Papa akutana na Fico,Waziri Mkuu wa Slovakia
Vatican News
Mkutano kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Slovakia,Bwana Robert Fico,Ijuma tarehe 14 Februari 2025 yalichukua muda wa nusu saa, kuanzia saa 9 hadi 9:30, aliyekaribishwa katika ukumbi wa Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican mahali ambapo Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akiendelea na shughuli zake kutokana na ugonjwa wa mkamba ambao amekuwa akiugua kwa siku kadhaa. Aliyeambatana na Waziri Mkuu ni ujumbe wa wajumbe sita, akiwemo mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 83, kama ilivyotangazwa na Fico mwenyewe tarehe 13 Februari kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Mara baada ya hapo, mkuu wa serikali ya Bratislava alihamia katika Jumba jingine la Vatican ili kufanya mkutano na Sekretarieti ya ya Vatican kwa hiyo na Kardinali Pietro Parolin, akiambatana na Monsinyo Miros?aw Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa. Taarifa ya Ofisi ya Vyombovya habari inabainisha kuwa Wakati wa majadiliano kulikuwapo na kulithibitishwa tena shukrani kwa pande zote juu ya uhusiano thabiti wa nchi mbili na kujitolea upya kwa pamoja kuhusiana na masuala ya kijamii. Katika muktadha huo, umakini maalum ulipewa kwa suala la kianthropolojia na masuala yanayohusiana na familia na elimu. Hali halisi ya kimataifa pia ilichunguzwa kwa kina, huku ikizingatia kukosekana kwa utulivu nchini Ukraine na matarajio ya amani, na vile vile juu ya makubaliano dhaifu ya Israeli na Palestina na dharuraaya kibinadamu huko Gaza.
Zawadi
Mwishoni mwa mazungumzo ya faragha, Papa, wakati wa kubadilishana zawadi za kiutamaduni, alimpatia Waziri Mkuu kazi ya kisanii ya Udongo wa Mfinyanzi inayoitwa "Huruma na Upendo", pamoja na hati za Papa, Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 2025, Kitabu cha Kuteswa kwa Ukweli, cha Wakatoliki wa Uigiriki nyuma ya Pazia la Chuma" na albam ya picha za rangi iliyochapishwa na LEV, matokeo ya mpango wa utafiti wa Taasisi ya Historia ya Kanisa ya Chuo Kikuu katoliki cha Kiukraine kuhusu maisha ya fumbo la Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kiukraine na urithi wafiadini. Waziri Fico alijibu kwa kazi ya shaba inayowaonesha Watakatifu Cyril na Methodius, Maaskofu wasimamizi wa Bara la Ulaya ambao sikukuu yao inaadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari, na mchoro wa msanii wa Slovakia anayeonesha Malaika mlinzi.
Shambulio la kupigwa risasi 2024
Hata hivyo katika ratiba ya mkuu wa serikali ya Bratislava atatembelea Chuo cha Kipapa cha Watakatifu wa Kislovakia Cyril na Methodius kilicho roma tarehe 14 Februari 2025. Mwaka 2024, mwezi wa Mei, Waziri Fico alikuwa mwathirika wa jaribio la mauaji, baada ya mkutano huko Handlova, alipigwa risasi kwenye kifua, tumbo na kiungo kimojawapo. Shambulio ambalo Papa mwenyewe pia alilikumbuka katika hotuba yake kwa bodi za wanadiplomasia wa Vatican kunako Januari iliyopita, huku akionesha kama mfano wa kusikitisha wa hali ya mashaka inayotokana na habari za uwongo ambazo huchochea chuki na kuhatarisha kuishi kwa raia na utulivu wa mataifa yote.