Sinodi,mkutano wa waratibu na makatibu wa Vikundi kumi vya Mafunzo
Vatican News
Kikao cha Waratibu na Makatibu wa Vikundi 10 vya Mafunzo kilifanyika majira ya asubuhi Jumanne tarehe 18 Februari 2025 kuhusu masuala yaliyojitokeza wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu. Kwa mujibu wa ujumbe kutoka Sekretarieti Kuu ya Sinodi unafahamisha kuwa “Mkutano huo ulianza kwa muda wa sala ambapo washiriki walimkumbuka Baba Mtakatifu, wakimuombea apone haraka.
Uwasilishaji wa kila mratibu
Katika taarifa hiyo tunasoma zaidi katika mawasiliano, kuwa baadaye, kila mratibu alichukua zamu kuwasilisha kazi za kikundi chake, akizingatia hasa njia iliyotumika na mafunzo (watu/mashirika) yanayohusika, muda unaotarajiwa wa utoaji wa ripoti ya kikundi, matatizo yaliyojitokeza na maswali ya wazi. Baada ya muda huu mzuri wa kushiriki, muhimu hasa kwa Vikundi hivyo vya Utafiti vinavyoshughulikia masuala ya ‘kuvuka mipaka’ Padre Giacomo Costa S.I., mshauri wa Sekretarieti Kuu, alitoa baadhi ya "vipengele muhimu kwa usawa fulani katika uandikaji wa ripoti na kwa utoaji wao".
Kusindikizana na Tume ya Kisheria
Waratibu wa vikundi walijulishwa juu ya kupatikana kwa Tume ya Kikanuni ili kusindikizana na kazi zao, hasa kwa maswali ambayo yanapaswa kugusa pia mwelekeo wa kisheria. Kardinali Mario Grech katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu aliwakumbusha washiriki haja ya kuzingatia michango hiyo ya nje ambayo bado inaweza kuwasili kupitia barua pepe (synodus@synod.va) kabla ya tarehe 31 Machi 2025, kwa Sekretarieti Kuu, kama alivyotangaza katika ufunguzi wa Kikao cha Pili cha Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu. Kama ilivyofanyika hadi sasa, michango mipya itatumwa mara moja kwa makatibu wa vikundi vinavyohusika.
Vikundi vya Utafiti
Vikundi kumi vya utafiti ni matokeo ya Kikao cha Kwanza cha Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, ambapo mfululizo wa maswali muhimu yaliibuka, kuhusu maisha na utume wa Kanisa katika mtazamo wa sinodi, ambayo Mkutano huo ulifikia makubaliano thabiti na ambayo, kwa sababu ya mada yao, yanahitaji kushughulikiwa katika kiwango cha Kanisa zima na kushughulikiwa. Vikundi kumi vya utafiti vilianzishwa mnamo Machi 2024 kufuatia Maandishi ya Papa Francisko juu ya ushirikiano kati ya Mabaraza ya Kipapa ya Curia Romana na Sekretarieti kuu ya Sinodi na Barua yake kwa Kardinali Mario Grech ambapo alimwomba Kardinali kuhakikisha kazi ya vikundi vya utafiti "kulingana na njia halisi ya sinodi" na kwa Sekretarieti Kuu "kutayarisha muhtasari wa kazi ambao unabainisha mamlaka ya vikundi kulingana na maelekezo yangu."