marekani wa majuma machache yaliyopita ni ya kufurahisha zaidi lakini sio pekee kwani: “Uingereza imepunguza misaada ya kimataifa kwa 50%: Ilikuwa ni nchi ambayo iliunga mkono Sierra Leone zaidi na uingiliaji kati uliofadhiliwa moja kwa moja na wakala wa misaada wa serikali ya Uingereza kwa miundo. Uingereza pia ilikuwa nchi iliyounga mkono Sudan Kusini zaidi: sasa mfumo ambao, ingawa ulikuwa na mapungufu, ulikuwa umetoa mchango muhimu katika kusaidia mtandao wa huduma za afya na ambao ulijulikana kama "mfuko wa pamoja wa Afya" umevunjwa." Tulimfikia Alessandra Cattani kwa njia ya simu, ambaye amekuwa akifanya kazi na CUAMM kwa miaka 18 na amekuwa katika hospitali ya Rumbek, mji mkuu wa Jimbo la Ziwa (Buhayrat) la Sudan Kusini, kwa miezi mitano iliyopita. Yeye ni daktari wa upasuaji lakini anafanya kazi katika wodi ya uzazi kwa sababu hakuna gynecologist (daktari wa masuala ya uzazi.)
Hospitali ndiyo njia ya mwisho, watu wanakuja hapa baada ya miezi kadhaa ya kutegemea waganga wa kienyeji... Asubuhi ya leo mtoto aliyeanguka kutoka katika mwembe alifika akiwa na (hemoperitoneum) kutokana na wengu kupasuka: Nilieleza kwamba anahitaji kufanyiwa upasuaji kwa sababu ana damu nyingi tumboni. Lakini wazazi hawakuamini wakaenda kwa mganga wa kienyeji. Jana alifika mvulana ambaye aliumwa na nyoka Julai(2024)na ana ugonjwa wa kidonda kwenye mguu wake: tulijaribu kuuokoa kwa kuusafisha bila kuukata. Lakini baada ya kusafishwa huko naye alimkimbia kwa mganga wa kienyeji." "Kama hospitali, tumekumbwa na ucheleweshaji mwingi wa kulipa mishahara. Hata misaada ya kimataifa ilipokuwa kubwa, hali ilikuwa ya matatizo kutokana na ufisadi, sasa hali itakuwa mbaya zaidi”, alisisitiza Cattani. Wauguzi wetu wamecheleweshwa kwa miezi mitano/sita kulipa mishahara yao. Hii ilisababisha mfululizo wa mgomo na matokeo makubwa. Desemba iliyopita(2024) hospitali ilifungwa, walitulazimisha kwenda nyumbani ili tusiwafanyie kazi… Watoto wachanga katika wodi ya watoto wachanga walirudishwa nyumbani, hata wale wanaotegemea oksijeni kutokana na matatizo makubwa ya kupumua. Watoto kadhaa walikufa.
Siku moja usiku waliniita kwa dharura na baba mmoja alikuja kwangu akiwa na mtoto mikononi mwake: aliniambia kuwa anakufa kwa sababu idara ya watoto ilikuwa imefungwa na wakamwambia arudi nyumbani kwa sababu hakuna madaktari, hapakuwa na mtu anayemtibu tena." Wasiwasi kuhusu kupunguzwa kwa misaada pia unatoka Ethiopia, ambayo pamoja na wakazi wake milioni 120 ni mojawapo ya nchi zilizo na uwiano mdogo wa wafanyakazi wa afya kwa idadi ya watu. Huko Wolisso, zaidi ya kilomita mia moja kutoka Addis Ababa, mtaalamu wa ndani Flavio Bobbio anafanya kazi na CUAMM. Hospitali hiyo, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki la Ethiopia, ilishughulikia wagonjwa 72,090 kati ya vyumba vya dharura na kliniki za wagonjwa wa nje mnamo 2024; 10,162 kulazwa hospitalini, 2,397 hatua za upasuaji, 3,453 kuzaliwa, 689 kwa upasuaji. "Pamoja na kufungwa kwa USAID - anaelezea - ??kuna wasiwasi kwa sababu watu wengi pengine watafukuzwa kazi na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)nyingi za ndani au hata za kimataifa zitakuwa na matatizo makubwa. Kuna hatari kwa programu za usaidizi katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu, malaria, ambazo zote zimehakikishwa kwa hospitali yetu na ambazo tunapokea dawa na vitendanishi kutoka kwa serikali bila malipo.
Mfumo huu unaweza kusumbua, na kusababisha madhara makubwa kwa hospitali, lakini zaidi ya yote kwa wagonjwa ambao wataona msaada wao wa matibabu umezuiwa." Wafanyakazi wa Wizara ya Afya ya Ethiopia pia wanafanya kazi kwa usaidizi kutoka Marekani. "Tutalazimika kuona - anahitimisha Bobbio - ikiwa mfumo huu utakwama. Inawezekana pia kuhakikisha msaada wa dawa muhimu, lakini dawa zenyewe basi zinahitaji vifaa vyote kuletwa mahali vinapopelekwa, kuhifadhiwa, na kusambazwa vya kutosha. Kwa sababu hii, kupunguzwa kwa misaada kwa ushirikiano wa kimataifa kuna athari mbaya na muhimu kwa hali ambazo tayari ni tete."
“Vita na matokeo yake vina athari kwanza kabisa kwa sababu ikiwa unatumia pesa kununua silaha huzitumii kwa shule na hospitali - alisema Padre Dante Carraro, mkurugenzi wa CUAMM, aliyerejea kutoka Sudan Kusini - Lakini pia huathiri mioyo ya watu na kuishia kudhoofisha kila kitu. Pia ninawafikiria watu wetu waliojitolea: kuna hatari ya kutoona tena tofali ndogo zinazowekwa kila siku na kila mmoja wetu kuwa muhimu ili kujenga nzuri. Bado ni matofali haya madogo ya uzuri ambayo yanadhoofisha mantiki ya vita, ya kufungwa, ya kujali biashara yako mwenyewe." Nimerejea kutoka Sudan Kusini - anaelezea kasisi kutoka Padua - kutoka hospitali ya Rumbek ambayo tumeanzisha shule ya wakunga: mnamo Januari kulikuwa na wahitimu 80 wapya. Vijana ambao wamesoma, na badala ya kufikiria tu jinsi ya kutoroka, wanakuwa msukumo wa kujenga kipande kidogo cha amani katika nchi yao. Matofali haya madogo ya uzuri ndio njia pekee, na yanaturuhusu kuendelea kuwa na matumaini."