杏MAP导航

Tafuta

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.  

Kard Parolin:wote wachangie ujenzi wa amani ya haki na ya kudumu,hakuna misimamo ya upande mmoja

Katika mahojiano yaliyotolewa na 'Eco di Bergamo’ iliyochapishwa Februari 15,Katibu wa Vatican amezungumza juu ya usitishaji wa mapigano huko Gaza,akitumaini kuwa itakuwa ya kudumu. “Syria inapaswa kusindikizwa katika njia ya ujumuishaji na kuishi kwa usawa."Katika diplomasia,"ni muhimu kukuza mazungumzo jumuishi,uvumilivu na kujenga uaminifu kati ya sehemu mbili na kuimarisha jukumu la taasisi za kimataifa.”

Vatican News


Mkataba kati ya Hamas na Israeli, vita vya Ukraine, hali ya Syria, uwepo wa Wakristo katika Mashariki ya Kati, amani duniani, matatizo ya ukweli wa kisasa na Kanisa, matumaini ambayo uhuisha Jubilei ni baadhi ya mada zilizotamkwa na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin katika mahojiano aliyotoa kwa Alberto Ceresoli, mkurugenzi wa Gazeti la kila siku la “L’Eco di Bergamo” yaani, “Mwangwi wa Bergamo” na kuchapishwa Jumamosi tarehe 15 Februari 2025.

Swali la kwanza linahusu usitishwaji wa mapigano huko Gaza na matumaini ya kardinali kwamba inaweza kuwa ya kudumu, na kwamba inaweza kukomesha mateso ya watu wa Palestina katika Ukanda na katika maeneo mengine ya Palestina." Sasa tunahitaji kutoa ishara za matumaini kwa wote wawili: kwa Waisraeli na kwa Wapalestina." Na kuhusu Syria, "kuna haja ya kuelewa ni mwelekeo gani tunaoelekea" na kuna haja ya kusindikiza katika njia ya ujumuishaji na kuishi pamoja kwa maridhiano. Kardinali Parolin anatumaini kwamba jumuiya ya kimataifa, na hasa mataifa jirani, yataisaidia nchi hiyo kubaki katika hali ya kimaeneo, kusaidia idadi ya watu katika umaskini ambao vita vimezalisha katika miaka hii ndefu.

Wakristo katika Mashariki ya Kati

Hali ngumu ya kijamii na kisiasa katika Mashariki ya Kati inasababisha swali la jukumu ambalo Wakristo wanaweza kuwa nalo leo hii, na sio wachache, Kardinali Parolin alibainisha, lakini sehemu muhimu na ya lazima, ambayo daima imechangia maendeleo na maendeleo ya nchi zao. Kuhusu Nchi Takatifu, “kila Mkristo anapaswa kwenda huko kwa uhuru na bila vizuizi,” alisema Kardinali Parolin, bila kusahau mahali pengine patakatifu huko Misri, Lebanon, Syria na Jordan.

Amani Ukraine na duniani

Kuhusu Ukraine, hata hivyo, Katibu wa Vatican alisema kwamba "kila mtu anaweza kuchangia amani lakini kwamba masuluhisho haya hayapaswi kamwe kutekelezwa kwa njia za upande mmoja, na hatari ya kukanyaga haki za watu wote, vinginevyo hakutakuwa na amani ya haki na ya kudumu.” Na kwa upande wa Diplomasia “inahitaji mtazamo unaokwenda zaidi ya mantiki ya migogoro na kupendelea mazungumzo jumuishi, uvumilivu na kujenga uaminifu kati ya wahusika, na kwa sababu hiyo ni muhimu kuamini katika mataifa mbalimbali na kuimarisha jukumu la taasisi za kimataifa." Kardinali alisisitiza, kuwa lakini ili kujenga amani, ujasiri unahitajika, kama Papa Francisko anavyosisitiza, na pia haki na msamaha, maadili matatu ambayo yanaonekana kukosekana katika jamii ya kisasa."

Ulaya na changamoto za siku zijazo

Kwa upande wa Ulaya, basi, ili ijue jinsi ya kukabiliana na changamoto kubwa, utamaduni na biashara ambapo Kardinali Parolin alirudia kutoa onyo la Mtakatifu Yohane Paulo II, ambalo pia lilichukuliwa na Papa Francisko kuwa: ‘Ulaya, jitafute, uwe mwenyewe!’”, huku tukikabiliwa na “kutokuamini Mungu kwa vitendo, imani ya watu wengi, kutojua kusoma na kuandika kidini na dini ya ‘kujitengenezea mwenyewe’, ingawa kwa hakika kuna sababu ya kuhangaika, ni lazima pia tuangalie matukio ya kutia moyo, kama vile ombi la vijana wengi nchini Ufaransa la kutaka kubatizwa. Lakini Wakatoliki lazima wajiulize kama, kwa ushuhuda wao wenyewe, imani, matumaini na mapendo, Injili vinaendelea kuwa ‘changamoto’.

Walei katika Kanisa na Jubilei

Mada nyingine iliyochunguzwa katika mahojiano na gazeti la Bergamo ni uwepo wa walei na hasa wanawake, katika Kanisa. Kwa upande wa Kardinali, wako mstari wa mbele ambapo lazima wapate huduma halisi katika nyanja zote za kikanisa, kuanzia Parokia, pia katika kukuza miito ya kipadre.” Hatimaye, Jubilei ambapo Kardinali Parolini alisema kuwa “ni wakati wa upatanisho, kwani inahitaji toba ya dhambi na uongofu, lakini kwa hili labda safari ya kila siku, ni ile ya kugundua tena maana ya dhambi na kuwa na uzoefu wa ukombozi wa msamaha wa Bwana, hasa katika Sakramenti ya Kitubio,” alipendekeza Kardinali Parolin,
 

15 Februari 2025, 15:57