Kard.Roche:Mama Teresa shuhuda wa kipekee wa matumaini kwa waliobaguliwa
Kardinali Arthur Roche
Tarehe 24 Desemba 2024, siku ambayo Baba Mtakatifu Francisko alifungua mlango wa Kanisa kuu la Vatican, kuashiria mwanzo wa Mwaka wa Jubilei ya Matumaini, Baraza la Kpapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti, lilitoa Agizo kwa niaba ya Baba Mtakatifu (Rej. N. 703/24) ambayo inahusu maadhimisho ya Mtakatifu Teresa wa Calcutta, Bikira, kuandikwa katika Kalenda ya Ibada ya Kirumi mnamo Septemba 5, kama ukumbusho wa hiari. Ushirikishwaji huu, uliopendwa na Baba Mtakatifu kwa kuitikia maombi ya maaskofu, watawa na vyama vya waamini na baada ya kutafakari kwa makini mvuto wa hali ya kiroho ya Mtakatifu Teresa wa Calcutta duniani kote, una lengo la kumpendekeza kama shuhuda wa kipekee wa matumaini kwa wale ambao wamekataliwa maishani.
Pamoja na Amri hiyo, maandishi yatakayoongezwa kwenye Kalenda na vitabu vyote vya kiliturujia kwa ajili ya adhimisho la Misa na Liturujia ya Vipindi, na vilevile kwa Mashahidi wa Kirumi, yamechapishwa kwa Kilatini. Sasa ni juu ya Mabaraza ya Maaskofu kutafsiri, kuidhinisha na baada ya kuthibitishwa na Baraza hili, kuchapisha maandiko ya kiliturujia kwa ajili ya maadhimisho haya, kama inavyotarajiwa na kanuni za sasa (tazama Barua ya Kitume katika mfumo wa Motu Proprio ya Magnum principium).
Katika mahubiri yake wakati wa Adhimisho la Ekaristi Takatifu ambapo Ibada ya Kutangazwa kwa Mtakatifu Teresa wa Calcutta iliyofanyika (tarehe 4 Septemba 2016), Baba Mtakatifu Francisko alimtaja kuwa ni mtoa huruma ya kimungu ambaye, kama "chumvi" inayokoleza kwa kila kitu na "nuru" inayoangazia giza, ilienea kwa kila kitu alichotimiza. Kwa hiyo, Mtumishi huyu wa mwisho kati ya wale wa mwisho ni picha halisi ya Msamaria Mwema. “Utume wake katika viunga vya miji na mashinani,” kama Baba Mtakatifu alivyobainisha katika mahubiri yake, “unasalia katika siku zetu kama ushuhuda fasaha wa ukaribu wa Mungu kwa maskini zaidi kati ya maskini zaidi.”
Katika maandiko ya kiliturujia ya maadhimisho haya, Mkusanyiko unatufunulia moyo wa hali yake ya kiroho ya: “wito wa kukidhi kiu ya Yesu Kristo Msalabani kwa kujibu kwa upendo mahitaji ya wahitaji zaidi.” Kwa sababu hiyo, tunamwomba Mungu Baba kwamba, kwa kuiga kielelezo chake, tupate kumtumikia Kristo akiwa ndani ya kaka na dada zetu wanaoteseka.
Katika Kitabu cha Masomo, somo la kwanza ni andiko kutoka kwa nabii Isaya kuhusu kufunga kwa kumpendeza Mungu (rej. Isa 58:6-11), ikifuatiwa na Zaburi 33: “Nitamhimidi Bwana nyakati zote.” Injili, iliyotanguliwa na Aleluya, inaakisi ufunuo wa mafumbo ya Ufalme kwa wadogo (rej. Mt 11:25), na inaripoti andiko zuri la Injili kwa mujibu wa Mathayo ambalo; baada ya kuorodhesha matendo ya huruma, ina maneno yafuatayo ambayo Mama Teresa alihuisha kwa namna ya ajabu: “chochote mlichomtendea mmoja wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinifanyia mimi” (rej. Mt 25:40).
Kuhusu Liturujia ya Vipindi, baada ya maelezo ya wasifu wake, usomaji wa pili wa Masifu na Masomo ni maandishi yaliyochukuliwa kutoka katika barua ambayo Mtakatifu alimwandikia Padre Joseph Neuner mnamo 1960, ambayo, alijifungua roho yake. Yeye anadhihirisha giza la kutokuwepo kwa Mungu ambalo aliishi nalo kwa miaka mingi, lakini ambalo alimtolea Mungu kwa furaha, ili, kwa kustahimili jaribu hilo kwa uaminifu, roho nyingi zipate nuru.
Maandiko ya kiliturujia yanahitimisha kwa sifa ya Mashahidi wa Kirumi ambayo sasa yanamweka katika nafasi ya kwanza kati ya maadhimisho ya tarehe 5 Septemba yak ila mwaka. Ushirikishwaji wa maadhimisho haya katika Kalenda ya Jumla ya Kirumi utusaidie kumtafakari mwanamke huyu, mwanga wa matumaini, mdogo wa kimo lakini mkubwa katika upendo, shuhuda wa hadhi na mapendeleo ya utumishi mnyenyekevu katika kutetea maisha ya kila mwanadamu na wale wote walioachwa, kutupwa na kudharauliwa hata katika uficho wa tumbo la mama.