杏MAP导航

Tafuta

2023.09.15 Jumba la Gavana wa mji wa Vatican. 2023.09.15 Jumba la Gavana wa mji wa Vatican. 

Makatibu wakuu wawili wateuliwa katika Mji wa Vatican!

Hawa ni Monsinyo Nappa,hadi sasa alikuwa katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na wakili Puglisi-Alibrandi,hadi sasa alikuwa makamu katibu mkuu wa mji wa Vatican.Kwa Sr Petrini,Gavana kuanzia tarehe 1 Machi 2025 ana "mamlaka ya kupanga na kutoa kwa makatibu wakuu uwezo maalum au kazi fulani."

Vatican News


Papa Francisko kwa "kurekebisha Sheria ya Msingi ya Mji wa Vatican ya tarehe 13 Mei 2023, na Sheria kifungu cha CCLXXIV cha serikali ya Vatican cha tarehe 25 Novemba 2018", amewateua, kuanzia tarehe 1 Machi 2025, Makatibu Wakuu wawili wa mji wa Vatican.

Wa kwanza ni Monsinyo Emilio Nappa, ambaye hadi uteuzi alikuwa ni katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, katika Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na makanisa maalum.

Wa pili ni Giuseppe Puglisi-Alibrandi, Mlei, rais wa Shughuli za Kimisionari za Kipapa na wakili, hadi sasa alikuwa makamu Katibu wa mji wa Vatican. Uteuzi huo uliwasilishwa kupitia taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican tarehe 25 Februari 2025.

Makatibu wawili wa mji wa Vatican.
26 Februari 2025, 11:10