杏MAP导航

Tafuta

2025.02.14  Mkutano katika Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii(Casina Pio IV). 2025.02.14 Mkutano katika Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii(Casina Pio IV). 

Vatican,mkutano kuhusu mfumo wa kodi wa haki na uwazi

Mkutano huo uliandaliwa na Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii na kushuhudiwa na ushiriki wa wageni wa kitaasisi na kitaaluma kutoka sehemu mbali mbali za dunia, tarehe 14 Februari 2025.Katika hotuba ya Katibu wa Vatican,Kardinali Pietro Parolin aliiuliza swali ni nini cha kufanya ikiwa mfumo wa kodi haufanyi kazi na kuwezesha mkusanyiko wa mali mikononi mwa wachache?

William Gallone,Joseph Tulloch na Angella Rwezaula –Vatican.

Uhalali, kutopendelea na uwazi kwa maneno mengine yakimaanisha mtazamo wa Papa Francisko wa kuondokana na ukosefu wa usawa katika uwanja wa kulipa  kodi,  vilikuwa ni vipengele muhimu sana katika Hotuba ya Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akizindua kazi za mkutano, wenye mada: “Haki ya Kodi na Mshikamano - Kuelekea nyumba ya pamoja na endelevu," wa "The Independent Commission for the Reform of International Corporate Taxation" (), "Tume Huru ya Marekebisho ya Kodi ya Kimataifa ya Mashirika(ICRICT)" tarehe 13 Februari 2025 ambapo Mkutano huo uliwaona ushiriki mkubwa wa viongozi wa kimataifa, watunga sera, wasomi na wawakilishi wa mashirika ya kiraia ambao walitoa wito wa kuwa na  mageuzi ya kimataifa ya kulipa kodi ili kulinda demokrasia kutokana na utajiri wa wachache uliokithiri.  Mkutano huo uliandaliwa na Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii (PASS) kwa ushirikiano wa  Tume Huru ya Marekebisho ya Kodi ya Kimataifa ya Mashirika ya Umma (ICRIT), katika ukumbi wa Casina Pio IV, Mjini Vatican.

Haja ya marekebisho ya kodi

Hatua ya kuanzia ni rahisi: mfumo wa sasa wa kodi haufanyi kazi, umerahisisha maisha kwa mashirika ya kimataifa, na umeongeza tofauti kati ya nchi na usawa wa kijamii, huku ukiongeza kasi ya kuwasili kwa mamlaka tajiri zaidi. Kwa njia hiyo Kardinali Parolin alikumbush kuwa, "ili ukodi itumike kwa manufaa ya wote, lazima ifanywe kwa njia ya haki. Changamoto si mpya hata kidogo, lakini ni mbali na rahisi," hasa kwa sababu, kama Sr Helen Alford, rais Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii(PASS), alivyokumbuka, akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican, "juu ya mfumo wa sasa wa kodi ya kimataifa ambayo ina zaidi ya miaka mia moja na ambayo haina uwezo wa kushughulika na ulimwengu wa leo uliojaa utandawazi. Kwa hivyo, marekebisho ya kodi yanahitaji ushirikiano fulani kati ya sehemu kadhaa za jamii.”

Mkutano huko Casina Pio IV

Kwa hiyo, tarehe 13 Februari,  kazi ilifunguliwa kwa mfululizo wa salamu za kitaasisi, ikiwa ni pamoja na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez, Thabo Mbeki, Rais wa zamani wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya Juu ya Mtiririko Haramu wa Fedha kutoka Afrika, na Aminata Touré, Waziri Mkuu wa zamani wa Senegal na sasa Mwakilishi Mkuu wa Urais wa Senegal, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Li Junhua.

Kukosekana kwa usawa kunatoka wapi? Je, kodi huimarisha na kuzaliana vipi ukosefu wa usawa katika viwango vya kimataifa na kitaifa? Kwa nini ukosefu wa usawa na usawa wa kodi huweka demokrasia katika hatari? Haya yote yalikuwa ni maswali katikati ya jopo la kwanza, ambalo Profesa Joseph Stiglitz, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya uchumi mwaka 2001 na mwenyekiti mwenza wa Icrit, alijaribu kujibu, miongoni mwa mengine: "Wengi wenu mnafahamu dhana ya Adam Smith ya 'mkono usioonekana', kulingana na ambayo kufuatilia maslahi ya mtu binafsi, ikiwa kunaongozwa na mkono usioonekana, husababisha ustawi wa jamii.  Ili kufikia hili, makampuni yanaweza kuzalisha bidhaa bora ikiwa gharama ni ya chini, wanaweza kupanua nguvu zao za soko, lakini pia wanaweza kuepuka kulipa kodi. Yaani wanaweza kuchukua fursa ya elimu, miundombinu na mfumo wa sheria unaotolewa na serikali bila kuchangia."

Nchi zinazoendelea

Leo ukosefu huu wa usawa sio tu matokeo ya ukiritimba wa makampuni makubwa ya teknolojia: "Hebu tufikirie juu ya unyonyaji wa maliasili katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Amerika ya Kusini," Stiglitz aliongeza, "ambapo utajiri hutolewa kwa sehemu ya thamani yake halisi. Rasilimali hizi ni za watu wa nchi hizo, lakini hazinufaishi watu wake. Utawala wa biashara ya kimataifa unadumisha mifumo ya ukoloni mamboleo, na kuziacha nchi zinazoendelea zikiwa chini ya uzalishaji wa bidhaa zenye thamani ya chini. Na inafanya hivyo kupitia miundo ya makusudi na makubaliano ya uwekezaji ambayo hupunguza uwezo wao wa kutoza ushuru au kudhibiti kulinda afya ya umma na mazingira."

Katika mantiki hiyo, ushuhuda wa Winnie Byanyima, mhandisi na mwanasiasa wa Uganda, mkurugenzi mtendaji wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa VVU/UKIMWI (UNAIDS), alitoa mfano wa ripoti ya hivi karibuni ya  Chuo Kikuu cha Oxford ambapo mwaka 2023 utajiri wa mabilionea uliongezeka kwa dola trilioni mbili, wakati idadi ya watu maskini ilisalia bila kubadilika ikilinganishwa na 1990. "Kama mkuu wa mwitikio wa UKIMWI duniani, alibainisha kuwa nchi nyingi za Afrika zikiwa na madeni, haziwezi kuwekeza katika mifumo yao ya afya.” Baadaye, akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican, mwanaharakati huyo wa kisiasa alikumbuka "uungaji mkono mkubwa wa nchi tajiri lakini pia alionya kwamba kupungua kwa hivi karibuni kwa misaada ya kifedha, hasa uamuzi wa utawala mpya wa Marekani wa kujadili fedha zinazopatikana kwa ajili ya misheni ya kibinadamu, unatishia kuathiri matokeo yaliyopatikana hadi sasa.”

Ulimwengu mwingineo

Kwa hakika, kanuni za kiulimwengu ambazo angalau tangu Vita vya Pili vya Dunia na kuendelea, zimechochea jukumu la nchi za Magharibi duniani hivi leo zimevunjwa pakubwa. Mifano miwili juu ya yote ilitolewa. Upanuzi wa kisiasa wa kijiografia wa Marekani umeleta kutoridhika na kutokubalika kwa ndani ya nchi, kupendelea na hata kuharakisha upanuzi wa msingi wa uchaguzi wa rais wa sasa Donald Trump na hivyo ushindi wake mara mbili.  Vile vile, mtindo wa Ulaya, wenye urasimu na udhibiti wa hali ya juu, umesababisha Bara la Kale (Ulaya) kupoteza mvuto wake wa viwanda, ambao sasa umebanwa kati ya Marekani na China, na kusababisha matatizo ya kiuchumi lakini juu ya matatizo yote ya kisiasa na kijamii, ambayo ni dhahiri katika Ujerumani ambayo inajiandaa kwenda kwenye uchaguzi. Kwa hili ni lazima basi tuongeze "mabadiliko ya enzi" tunayokabiliana nayo, ambapo migogoro na mgawanyiko wa kikanda inazidi kuongezeka.

 Maswali mengi lazima yajibiwe

Je, kuna nafasi gani, ndani ya ulimwengu huu mpya, kwa kanuni za kiulimwengu zilizopitishwa kwa msingi wa mantiki ya kibinadamu na kisheria? Zaidi ya yote, wanawezaje kuwekwa katikati ya jamii ambayo inaelekea zaidi kuelekea ubinafsi? Kupitia zana gani matokeo fulani yanaweza kupatikana? Ni wadau gani watatafsiri mahitaji haya? Maswali mengi na magumu yanasalia wazi kwa sasa, lakini mkutano wa tarehe 13 Februari 2025  ulitaka kutoa nuru  juu ya haja ya kuwa na majibu ya  karibuni, ukihusisha kila mtu, mazungumzo na kuzingatia ukweli mpya ambao ulimwengu unaozidi kuwa na nguvu, hujikuta ukiwa na nguvu ambayo, hata hivyo, vita vya mfumo wa kodi ya  haki kwa wote haviwezi kutengwa.

Kwa sababu, kama alivyokumbusha Papa Francisko katika hotuba yake kwa ujumbe wa Wakala wa Mapato tarehe 31 Januari 2022: “Kodi lazima iendeleze ugawaji upya wa mali, kulinda hadhi ya maskini na wasiobahatika, ambao daima wana hatari ya kukandamizwa na wenye nguvu. Uwazi katika usimamizi wa fedha, unaotokana na kujitolea kwa wafanyakazi wengi, unadhihirisha uhuru wa moyo na kutoa mafunzo kwa watu kuwa na ari zaidi katika kulipa kodi, hasa ikiwa ukusanyaji wa kodi unachangia kuondokana na ukosefu wa usawa, kufanya uwekezaji ili kuwepo kwa kazi zaidi, kuhakikisha afya njema na elimu kwa wote, kuunda miundombinu ya kuwezesha maisha ya kijamii na uchumi.”

Mkutano Casino Pio IV
15 Februari 2025, 10:53