Ukraine,Gallagher:kutoka Vatican ni wito wa haraka wa kumaliza migogoro
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika kutimiza mwaka wa tatu wa kuanza kwa uvamizi mkubwa wa Urusi katika nchi ya Ulaya ya Mashariki, wito kutoka Vatican ni uharaka wa dharura na ambao ushughulikwe kwa pande zote zinazohusika ili kumaliza mzozo ambao katika miaka hii mitatu umesababisha mateso makubwa kwa Ukraine, na kusababisha waathiriwa wengi, wakiwemo raia wengi wasio na hatia, na kuliacha taifa likiwa na makovu ya vitendo vingi vya uharibifu. Hayo yalisemwa na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano ya Kimataifa na Mashirika ya Kimataifa, akiwa msemaji wa ujumbe na mahangaiko ya Vatican kwa washiriki wa Mkutano wa 1509 wa Baraza la Kudumu la Usalama na Ushirikiano wa Nchi za Umoja wa Ulaya (OSCE )huko mjini Vienna nchini Austria. Akizungumza kwa njia ya video, Askofu mkuu alishutumu matokeo mabaya ya kibinadamu ya miaka hii mitatu ya vita ambayo, pamoja na vifo na majeruhi, imesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu muhimu na uharibifu wa mazingira, unaozidisha zaidi mgogoro.
Kujitolea kwa watoto na wafungwa
Askofu Mkuu Gallagher alisisitiza dhamira ya Vatican ya kuwezesha urejeshwaji wa watoto na, wakati huo huo, inahimiza kuachiliwa kwa wafungwa, hasa askari na raia waliojeruhiwa vibaya. "Vita ni janga kubwa. Ni kukana ubinadamu,” alisema katika mazungumzo hayo, akirudia maneno ambayo mara nyingi hutamkwa na Papa Francisko kuwa: “Tusisahau: vita daima ni kushindwa, daima.”
Taasisi muhimu ya OSCE kwa suluhisho la haki na la kudumu
Katika mtazamo huu, Vatican inaitaka OSCE kama "taasisi muhimu katika kutafuta suluhisho la haki na la kudumu, linalozingatia sheria za kimataifa na kushirikisha pande zote kwenye mzozo.Urejesho na udumishaji wa amani, usalama na uhusiano mzuri kati ya Nchi zinazoshiriki lazima ubaki kuwa kipaumbele cha msingi" kwa Shirika ambalo, Askofu Mkuu alisisitiza, limeonesha kushindwa kabla ya kuzuia kuzuka kwa vita na kisha katika kuwezesha suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo wa Ukraine.” Hii yote, Askofu alisema, inaakisi, kwa sehemu, utashi wa kisiasa usiotosheleza wa Nchi zinazoshiriki. Walakini, haijachelewa sana kurejesha umuhimu wa Shirika kama jukwaa la kimataifa linalofaa kwa mazungumzo ya wazi na ya uaminifu, msingi wa lazima kwa njia yoyote inayofaa ya amani.
'Kurejesha roho ya Helsinki'
Na kama katika hotuba yake huko Malta kwenye Baraza la Mawaziri la 31 la OSCE, ambalo aliwahimiza wanachama kushiriki katika mazungumzo ili kuponya migawanyiko, Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka kumbukumbu ya miaka 50 ya Sheria ya Mwisho ya Helsinki. Hiyo ni, makubaliano ya majira ya kiangazi mnamo 1975 yaliyotiwa saini na Nchi thelathini na tano, kusimamisha Vita Baridi. Kutokana na ari ya makubaliano haya, Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya lilizaliwa. Na ni "roho hii ya Helsinki" ambayo Mataifa yanayoshiriki lazima yarudi katika enzi hii ya kushangaza kwa ubinadamu.
Mazungumzo yenye kujenga na kukuza ushirikiano
"Sheria ya Mwisho ya Helsinki inajumuisha wazo linaloshirikishwa na Mataifa yote yanayoshiriki kwamba amani sio kukosekana kwa vita au kudumisha usawa wa madaraka tu, bali ni matokeo ya kukuza uhusiano wa kirafiki, kushiriki katika mazungumzo ya heshima na kujenga na kukuza ushirikiano, alisema Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa. Kanuni hizi, kwa kuzingatia sheria za kimataifa na ulinzi wa haki za binadamu kwa wote ni muhimu leo hii ??kama ilivyokuwa miongo mitano iliyopita.
Wito wa Papa Desemba 2024
Kwa kumalizia, Askofu Mkuu alitoa ombi lake mwenyewe la Papa Francisko kwa ajili ya “Ukraine inayoteswa” katika Urbi et Orbi ya mnamo tarehe 24 Desemba 2024: “Milio wa silaha inyamazishwe katika Ukraine iliyokumbwa na vita! Na pawepo na ujasiri unaohitajika kufungua mlango wa mazungumzo na ishara za mazungumzo na kukutana, ili kufikia amani ya haki na ya kudumu”.