杏MAP导航

Tafuta

Tuombee nchi ya Lebanon. Tuombee nchi ya Lebanon. 

Kardinali Czerny:Nchini Lebanon kupeleka msaada wa Papa katika nchini inayoteseka

Kuanzia tarehe 19- 23 Februari 2025, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuhamaSisha Maendeleo fungamani ya Kibinadamu ameelekea Beirut kutembelea na kuhimiza mipango ya Kanisa mahalia na mashirika ya kibinadamu.Ratiba yake itakuwa sala katika bandari iliyoharibiwa na mlipuko.Mkutano na Mufti na kundi la wakimbizi wa Syria:"Changamoto ya wakimbizi ni kubwa,ukosefu wa usalama na watoto wengi bila hati hivyo wanakabiliwa na biashara haramu ya binadamu na ajira ya watoto.”

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Miongoni mwa safari nyingi, zilizofanywa duniani kote katika miaka ya hivi karibuni, utume nchini Lebanon ambao Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Kibinadamu, alijiandaa  kuanzia tarehe 19 - 23 Februari 2025 kuelekea katika changamoto nzito zaidi. Alisema hayo akizungumza na Mwandishi wa Vatican News kabla ya kuanza safari hiyo. Sio kwa sababu ya programu nyingi za matukio tu kama vile Mkutano Mkuu wa Mapadre na Maaskofu wa Kikatoliki wa Lebanon (APECL) na Mufti wa Tripoli (Kardinali  wa pili baada ya safari ya Katibu Vatican Parolin) bali atakuwa na mkutano na mamlaka ya juu ya kisheria ya Kiislamu nchini, lakini pia kwa athari ya kihisia ya kuona kwa karibu idadi ya watu waliochoshwa na mzozo wa kiuchumi, na mkwamo wa muda mrefu wa kisiasa na na milipuko ya mabomu ya Israeli ambayo, pamoja na kuharibu Kusini, imezidisha hali ya dharura ya watu waliohamishwa na wakimbizi.

Katika Ardhi ya Mierezi, Kardinali mjesuit kama ilivyoelezwa katika mpango uliotolewa na DSSUI - atapata muda wa maombi katika bandari ya Beirut kukumbuka mlipuko mkubwa ulitokea mnamo tarehe 4  Agosti  2020 uliosababisha maelfu ya vifo na majeruhi. Kisha, miongoni mwa ahadi nyingine zilizopangwa, atakutana na vijana wanaoshiriki katika mafunzo ya amani, kutembelea shule ambayo inakaribisha watoto wa imani tofauti na kwenda Bab al Tabbaneh, inayojulikana kama "favela ya Mediterania" kwa kiwango cha juu sana cha umaskini na utumiaji wa madawa ya kulevya. Hatimaye, atawaona baadhi ya wahamiaji, wakimbizi wa ndani na wakimbizi wanaosaidiwa na Caritas na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Jesuit (JRS). Kardinali Czerny mwenyewe alieleza maana ya safari hiyo kwenye vyombo vya habari vya Vatican, vitakavyoshiriki utume huo, akisema kwamba anaondoka akiwa na wazo moyoni mwake kwa ajili ya Baba Mtakatifu aliyelazwa katika hospitali ya Gemelli: “Tutamkabidhi yeye na kupona kwake kwa Mama Yetu wa Lebanon.

Ziara ya Lebanon
19 Februari 2025, 11:46