杏MAP导航

Tafuta

2025.02.07: Uwasilishaji wa Barua za Utambulisho za Mheshimiwa Timur Primbetov,Balozi wa Kazakhstan 2025.02.07: Uwasilishaji wa Barua za Utambulisho za Mheshimiwa Timur Primbetov,Balozi wa Kazakhstan  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa apokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Kazakhstan

Tarehe 7 Februari 2025, Papa Papa amepokea Barua za Utambulisho za Mheshimiwa Timur Primbetov,Balozi wa Kazakhstan kuwakilisha nchi yake mjini Vatican.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko,  Ijumaa tarehe 7 Februari 2025 amepokea Barua za utambulisho wa Balozi wa Kazakhstan, Mhesh. Timur Primbetov ili kuwakilisha Nchi yake Mjini Vatican.

Alizaliwa tarehe 17 Septemba 1973, ameona na ana mtoto mmoja.

Mafunzo ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Kitaifa, Al-Farabi cha Kazakhstan (1996).

Nyadhifa nyingine: ni pamoja na kuwa Katibu wa Tatu,wa  Idara ya Ulaya na Amerika, MAE (1997 - 1999), Katibu wa Tatu, na baadaye wa Pili, Balozi wa Hispania  (1999 – 2004),  Mtaalam Mkuu, Inspekta, Mkuu wa Kitengo cha Protokali za Rais wa Jamhuri ya Khazak(2004 – 2008)

Makamu Mkuu wa Ofisi ya Protokali ya Rais wa Jamhuri Khaza. (2008 – 2018); Waziri-Mshauri,Balozi wa Shirikisho la Urusi  (2018 – 2019); Balozi wa  Lettonia (2019 – 2023); Balozi wa Mexico (2023 – 2024).

07 Februari 2025, 17:39